Bodi ya Ushauri ya Wenyeji

Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huwapa Wenyeji kiti kwenye meza ili kuwakilisha sauti ya jumuiya katika kuelekeza mustakabali pamoja na Airbnb.

Kutana na wanachama

Wenyeji hawa 23 wanawakilisha wanajumuiya wetu bora na wao ni kielelezo chema. Wao ni Viongozi wa Jumuiya, Mabalozi Wenyeji Bingwa, wanachama wa Kituo cha Jumuiya au wanajihusisha katika mipango mingine ya jumuiya kwenye Airbnb. Wanapenda sana kukaribisha wageni, wamechangia pakubwa kwenye jumuiya ya Airbnb na wana sauti muhimu tunaposonga mbele pamoja.

Dandara Buarque

Mimi ni Kiongozi wa Jumuiya na Balozi Mwenyeji Bingwa huko Maceió, Brazili. Airbnb ni shauku yangu kubwa kwa sababu inaniwezesha kuingiliana vyema na watu na tamaduni nyingi tofauti.

Dolly Duran

Mwaka 2017, nilianza kukaribisha wageni kwenye studio ndogo katika nyumba yangu huko Florida ili kunisaidia kulipa rehani. Sasa ninasimamia nyumba nyingi na ninahudumu kama Balozi Mwenyeji Bingwa, nikisaidia wenyeji wapya kuanza.

Rachel Melland

Karibu muongo mmoja baada ya kuanza kukaribisha wageni kwenye mahema ya miti kwenye shamba letu katika Hifadhi ya Taifa ya Peak District nchini Uingereza, bado ninapenda kuona furaha ya wageni wanapowasili. Mimi pia ni Balozi Mwenyeji Bingwa.

José Manuel Esquivel Ramírez

Miaka michache iliyopita, nilirejesha nyumba huko Jerez, Uhispania na nikaanza kukaribisha wageni. Sasa ninahudumu kama Kiongozi wa Jumuiya na kubuni nyumba kwa ajili ya Wenyeji wengine, nikichangia uchumi na uendelevu wa jumuiya yangu.
Tazama wasifu

Jue Murugu (Juliette)

Kukaribisha wageni kumekuwa shauku yangu tangu mwaka 2015! Kama Kiongozi wa Jumuiya na Balozi Mwenyeji Bingwa huko Nairobi, nimenyenyekezwa na ninafurahi kuona baadhi ya watu ambao nimewasaidia wakiwa Wenyeji Bingwa.
Tazama wasifu

Katie Mead

Jasura yangu ya kushangaza ya kukaribisha wageni ilianza mwaka 2014. Kama Balozi Mwenyeji Bingwa na Kiongozi wa Jumuiya, nimewasaidia Wenyeji wakazi na kutetea sheria zinazofaa katika Ziwa Arrowhead, California.
Tazama wasifu

Keshav Aggarwal

Mwaka 2019, nilianza kuandaa tukio la sanaa barabarani kupitia Airbnb jijini Delhi, India na nimeanza safari mpya ya kukaribisha wageni kwenye nyumba za kipekee za udongo. Ninafurahia kujenga uhusiano wa kitamaduni kama Kiongozi wa Jumuiya ya Kimataifa kwa ajili ya Matukio ya Mtandaoni.
Tazama wasifu

Mauricio Bernal Cruz

Kama Kiongozi mwenye fahari wa Meksiko na wa Jumuiya, ninathamini sana mahali ninapoishi na ninapenda kuwahamasisha wengine wajisikie nyumbani. Nimekuwa mwenyeji wa Airbnb tangu mwaka 2019.
Tazama wasifu

Rie Matsumura

Ninajivunia kuwakaribisha wageni kutoka tamaduni tofauti huko Okinawa, Japani tangu mwaka 2016. Nimehudumu kama Kiongozi wake wa Jumuiya tangu mwanzo, nikijitahidi kupanua fursa za kukaribisha wageni kwenye kisiwa hicho.
Tazama wasifu

Sarah Huang (Yang-Fen)

Nilianza kuwa mwenyeji huko Adelaide, Australia mwaka 2016. Sasa mimi ni Balozi Mwenyeji Bingwa na Kiongozi wa Jumuiya mwenye kauli mbiu isiyo rasmi ya Airbnb: "Kujifunza kutoka kwa wengine, kushiriki na wengine, kuwahudumia wengine."
Tazama wasifu

