Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Ni nini kitakachofanyika baada ya kuchapisha?

Unaweza kusasisha kalenda yako, uweke sera ya kughairi na uwekewe nafasi.
Na Airbnb tarehe 14 Jul 2022
Imesasishwa tarehe 16 Jun 2025

Hongera! Uko tayari kuchapisha tangazo lako. Wageni wataweza kupata tangazo lako lililochapishwa katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb ndani ya saa 24.

Hakikisha uko tayari kwa ajili ya nafasi zinazowekwa kwa kuchukua hatua hizi za mwisho kwenye kalenda yako na kichupo cha Matangazo.

Kuweka mipangilio ya kalenda yako

Kalenda yako imefunguliwa na inaweza kuwekewa nafasi mara tu utakapochapisha, kwa hivyo hakikisha unasasisha upatikanaji wako mara moja. Zuia tarehe zozote ambazo huwezi kukaribisha wageni. Chagua wakati tangazo lako linapatikana kwa hadi miaka 2. Unaweza pia kurekebisha mipangilio kama vile muda wa mapema ambao wageni wanaweza kuweka nafasi na muda unaohitaji kati ya nafasi zilizowekwa.

Kuunda sheria za nyumba yako

Sheria za nyumba yako huweka matarajio kwa wageni na kuwasaidia kuamua iwapo nyumba yako inafaa kwa safari yao. Unda sheria za nyumba yako kwa kuweka idadi ya juu ya wageni kwenye tangazo lako, saa za utulivu na nyakati za kuingia na kutoka.

Unaweza pia kuchagua kutoka kwenye seti ya sheria za kawaida za nyumba, kama vile iwapo unaruhusu:

  • Wanyama vipenzi
  • Matukio
  • Uvutaji sigara, uvutaji wa mvuke wa sigara za kielektroniki na sigara za kielektroniki
  • Kurekodi video na kupiga picha za kibiashara

Kuchagua sera ya kughairi

Fikiria jinsi unavyotaka kuruhusu wageni kughairi na bado warejeshewe fedha zote au sehemu ya fedha. Una chaguo la kuchagua sera za kughairi kwa nafasi zilizowekwa za chini ya usiku 28 pamoja na ukaaji wa muda mrefu wa usiku 28 au zaidi mfululizo.

Kuchagua sera inayofaa kwako kunahusu usawa. Unataka kujilinda dhidi ya ughairi wakati bado unawavutia wageni ambao wanataka uwezo wa kubadilika wanapopanga safari. Kuchagua sera ya kughairi inayoweza kubadilika zaidi kunaweza kuongeza nafasi unazowekewa.

Kuweka vistawishi zaidi

Tayari umechagua kutoka kwenye orodha fupi ya vistawishi maarufu unapounda tangazo lako. Baada ya kuchapisha, unaweza kuweka vistawishi vyako vingine kutoka kwenye orodha yetu kamili ya machaguo karibu 150.

Wageni wengi hutumia vichujio ili kutafuta nyumba zilizo na vistawishi mahususi wanavyotaka. Kukamilisha orodha yako ya vistawishi husaidia tangazo lako lionekane katika matokeo ya utafutaji na kuweka matarajio ya wageni.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
14 Jul 2022
Ilikuwa na manufaa?