Ruka kwenda kwenye maudhui

Tunaweza kuwa mbali, lakini tutapambana kuvuka hali hii pamoja.

Kuanzisha Matukio ya Mtandaoni

Sasa unaweza kukutana na watu ulimwenguni kote wakati unajaribu kitu kipya. Jiunge na vipindi vya video vya moja kwa moja, vyenye maingiliano vinavyoongozwa na wenyeji weledi—yote hayo bila kuondoka nyumbani.

Mkaribishe shujaa: tusaidie kuwapa makazi wahudumu wa mstari wa mbele duniani kote

Kwa kutumia sehemu za kukaa za mstari wa mbele, Airbnb inashirikiana na wenyeji wetu ili kuwapa watoa huduma za afya 100,000, wafanyakazi wa misaada, na wahudumu wa dharura sehemu za kukaa ambazo ni safi, zitakazowafanya wawe karibu na wagonjwa wao na kukaa mbali na familia zao kwa ajili ya usalama.