Hakikisha una vifaa hivi vya kusafisha vya kutosha
Vidokezi
Hakikisha una kila kitu unachohitaji kabla ya kuanza kusafisha
Jaza tena mavazi ya kujikinga, zana za kufanyia usafi na zana za kemikali, kisha andaa zana ili wageni waweze kufanya usafi pia
Utakapokuwa umemeliza, jaza tena vifaa vya kutumia ili uweze kuwa tayari kwa ajili ya mgeni anayefuata
- Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili ili uchunguze mchakato wa kufanya usafi wa kina
Je, upo tayari kufanya usafi wako kwa kiwango cha juu? Kama sehemu ya mchakato wa hatua 5 wa Airbnb wa kufanya usafi wa kina, kwa kuzingatia kitabu cha mwongozo wa kufanya usafi, tumetengeneza orodha ya vifaa vilivyopendekezwa, kuanzia zana za kujikinga hadi bidhaa za kufanyia usafi kwa ajili ya wageni. Hivi ni baadhi ya vifaa vya kuvihifadhi ili ufanye usafi kwa ufanisi zaidi.
Mavazi ya kujikinga
Unaweza kusaidia kupunguza uwezekano wako wa kuwa katika mazingira ya viini na kemikali kwa kutumia zana zifuatazo wakati unafanya usafi:
- Glavu zinazoweza kutumika kisha kutupwa (inapendekezwa)
- Barakoa au kitambaa cha kufunika uso (inapendekezwa)
- Miwani za usalama (hiari, kwa kusafisha bafuni)
- Aproni au gauni (hiari)
- Vifuniko vya kiatu (hiari)
- Ngao ya uso (hiari)
Vifaa
Ukiwa na vifaa vya msingi, utaweza kutekeleza kwa ufanisi mchakato wa kufanya usafi wa kina. Hiki ndicho unachokihitaji:
- Ufagio na chombo cha kuzolea taka
- Ndoo (ikiwa ni lazima)
- Kifutio cha vumbi
- Mifuko ya taka
- Nguo zenye nyuzi ndogo
- Mopa
- Taulo za karatasi
- Brashi ya kusugulia
- Vifutio vya kusugulia (jikoni pekee)
- Ngazi ya kupandia (ikiwa ni lazima)
- Brashi ya choo
- Kifaa cha kunyonya vumbi
- Mifuko ya kunyonya vumbi (ikiwa ni lazima)
- Mashine ya kuosha vyombo
- Mashine ya kuosha vyombo na mashine ya kukausha
Bidhaa
Tunapendekeza utumie dawa za kuua viini na vitakasa mikono ambavyo vimesajiliwa na mashirika husika ya serikali (kwa mfanoShirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani au Shirika la Kemikali la Ulaya). Weka hifadhi:
- Bidhaa ya kusafishia sehemu mbalimbali
- Dawa ya kuua viini katika sehemu mbalimbali
- Bidhaa ya kusafishia vioo
- Dawa ya kuondoa madoa
- Sabuni ya kufulia
- Dawa ya kufulia ya kuondoa madoa
- Sabuni ya mashine ya kuoshea vyombo
- Bidhaa ya kusafishia zulia (ikiwa ni lazima)
- Bidhaa ya kusafishia sakafu
- King'arisha samani/mbao
- Bidhaa ya kusafishia oveni (jikoni tu)
- Dawa ya kuondoa grisi (jikoni tu)
- Bidhaa ya kuondolea kuvu (ikiwa ni lazima)
Kile unachohitaji kujua kuhusu kutakasa kwa kutumia dawa ya kuua viini
Labda unajiuliza iwapo bidhaa unazozitumia ni imara kiasi cha kusaidia kupunguza idadi ya viini, kama vile bakteria na virusi. Huu ni muhtasari mfupi:
- Hakikisha unatumia vitakasa mikono vilivyoidhinishwa. Tafadhali wasiliana na mashirika husika ya serikali, kama vile Shirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani (EPA) au Shirika la Kemikali la Ulaya, ili kupata orodha ya vifaa vya kufanyia usafi na dawa za kuua viini zilizoidhinishwa. Kwa mfano, nchini Marekani, bidhaa zinazopendekezwa na EPA hujumuisha vifutio vya Clorox, dawa za kunyunyuzia za Lysol na dawa nyingine za kuua viini zinazofahamika.
