Kuchagua picha bora za sehemu yako
Waalike wageni wachunguze tangazo lako kwa kutoa picha zenye ubora wa juu.
Na Airbnb tarehe 5 Mei 2021
Imesasishwa tarehe 28 Jun 2024
Picha zinawasaidia wageni kujiona katika nyumba yako na kuamua iwapo inakidhi mahitaji yao. Unahitaji angalau picha tano ili uanze na unaweza kuongeza zaidi baadaye.
Kamera nyingi zinaweza kupiga picha za tangazo zenye ubora wa juu, ikiwemo ile iliyo kwenye simu yako mahiri. Fuata vidokezi hivi ili kutoa mtazamo wazi wa nyumba yako:
Piga picha ya sehemu yako kwa ubora wake. Tumia mwangaza hafifu, wa asili na uangazie maelezo muhimu, ikiwemo vistawishi maarufu na vipengele vya kipekee.
- Weka kitu hicho katikati ya fremu. Piga picha za mlalo na uwashe gridi ili zikusaidie kupanga vitu. Tutapunguza picha kiotomatiki katika miraba ili zitoshee kwenye matokeo ya utafutaji ya Airbnb na kwenye tangazo lako.
- Andika maelezo mafupi. Weka maelezo ambayo picha hazionyeshi. Kwa mfano, "Meza ya kulia chakula inapanuka ili kutoshea watu 10."
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
5 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?