Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Jinsi utafutaji wa Airbnb unavyofanya kazi

  Zijue sababu zinazoathiri utafutaji na jinsi ya kusaidia kuongeza kiwango chako.
  Na Airbnb tarehe 1 Des 2019
  Inachukua dakika 4 kusoma
  Imesasishwa tarehe 13 Mei 2021

  Vidokezi

  • Airbnb inatumia ishara zaidi ya 100 ili kuamua namna ya kupanga matangazo kwenye matokeo ya utafutaji

  • Ili kusaidia kupandisha kiwango chako: weka bei zenye ushindani na ukubali maombi zaidi ya kuweka nafasi

  • Ili kupata tangazo lako: Linganisha vigezo vyako vya utafutaji na mipangilio ya kuweka nafasi ya tangazo lako, matakwa na tarehe zinazopatikana

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili wa kuanzisha tangazo lenye mafanikio

  Umeunda na kuchapisha tangazo zuri na sasa marafiki na familia yako wanataka kuliangalia. Wanalipataje? Na kati ya matangazo yote yaliyochapishwa, ni kwa jinsi gani algorithimu ya kiwango cha utafutaji wa Airbnb huamua tangazo jipi lionyeshwe kwa msafiri anayetafuta kwenye eneo lako? Pata maelezo kuhusu sababu zinazoshawishi kiwango cha utafutaji wa tangazo lako na uelewe jinsi ya kuhakikisha unaweza kupata tangazo lako kwenye utafutaji.

  Misingi ya utafutaji wa Airbnb

  Algorithimu ya utafutaji ya Airbnb inazingatia ishara zaidi ya 100 ili kuamua namna ya kupanga matangazo kwenye matokeo ya utafutaji. Imeundwa ili kuwaelekeza wageni kwenye matangazo wanayoyataka, kulingana na mamilioni ya mifano ya utafutaji ambao uliongoza kwenye kuweka nafasi wakati uliopita. Pia hufanywa mahususi kwa kila mgeni kulingana na sababu kama vile, mahali, safari za wakati uliopita na matangazo yaliyowekwa kwenye matamanio. Si kila ishara inapewa uzito sawa na huhitaji kuwa na tangazo kamilifu au mahali pazuri kabisa ili tangazo lako liwe na kiwango kizuri.

  Mambo muhimu 3 yanayoathiri kiwango chako

  1. Tangazo lako linawavutia wageni kwa kiasi gani
  Algorithimu ya Airbnb inazingatia ni mara ngapi wageni wanabofya kwenye tangazo lako, ni mara ngapi wageni wanajaribu kuwasiliana na wewe kutoka kwenye ukurasa wako wa tangazo na ni maombi mangapi ya kuweka nafasi unayoyakubali. Ikiwa wageni wengi zaidi wataweka tangazo lako kwenye matamanio yao, pia litakuwa na kiwango cha juu na kuna uwezekano wageni hao watalipata tena tangazo lako katika utafutaji wa siku zijazo.

  2. Bei
  Airbnb inazingatia jinsi bei ya tangazo lako ilivyo yenye ushindani kwa kulinganisha na sehemu kama yako katika eneo lako. Algorithimu ya utafutaji inazingatia jumla ya bei yako kabla ya kodi, ikiwa ni pamoja na mapunguzo yoyote au ada ya ziada. Kuweka bei yenye ushindani kunaweza kusaidia kuboresha kiwango cha utafutaji wako, kwa kuwa matangazo yenye bei nzuri katika eneo lolote huwa yanaorodheshwa mwanzoni.

  Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufanya mabadiliko kwenye bei yako

  3. Upatikanaji
  Tangazo lako litaonekana kwenye matokeo zaidi ya utafutaji ikiwa kalenda yako ina tarehe nyingi zilizo wazi, au ikiwa umewasha kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo. Kadiri unavyoweka tarehe zilizo wazi, ndivyo kunakuwa na uwezekano zaidi wa tangazo lako kuonekana kwenye utafutaji mbalimbali—ikiwa unatumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, tangazo lako litaonekana popote pale ambapo wageni watatafuta matangazo yaliyopo katika eneo lako yanayoruhusu Kuweka Nafasi Papo Hapo.

  Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasha au kuzima kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

  Kidokezi: Kujibu maombi ndani ya saa 24 kunaweza kusaidia kuboresha kiwango chako kwenye utafutaji.

