Kuweka bei yako ya kwanza
Kuweka bei yenye ushindani kunaweza kusaidia tangazo lako lionekane na kuwahimiza wageni waweke nafasi. Sikuzote unasimamia bei yako na unaweza kuibadilisha wakati wowote.
Kupanga bei kwa siku za wiki na wikendi
Kwanza unachagua bei ya msingi ya siku za wiki. Hii ndiyo bei chaguomsingi kwa usiku wote kwenye kalenda yako. Una chaguo la kuongeza malipo kwa wikendi, ambayo ni Ijumaa na Jumamosi.
Vidokezi vya bei vilivyoonyeshwa hutumia vipengele kama vile eneo, vistawishi, nafasi ulizowekewa hapo awali na bei za hivi karibuni katika eneo lako. Ikiwa ungependa kuweka bei tofauti kuliko ile inayopendekezwa, jaribu kusawazisha gharama zako na kile ambacho wageni wako tayari kulipa. Haya ni mambo machache ya kuzingatia.
- Gharama zako za kukaribisha wageni: Hizi zinaweza kujumuisha rehani, huduma, matengenezo na kodi.
- Thamani unayotoa: Zingatia kile unachoonyesha kwenye tangazo lako, kama vile vistawishi maarufu, vipengele vya ufikiaji na ukaribu na vivutio vya eneo husika.
- Jumla ya bei ambayo wageni wanalipa: Kumbuka kwamba ada zozote unazopanga kuweka, kama vile ada ya mnyama kipenzi, huathiri jumla ya bei.
Kuanza na bei ya chini kunaweza kukusaidia kuwavutia wageni wako wa kwanza na tathmini.
Kuweka mapunguzo
Promosheni na mapunguzo yanaweza kusaidia kuboresha nafasi ya tangazo lako kwenye utafutaji na kuwavutia wageni.
- Promosheni ya tangazo jipya: Toa punguzo la asilimia 20 kwenye nafasi 3 za kwanza unazowekewa ili kukusaidia kupata wageni wako wa kwanza na tathmini.
- Punguzo la dakika za mwisho: Punguza bei yako kwa nafasi zinazowekwa mahali popote kati ya siku 1 na 28 kabla ya kuingia ili kukusaidia kujaza mapengo kwenye kalenda yako.
- Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi: Mapunguzo kwa ajili ya sehemu za kukaa za muda mrefu yanaweza kusaidia kujaza kalenda yako haraka na kupunguza idadi ya wageni wanaoingia na kutoka.
Bei yako iliyopunguzwa inaonekana kando ya ile yako ya awali, ambayo imepigwa kistari.
Utaweza kufikia nyenzo zaidi za kupanga bei baada ya kuchapisha tangazo lako. Kutumia nyenzo za Airbnb kurekebisha bei yako mara kwa mara kunaweza kukusaidia kufikia malengo yako ya mapato.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.