Kuweka matarajio kwa kuweka eneo sahihi

Wageni wanahitaji kuweza kupata eneo lako kwa urahisi.
Na Airbnb tarehe 8 Mac 2023
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 8 Mac 2023

Eneo la tangazo linaweza kuchangia pakubwa katika uamuzi wa wageni wa kuweka nafasi. Na mara tu wageni wanapoweka nafasi, wanahitaji eneo lako halisi ili waingie kwa urahisi.

Kuweka eneo sahihi

Ni muhimu uonyeshe eneo sahihi kwenye tangazo lako la Airbnb. Pia ni wazo zuri kutoa taarifa hiyohiyo katika maelezo ya tangazo lako. "Ninaelezea katika maelezo ya tangazo langu mahali nyumba ilipo," anasema Juliette, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huko Nairobi, Kenya.

Unaweza tu kufanya mabadiliko kwenye anwani yako hadi ukubali nafasi ya kwanza uliyowekewa. Baada ya hapo, utahitaji kuwasiliana na Usaidizi wa Jumuiya ili kupata msaada.

Kuhakikisha kuwa wageni wanaweza kupata eneo lako

Hakuna jambo kama hilo la kuwa mahususi sana linapokuja suala la kuwaelekeza wageni kwenye eneo lako kabla ya kuingia. Juliette anashiriki na wageni alama za GPS yake. Anasema pia anashiriki maelezo halisi, kama vile rangi ya lango lake na kile kilichoandikwa juu yake.

Juliette pia anapatikana wakati wa kuingia, ikiwa wageni watapata shida ya kupata eneo hilo. "Kwa kuwa wana mawasiliano yetu, kwa kawaida wanatupigia simu wakiwa na matatizo yoyote," anasema.

Unaweza kuweka taarifa zaidi, kama vile maelezo kuhusu kitongoji na maegesho, kwenye maelezo ya tangazo lako. Pamoja na ramani, hii inaweza kusaidia wageni kujua nini cha kutarajia na kuwapa uhakika katika uamuzi wao wa kuweka nafasi.

Kuchagua eneo la jumla au mahususi

Unaweza kuchagua jinsi eneo lako linavyoonekana katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb:

  • Eneo la jumla: Ramani ya tangazo lako inaonyesha eneo linalolizunguka, ndani ya karibu nusu maili (chini ya kilomita 1) ya anwani ya mtaa.
  • Mahali mahususi: Ramani inaonyesha pini kwenye makutano ya barabara iliyo karibu, lakini haiashirii mahali halisi. Unaweza kuburuta ramani hadi pini ionyeshe mahali sahihi.

Wageni hawapokei anwani yako ya mtaa hadi nafasi waliyoweka ithibitishwe. Mpangilio chaguo-msingi ni wa eneo la jumla.

Eneo la jumla (kushoto) na eneo mahususi (kulia) yameainishwa katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb.

Kuweka taarifa zaidi

Ikiwa wageni wanatatizika kupata eneo lako, zingatia kuweka nambari za mtaa kwenye mlango wako wa mbele au taa bora kwenye njia ya kupita gari.

Wakati mwingine unaweza kuhitaji kuwa na ubunifu kidogo. "Nyumba zetu za matope ni vigumu kuzipata," anasema Keshav, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huko New Delhi, India. "Muundo wa mtaa upo tofauti kidogo. Kwa kweli utamhitaji mtu aweze kukufikisha hapo.”

Keshav amekuwa akijaribu kuangalia njia ya kufanya iwe rahisi kwa wageni kuingia bila msaada. "Tumeanza kufikiria jinsi tunavyoweza kuweka ishara kwenye barabara kuu, bango dogo ambalo ni la kudumu," anasema.

Kufikiria kwa makini kuhusu machaguo yako

Maelezo ya tangazo lako, ikiwa ni pamoja na mahali lilipo, husaidia kuweka matarajio ya wageni na kujibu maswali yao kuhusu iwapo sehemu yako inakidhi mahitaji yao. Hii inaweza kuwapa wageni uhakika zaidi katika kuweka nafasi na kukusaidia kuepuka tathmini hasi.

Kwa mfano, wageni wanaweza kutaka kukadiria umbali wa kituo cha usafiri kilicho karibu au kuthibitisha kwamba nyumba yako ya ufukweni iko karibu na mchanga. Kuchagua kuonyesha eneo mahususi katika matokeo ya utafutaji kunaweza kufanya sehemu yako ivutie zaidi.

Wakati huo huo, kuweka mpangilio wa eneo la jumla kunaweza kukusaidia kudhibiti matatizo ya faragha na usalama. Kuchagua kuonyesha eneo lililo karibu na eneo lako katika matokeo ya utafutaji kunaweza kukupa wewe na wageni wako utulivu mkubwa wa akili.

Airbnb
8 Mac 2023
Ilikuwa na manufaa?