Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Angalia zana mpya kwa ajili ya huduma yako

Simamia na ukuze biashara yako kwa kutumia programu mpya ya Airbnb.
Na Airbnb tarehe 13 Mei 2025
Imesasishwa tarehe 25 Jun 2025

Sasa huduma yako inaweza kufikia mamilioni ya watu kwenye Airbnb. Zana zetu za kiwango cha kimataifa zinakusaidia kurahisisha ratiba, kuvutia nafasi zinazowekwa, kutuma ujumbe kwa wageni, kuelewa mapato na kupata vidokezi kuhusu ukadiriaji na tathmini.

Utapata zana zilizopangwa kwenye vichupo hivi 5 wakati umeingia kwenye akaunti kama mwenyeji.

Leo

Kichupo kipya cha Leo ndicho unachokiona unapofungua programu. Unaweza kuona maelezo ya nafasi iliyowekwa kwa ufupi ili kusaidia kupanga siku yako na kutoa ukarimu wa kipekee.

  • Badilisha kwa urahisi kati ya mionekano ya nafasi ulizowekewa za sasa na zinazokaribia kisha uchuje kulingana na huduma inayotolewa.
  • Jiandikie maelezo kuhusu nafasi zilizowekwa, kama vile vikumbusho kuhusu matukio au maombi maalumu.
  • Pata vidokezi kuhusu mambo ya kufanya kwa kila nafasi iliyowekwa, kama vile kusoma tathmini na kuwashukuru wageni wako.

Kalenda

Kalenda hufanya iwe rahisi kutazama ratiba yako kila saa na kufanya marekebisho.

  • Angalia nafasi ulizowekewa zilizothibitishwa na nafasi zilizo wazi zilizobaki ili kujazwa.
  • Boresha upatikanaji wako. Unaweza kuongeza nyakati ambazo unaweza kufanya kazi nje ya saa zako za kawaida au kuzuia nyakati ambazo huwezi kufanya kazi wakati wa saa zako za kawaida. Wakati wowote unaozuia katika kalenda yako unatumika kwenye huduma zote unazotoa.
  • Oanisha kalenda zako za Airbnb na Google ili ufuatilie kila kitu katika sehemu moja.

Wageni wanaweza kuweka nafasi ya huduma papo hapo kwenye siku yoyote isiyowekewa nafasi kwenye kalenda yako, kwa hivyo ni muhimu kusasisha upatikanaji wako.

Matangazo

Kichupo cha Matangazo kinakusaidia kusimamia maelezo ya tangazo lako. Hapa ndipo unapoweka upatikanaji wako na bei na kuonyesha huduma yako kwa wageni.

  • Ainisha huduma mbalimbali zinazotolewa katika bei ya kuingia, ya kawaida na ya juu ili kuwapa wageni machaguo zaidi na kukusaidia kufikia malengo yako ya mapato.
  • Weka saa zako za kawaida zinazopatikana kwa kila huduma inayotolewa. Unaweza kuweka saa sawa kwa huduma zote zinazotolewa au nyakati tofauti kwa kila moja. Wageni hawataweza kupata na kuweka nafasi ya huduma zinazotolewa ambazo hazina saa zinazopatikana zilizowekwa.
  • Weka mapunguzo ya muda mfupi, kwa watakaowahi na kwa kikundi kikubwa ili kuwashawishi wageni kuweka nafasi.
  • Shiriki picha za tangazo zenye ubora wa juu ili kutoa wazo sahihi la huduma yako na kuwahamasisha wageni waweke nafasi.

Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Huduma kwenye Airbnb.

Ujumbe

Kichupo cha Ujumbe kinakusaidia kuwasiliana na wageni kabla, wakati na baada ya huduma. Utatuma ujumbe kwa mgeni anayeweka nafasi na wageni wowote anaowaalika kujiunga kwenye nafasi iliyowekwa.

  • Pata maelezo kuhusu mapendeleo na matarajio ya wageni mapema, ili uweze kurekebisha huduma yako ili iwafae.
  • Unda huduma mahususi unayotoa na uweke bei mahususi.
  • Shiriki video au picha ili ujitambulishe na uwape wageni wazo bora la kile unachotoa.
  • Jibu maswali ya kawaida kupitia majibu ya haraka yanayoweza kufanywa kuwa mahususi ambayo yaliandikwa mapema au uunde violezo vyako mwenyewe.
  • Ratibu majibu ya haraka ili kutuma maelezo muhimu kiotomatiki katika nyakati muhimu, kama vile wakati wa kuweka nafasi na siku moja kabla ya huduma.
  • Wasiliana na Airbnb Usaidizi au utume ujumbe kwa mwenyeji unapotumia programu kama mgeni.

Menyu inakupa ufikiaji wa mapato yako, vidokezi na mipangilio mingine. Utapata vidokezi mahususi na nyenzo zaidi ili kusaidia kukuza biashara yako ya kukaribisha wageni.

  • Angalia mapato yako na uunde ripoti mahususi kwenye dashibodi ya mapato.
  • Angalia tathmini na ukadiriaji wote wa kina wa wageni katika sehemu ya vidokezi.
  • Simamia mipangilio ya akaunti yako na upate nyenzo za kukaribisha wageni.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
13 Mei 2025
Ilikuwa na manufaa?