Chagua sera ya kughairi inayokufaa

Pata sera inayokufaa na mahitaji yako ya kukaribisha wageni.
Na Airbnb tarehe 5 Feb 2020
Inachukua dakika 4 kusoma
Imesasishwa tarehe 19 Jan 2023

Vidokezi

  • Sera sahihi ya kughairi inaweza kukusaidia kuvutia nafasi zinazowekwa unazotaka

  • Fikiria kuhusu mahitaji yako, malengo na wageni wanaofaa unapochagua sera

  • Unaweza kusasisha sera yako wakati wowote

Kuchagua sera ya kughairi kunaweza kuwa tendo la kusawazisha. Unataka kuzuia kughairi huku pia ukiendelea kuwavutia wageni na wageni wa leo wanataka uwezo zaidi wa kubadilika wanapopanga safari zao zinazokaribia.

Kwa sababu kila Mwenyeji ana mahitaji tofauti, tumeunda sera kadhaa za kughairi. Unaweza kuchagua sera za kawaida na za muda mrefu zinazokufaa zaidi.*

Sera za kawaida

Sera yako ya kawaida ya kughairi ni kwa ajili ya nafasi zilizowekwa za muda mfupi. Inatumika kwa nafasi zote zilizowekwa chini ya usiku 28 mfululizo.

  • Sera ya kughairi inayoweza kubadilika:Wageni wanaweza kughairi hadi saa 24 kabla ya kuingia na warejeshewe fedha zote nawe hutalipwa. Ikiwa wataghairi chini ya saa 24 kabla ya kuingia na wasiingie kamwe, utalipwa usiku wa kwanza. Ikiwa wataghairi baada ya kuingia, utalipwa kila usiku ambao watakaa, pamoja na usiku 1 wa ziada.
  • Sera ya kadiri ya kughairi: Wageni wanaweza kughairi hadi siku 5 kabla ya kuingia na warejeshewe fedha zote nawe hutalipwa. Ikiwa wataghairi baada ya hapo, utalipwa kila usiku ambao wanakaa, pamoja na usiku 1 wa ziada na asilimia 50 kwa siku zote ambazo hawakukaa.
  • Sera kali ya kughairi: Ili warejeshewe fedha zote, wageni lazima waghairi angalau siku 30 kabla ya kuingia. Wanaweza pia kurejeshewa fedha zote ndani ya saa 48 baada ya kuweka nafasi ikiwa kughairi kunafanyika angalau siku 14 kabla ya kuingia. Ikiwa wataghairi kati ya siku 7 hadi 30 kabla ya kuingia, utalipwa asilimia 50 kwa usiku wote. Ikiwa wataghairi chini ya siku 7 kabla ya kuingia, utalipwa asilimia 100 kwa usiku wote.
  • Sera kali ya kughairi: Ili warejeshewe fedha zote, wageni lazima waghairi ndani ya saa 48 baada ya kuweka nafasi na kughairi lazima kufanyike angalau siku 14 kabla ya kuingia. Ikiwa wataghairi kati ya siku 7 hadi 14 kabla ya kuingia, utalipwa asilimia 50 kwa usiku wote. Ikiwa wataghairi baada ya hapo, utalipwa asilimia 100 kwa usiku wote.

Sera za muda mrefu

Sera yako ya kughairi ya muda mrefu inatumika kwa nafasi zilizowekwa za usiku 28 mfululizo au zaidi. Inabatilisha sera yako ya kawaida.

  • Sera Thabiti ya kughairi ya muda mrefu: Ili warejeshewe fedha zote, wageni lazima waghairi angalau siku 30 kabla ya kuingia. Ikiwa mgeni ataghairi baada ya hapo, utalipwa asilimia 100 kwa ajili ya usiku wote uliokaliwa, pamoja na usiku 30 wa ziada. Ikiwa zimebaki chini ya usiku 30 kwenye nafasi iliyowekwa wakati mgeni anaghairi, utalipwa asilimia 100 kwa ajili ya usiku wote uliobaki.
  • Sera kali ya kughairi ya muda mfupi: Wageni wanaoghairi nafasi iliyowekwa wanaweza kurejeshewa fedha zote ikiwa tu wataghairi nafasi waliyoweka ndani ya saa 48 baada ya kuweka nafasi na angalau siku 28 kabla ya tarehe yao ya kuingia. Ikiwa mgeni ataghairi baada ya hapo, utalipwa kwa ajili ya usiku wote uliokaliwa pamoja na usiku 30 wa ziada kuanzia tarehe ya kughairi. Ikiwa mgeni ataghairi wakati zimebaki chini ya siku 30 kwenye nafasi iliyowekwa, utalipwa asilimia 100 kwa ajili ya usiku huo wote uliobaki.