  Njia nyingine za kupandisha kiwango chako

  • Tengeneza mvuto mzuri wa kwanza: Tengeneza mvuto mzuri wa kwanza: Hakikisha picha yako ya kwanza ya tangazo lako inakuwa angavu, yenye ubora wa juu, iliyokaa mlalo. Kadiri unavyopata mibofyo zaidi kutoka kwa wasafiri wenye shauku, ndivyo utakavyokuwa na kiwango cha juu kwenye matokeo ya utafutaji kadiri muda unavyokwenda. Picha ya kuvutia na ya halisi ni njia nzuri ya kuonyesha sehemu yako.
  • Kuwa mtu wa kutoa majibu: Kujibu maombi ndani ya saa 24 kunaweza kusaidia kuboresha kiwango chako kwenye utafutaji.
  • Kubali maombi ya kuweka nafasi: Kwa sababu kukataliwa unapojaribu kuweka nafasi ni uzoefu mbaya kwa wageni, kukataa tena na tena maombi ya kuweka nafasi kunaweza kuathiri kiwango chako katika utafutaji. Licha ya hayo, wakati mwingine inakuwa lazima kukataa ombi la kuweka nafasi.
  • Uwe Mwenyeji Bingwa Ingawa Airbnb haimwinui kwa njia dhahiri Mwenyeji Bingwa katika utafutaji, sababu zinazohitajika ili kuwa Mwenyeji Bingwa, kama vile ukadiriaji mzuri, kiwango cha juu cha kutoa majibu na sehemu yako kuwekewa nafasi mara kwa mara, husaidia tangazo lako kuwa na kiwango cha juu. Wageni pia wana chaguo la kuchuja matokeo yao ya utafutaji ili kuonyesha tu matangazo ya Wenyeji Bingwa.

  Kupata tangazo lako kwenye utafutaji

  Wataalamu wa usaidizi wa jumuiya ya Airbnb wanapata maswali mengi kutoka kwa wenyeji wapya ambao wanasema hawayaoni matangazo yao kwenye utafutaji. Hizi ni sababu mbili kwa nini hii inaweza kutokea:

  1. Kuna ucheleweji wa kuchapisha. Kwa kawaida kuna uchelewaji kati ya muda unaochapisha tangazo na wakati linapoonekana kwenye matokeo ya utafutaji. Ikiwa hutalipata tangazo lako ndani ya saa 24, unaweza kuwasiliana na usaidizi wa jumuiya ili kujua ni kwa nini.

  2. Utafutaji wako ni wa jumla sana. Utafutaji mpana unaojumuisha jiji zima bila kuwa na tarehe unaweza kuleta maelfu ya matokeo na tangazo lako huenda lisionekane kwenye orodha. Lakini hivi sivyo namna ambavyo wageni halisi wanatumia tovuti. Kwa hivyo fikiria kama msafiri wakati anatafuta tangazo lako: tumia tarehe maalumu, kuza ramani, au angalia vistawishi maalumu kwa kutumia vichujio, au uweke kichujio cha bei.

  Vidokezi vya kupata tangazo lako kwenye utafutaji

  • Hakikisha vigezo vyako vya utafutaji vinaoana na mipangilio na matakwa uliyoyaweka kwa ajili ya tangazo lako
  • Angalia endapo tarehe zako zinakidhi matakwa yako ya kiwango cha chini cha usiku na kwamba unatafuta tarehe ambazo zinapatikana kwenye kalenda yako
  • Hakikisha utafutaji wako haujumuishi wageni zaidi ya idadi ya juu uliyoionyesha kwenye mipangilio yako
  • Ikiwa umewasha kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo na unahitaji kwamba wageni wawe na tathmini nzuri za hapo awali kabla hawajaweka nafasi, utahitaji kuingia kwenye akaunti na upate tathmini nzuri kama mgeni wa Airbnb ili upate tangazo lako kwenye utafutaji
  • Kumbuka kwamba kila mgeni anaona arifa iliyowekwa mahususi kidogo, kulingana na historia yake ya zamani ya kuvinjari Airbnb—na kutafuta kwa kutumia kifaa tofauti au kwa kutumia dirisha fiche kunaweza kubadilisha matokeo ya utafutaji wako
  • Ikiwa tangazo lako lina kipengele maalumu—kwa mfano, ikiwa unaruhusu wanyama vipenzi—jaribu kuweka kichujio hicho kwenye utafutaji wako; unaweza usiwe kwenye orodha ya kwanza katika utafutaji wa jumla kwenye eneo lako, lakini unaweza kuwa karibu na orodha ya kwanza ya utafutaji wa sehemu ambazo zina kipengele hicho maalumu
  • Vivyo hivyo, ikiwa tangazo lako linaweza kuchukua idadi kubwa ya wageni (kama 10 au zaidi), linaweza kuonekana kwenye orodha ya kwanza kwenye utafutaji wa sehemu ambazo zinaweza kuchukua kwa mfano, wageni wanane; na kuonekana kwenye orodha ya chini ya utafutaji kwenye sehemu zinazochukua mgeni mmoja au wawili
  Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Airbnb inatumia ishara zaidi ya 100 ili kuamua namna ya kupanga matangazo kwenye matokeo ya utafutaji

  • Ili kusaidia kupandisha kiwango chako: weka bei zenye ushindani na ukubali maombi zaidi ya kuweka nafasi

  • Ili kupata tangazo lako: Linganisha vigezo vyako vya utafutaji na mipangilio ya kuweka nafasi ya tangazo lako, matakwa na tarehe zinazopatikana

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili wa kuanzisha tangazo lenye mafanikio
  Airbnb
  1 Des 2019
  Ilikuwa na manufaa?