Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Kurekebisha bei na mipangilio yako ili kukidhi uhitaji wa eneo lako

  Pata maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kuitikia mienendo ya usafiri katika eneo lako ili uongeze kipato kupitia Airbnb.
  Na Airbnb tarehe 7 Okt 2019
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 15 Feb 2023

  Kushughulikia mabadiliko ya uhitaji kunaweza kuwa muhimu kwa mafanikio yako kama Mwenyeji. Unaweza kuongeza mapato yako kwa kufanya sehemu yako ipatikane kwenye tarehe maarufu na kurekebisha bei yako kwa ajili ya msimu, hafla za eneo husika na mielekeo ya kusafiri.

  Mwaka jana, matangazo yenye bei ambazo zilisasishwa angalau mara nne yalikuwa na zaidi ya asilimia 30 ya usiku uliowekewa nafasi kuliko yale ambayo hayakufanya hivyo.* Ili kukusaidia kuona fursa hizi, tumekusanya vidokezi na nyenzo kadhaa, pamoja na mapendekezo machache kutoka kwa Wenyeji.

  Elewa mahitaji ya eneo lako

  Anza kwa kutafuta kwenye Airbnb matangazo ya eneo lako yanayofanana na yako. Ukizingatia kwa makini jinsi na wakati ambapo Wenyeji wengine wanarekebisha bei zao kunaweza kukusaidia kujifunza kile kinachofanikiwa katika eneo lako. Baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na:

  • Mielekeo ya kila siku. Mahitaji yanaweza kubadilika kulingana na siku ya wiki, hasa kwa ukaaji wa muda mfupi. Ijumaa na Jumamosi huwa maarufu kwa wageni wanaokwenda kwa ajili ya burudani, wakati Jumapili hadi Alhamisi zinaweza kuwavutia wageni wanaosafiri kwa ajili ya biashara.

  • ya Mabadiliko ya msimu. Eneo linaweza kuathiri uhitaji, hasa katika maeneo ambayo huvutia umati wa watu katika nyakati fulani za mwaka. Kukaribisha wageni wakati wa msimu wa wageni wengi katika eneo lako kunaweza kukusaidia kuongeza kipato.

  • Matukio maalumu. Mikutano, sikukuu, na matukio mengine makubwa yanaweza kusababisha uhitaji mkubwa. Ili kufuatilia matukio ya eneo lako, wasiliana na ofisi ya utalii ya eneo lako, jiunge kwenye makundi ya mitandao ya kijamii na ujisajili kwenye tovuti kadhaa za kukatisha tiketi za matukio. Vyombo vya habari vya mahali ulipo na vyuo vikuu pia vinaweza kuwa vyanzo vizuri.

  Kabla ya kurekebisha bei zako, kumbuka kuweka upatikanaji kwenye kalenda yako ili eneo lako lipatikane unapotarajia ongezeko la uhitaji. Unaweza pia kuangalia kichupo chako cha Fursa ili kupata vidokezi kuhusu kile ambacho wageni wanatafuta katika eneo lako, ikiwemo tarehe maarufu na aina za sehemu za kukaa.

  Fanya mipangilio yako ya bei iwe mahususi

  Mara baada ya kuelewa vizuri mielekeo ya eneo lako, unaweza kuwekabei mahususi kwa ajili ya siku za wiki, wikendi na likizo, au urekebishe bei yako wakati kuna mkutano au hafla kubwa inayokuja katika eneo lako.

  Ili kujua ni nini kinachofaa zaidi kwako na kwa wageni wako, jaribu kutumia nyenzo ya kuhakiki bei. Unaweza kujumuisha maelezo mbalimbali ili kupata mchanganuo wa bei ambayo wageni watalipa na malipo utakayopokea katika hali tofauti.

  Onekana kwa kutoa mapunguzo

  Katika vipindi vya uhitaji mdogo, sehemu nyingi katika eneo lako zinaweza kosa kuwekewa nafasi. Jaribu kuwavutia wageni kwenye tangazo lako kwa kuweka promosheni au kushusha bei yako.

  Bei ya ushindani inaweza kusaidia tangazo lako liwekwe kwenye nafasi ya juu katika utafutaji na kufanya iwe rahisi kwa wageni kupata na kuweka nafasi kwenye sehemu yako. Zingatia kuweka mapunguzo kwa hali tofauti za kuweka nafasi, ikiwemo:

  • Mapunguzo kwa watakaowahi. Kufungua kalenda yako na kuweka punguzo kwa ajili ya kuweka nafasi mapema kunaweza kuwavutia wageni wanaoweka mipango mapema.

  • Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi. Kuhimiza ukaaji wa muda mrefu kwa kuwapa bei ya chini kunaweza kuondoa mapengo ya muda kati ya nafasi zinazowekwa za muda mfupi.

  • Mapunguzo ya dakika za mwisho. Kupunguza bei yako wakati tarehe ya kuingia inakaribia kunaweza kuongeza nafasi unazowekewa na kupunguza ughairi.

  Jaribu mapendekezo haya ya Wenyeji

  Kujua nini cha kutoza wakati gani linaweza kuwa jambo la sanaa kidogo. Hizi hapa ni baadhi ya mbinu ambazo Wenyeji wamezijaribu:

  • Kupanga mapema. "Kwa kawaida tunapata maombi ya kuweka nafasi kwa ajili ya mkesha wa mwaka mpya kuanzia mapema mwezi Agosti, kwa hivyo kuwa mwangalifu na uweke mapema bei zako za sikukuu.” —Branka na Silvia wa Zagreb, Koreshia

  • Kutumia mahitaji ya chini ya usiku. "Ninaweka bei za likizo kwa kiwango cha chini cha usiku nne, na Mkesha wa Mwaka Mpya ukiwa na kiwango cha juu zaidi.” —Letti wa Atascosa, Texas.
  • Kupata thamani katika vipindi ambavyo wageni si wengi. "Ninapendekeza kupunguza bei kwa misimu ambayo watumiaji si wengi ili kuweka usawa kidogo. Au kutumia muda kwa ajili ya kufanya maboresho au matengenezo, kwa kuwa mambo yatakuwa mengi tena na hutakuwa na muda.” —Sandra wa Daylesford, Australia

  • Kutarajia kufanya makosa. "Mwongozo wako bora ni endapo unawekewa nafasi na kupata tathmini nzuri.” —Jeff na Jess wa Durham, North Carolina

  * Kulingana na matangazo duniani kote (isipokuwa China, Urusi, na Ukraine) yaliyokuwa na nafasi ya usiku mmoja iliyopatikana kuanzia Januari hadi Septemba 2022 na kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki hakikuwa kimewashwa. Sababu za ziada zinaathiri idadi ya usiku uliowekewa nafasi.

  Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Airbnb
  7 Okt 2019
  Ilikuwa na manufaa?