- Acha bidhaa hiyo ikauke kwa hewa. Ikiwa utaondoa dawa ya kuua viini kabla ya muda uliopendekezwa wa unyevu kukamilika, hakuna uhakikisho kwamba bidhaa hiyo imeua viini vilivyoandikwa kwenye lebo.
- Vifutio vya dawa ya kuua viini vinafaa.Acha sehemu zibaki kuwa na unyevu kwa muda mrefu wa kutosha—kiwango cha muda hutegemea bidhaa husika, kwa hivyo angalia lebo.
- Usitumie dawa za kuua viini ambazo hazijathibitishwa. Ingawa siki na mafuta ya asili yanaweza kuwa visafishaji vyenye ufanisi, vitu hivi havijathibitishwa kuwa ni dawa za kuua viini na mawakala wanaosimamia sheria.
- Kamwe usichanganye bidhaa za kusafishia. Kuchanganya baadhi ya bidhaa, kama vile dawa za kuondoa madoa na amonia, kunaweza kuzalisha hewa za sumu ambazo ni hatari kupumuliwa.
Vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya wageni
Tumesikia kutoka kwa wageni kuwa wanataka kuwa na uwezo wa kufanya usafi wenyewe wanapokaa kwenye sehemu yako. Wasaidie kwa kuweka akiba ya vifaa wanavyoweza kutumia, ikiwa unakaribisha familia, hakikisha unahifadhi bidhaa zozote za kufanyia usafi kwa kuweka mbali na watoto. Hiki ndicho wageni wanahitaji zaidi:
- Taulo za karatasi zinazotumiwa mara moja na kutupwa
- Bidhaa ya kusafisha sehemu mbalimbali
- Dawa ya kuua viini ya kufutia au kunyunyiza
- Kitakasa mikono cha kuua bakteria
- Sabuni ya ziada ya mkono
Ukumbusho wa usalama kutoka kwa wataalamu wetu
- Usiingie kwenye sehemu bila kuwa na zana za kujilinda zilizopendekezwa, usitumie zana za kujikinga zilizochafuka
- Hakikisha unasoma lebo zote za usalama ili uelewe jinsi ya kutumia kwa usahihi kemikali za kufanyia usafi
- Daima weka bidhaa za kemikali mbali na watoto
- Ili kusaidia kuzuia kuenea kwa viini, usiguse uso wako wakati unafanya usafi
Utakapokuwa umemaliza kufanya usafi, kumbuka kununua vifaa ambavyo vimepungua au ambavyo vinakaribia muda wake wa kuisha matumizi, kwa njia hiyo, unaweza kubadilisha na kujaza bidhaa kabla ya usafishaji unaofuata.
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina hutoa matakwa rahisi kwa ajili ya kusafisha nyumba yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutekeleza hatua hizo, tafadhali rejelea Kitabu chote cha mwongozo wa kufanya usafi cha Airbnb. Kama Mwenyeji, unaweza kuchukua hatua za ziada ili ujilinde, ulinde timu yako na wageni wako; na daima unapaswa kuomba ushauri na kufuata sheria au miongozo yoyote ya eneo husika. Airbnb haiwajibiki kwa majeraha au ugonjwa wowote unaotokana na kufuata mchakato huu wa kufanya usafi. Kwa miongozo ya kufanya usafi na sheria mahususi zinazohusu eneo lako unakokaribisha wageni, tafadhali alamisha Makala haya ya Kituo cha Msaada.
Vidokezi
Hakikisha una kila kitu unachohitaji kabla ya kuanza kusafisha
Jaza tena mavazi ya kujikinga, zana za kufanyia usafi na zana za kemikali, kisha andaa zana ili wageni waweze kufanya usafi pia
Utakapokuwa umemeliza, jaza tena vifaa vya kutumia ili uweze kuwa tayari kwa ajili ya mgeni anayefuata
- Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili ili uchunguze mchakato wa kufanya usafi wa kina