Kumbuka: Ada za usafi hurejeshwa sikuzote ikiwa mgeni ataghairi kabla ya kuingia, bila kujali sera ya kughairi ya Mwenyeji. Marejesho ya ada za huduma za mgeni za Airbnb hutegemea sababu kadhaa. Pata maelezo zaidi kuhusu marejesho ya ada

Unaweza kusasisha sera yako wakati wowote ili kudhibiti muda wa mapema ambao wageni wanaweza kughairi kabla ya kuingia na kurejeshewa fedha.

Je, sera ipi inanifaa?

Inategemea jinsi ambavyo kughairi kunaweza kukuathiri wewe na biashara yako ya kukaribisha wageni. Fikiria kuhusu mahitaji na malengo yako pamoja na wageni wako bora na uchague sera inayowasaidia.

Fikiria kuchagua sera inayoweza kubadilika ikiwa:

  • Ni msimu wa wageni wachache na unataka kuwavutia wageni wanaopenda kuwa na uwezo wa kubadilika katika mipango yao ya kusafiri.
  • Ni msimu wa wageni wengi na una uhakika sehemu yako itawekewa nafasi tena iwapo mgeni ataghairi.
  • Tangazo lako liko katika eneo lenye ushindani na huna wasiwasi kuhusu kughairi kunakofanywa kwa kuchelewa.

Fikiria kuchagua sera ya kadiri ikiwa:

  • Unataka kuzuia kughairi kwa dakika za mwisho.
  • Unataka kuwa na muda wa kuwekewa nafasi nyingine ikiwa mgeni ataghairi.
  • Bado unataka kuwavutia wageni ambao mipango yao inahitaji uratibu zaidi, kama vile wasafiri wa kikazi ambao wanahitaji kuweka nafasi zinazoweza kurejeshewa fedha.

Fikiria kuchagua sera thabiti ikiwa:

  • Unataka kuepuka kughairi lakini unaweza kukubaliana na hali hiyo ikiwa utapokea ilani ya mapema kwa muda muafaka.
  • Unapenda kuwa na wakati zaidi wa kuwekewa nafasi nyingine ikiwa mgeni ataghairi.
  • Sehemu yako ina uhitaji mwaka mzima.

Kinachotofautisha sera thabiti na sera kali ni kwamba wageni bado wanaweza kurejeshewa fedha zote kupitia sera thabiti ikiwa wataghairi siku 30 kabla ya kuingia.

Fikiria kuchagua sera kali ya kughairi ikiwa:

  • Unataka kuepuka kughairi na huna muda wa kupata au kusimamia nafasi mbadala zinazowekwa.
  • Unakaribisha wageni mwenyewe na kughairi kwa dakika za mwisho kunavuruga sana ratiba yako.
  • Sehemu yako ina uhitaji mkubwa na sera kali haitawazuia wageni kuiwekea nafasi.

Baadhi ya Wenyeji hujipatia pesa zaidi kwa kuweka chaguo la kutorejeshewa fedha kwenye sera yao ya kughairi. Chaguo hilo huwaruhusu wageni kuchagua sera kali ya kughairi kwa bei iliyopunguzwa, kwa kawaida ni punguzo la asilimia 10 kwenye bei yako ya msingi. Ikiwa watajiondoa na baadaye waghairi nafasi waliyoweka, utabaki na malipo yako yote kwa usiku wote uliowekewa nafasi.

Kuchagua sera ya kughairi kunahusu kupata kile kinachokufaa wewe na wageni wako. Kumbuka tu kwamba watu wengi hutaka uwezo wa kubadilika wanaposafiri. Ili kusaidia kulinda nafasi walizoweka, jaribu kuanza na sera ya kughairi inayoweza kubadilika zaidi ambayo inasaidia utaratibu wako wa kukaribisha wageni.

Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu wa kuweka tangazo lenye mafanikio

*Sera tofauti zinatumika kwa nafasi zilizowekwa nchini Ujerumani, Italia na Korea Kusini.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Sera sahihi ya kughairi inaweza kukusaidia kuvutia nafasi zinazowekwa unazotaka

  • Fikiria kuhusu mahitaji yako, malengo na wageni wanaofaa unapochagua sera

  • Unaweza kusasisha sera yako wakati wowote
Airbnb
5 Feb 2020
Ilikuwa na manufaa?