Tatiya Uttarathiyang

Mimi ni Kiongozi wa Jumuiya nchini Thailand ambaye ninapenda jinsi Airbnb inavyofanya ulimwengu uwe mdogo. Nilianza kukaribisha wageni mwaka 2013 kama jambo nipendalo na sasa ninakaribisha wageni na kushirikiana kukaribisha wageni kwenye nyumba na Matukio kadhaa muda wote.
Tazama wasifu

Marielle Térouinard

Kukaribisha wageni kunakuwezesha kuona ulimwengu na kwangu mimi, hilo ni jambo la ajabu. Nilijiunga na Airbnb mwaka 2013 katika kijiji kidogo karibu na Chartres, Ufaransa na sasa ni Kiongozi wa Jumuiya na mtu anayejitolea.
Tazama wasifu

Claudia Pattarini

Tangu nilipoanza kukaribisha wageni mwaka 2015, nilianzisha kundi la Jumuiya ya Airbnb ya Ziwa Como pamoja na Wenyeji wengine nchini Italia. Ninaleta ujumuishaji wa kijamii, ufikiaji wa kiuchumi na heshima kwa mazingira katika kukaribisha wageni.
Tazama wasifu

Daniel Chamillard

Nilianza kukaribisha wageni mwaka 2012 na sasa ni shauku yangu! Kama Balozi Mwenyeji Bingwa nchini Uhispania, ninawahimiza na kuwahamasisha watu wawe sehemu ya jasura hii ya kusisimua.
Tazama wasifu

Deirdre Gower

Nilianza kuandaa Matukio ya Airbnb ya ana kwa ana mwaka 2014 na nikazindua Tukio la Mtandaoni mwaka 2020. Mimi ni Kiongozi wa Jumuiya huko Cape Town, Afrika Kusini na ninatetea usafiri unaofikika.
Tazama wasifu

Delphine Bresson

Tangu mwaka 2020, nimekuwa nikikaribisha wageni katika kijiji kilicho karibu na Msitu wa Fontainebleau nchini Ufaransa. Kama kiongozi wa jumuiya yangu, ninafuatilia kikamilifu njia za kukuza utalii endelevu.
Tazama wasifu

Felicity Stevens

Nimekuwa nikiwakaribisha wageni kutoka ulimwenguni kote kwenye eneo letu linalovutia huko Sydney kwa muongo mmoja. Ninazingatia kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, kuhifadhi rasilimali na kupunguza taka.
Tazama wasifu

Jennifer Schnier

Nilianza kukaribisha wageni mwaka 2018 katika Georgian Bay Biosphere nchini Kanada, funguvisiwa la maji safi lililo kubwa zaidi ulimwenguni. Nina Tukio endelevu la usafiri na ninaonyesha suluhisho endelevu kwa ajili ya wageni.
Tazama wasifu

Kirk Brown

Nilianza kushirikiana na rafiki yangu kukaribisha wageni mwaka 2020 huko Atlanta na tukawa Wenyeji Bingwa wenye kupata faida muda mfupi baadaye. Pia niwasaidia Wenyeji wapya kwenye tovuti.
Tazama wasifu

Nadia Giordani

Nilianza kuwa Mwenyeji mwaka 2016, baada ya kujenga kijumba changu cha kwanza. Sasa ninasimamia tangazo jingine na nina fursa ya kushirikiana na Wenyeji wengine kama Kiongozi wa Jumuiya huko Atlanta.
Tazama wasifu

Pauline Aughe

Nilianza kukaribisha wageni mwaka 2015 kama njia ya kumsaidia mume wangu aliyekuwa anaugua ugonjwa unaodhoofisha. Tangu wakati huo, kukaribisha wageni kumekuwa tukio lenye kunufaisha kwa familia yetu nzima.
Tazama wasifu

Ronaldo Monge

Nilizaliwa na kulelewa huko Puerto Rico, nilianza kukaribisha wageni mwaka 2015 kwenye chumba changu cha ziada cha kulala huko Chicago. Sasa ninawaelimisha Wenyeji, wenyeji wenza, mimi ni Mwenyeji Bingwa na ninaandaa Matukio matano tofauti ya Airbnb.
Tazama wasifu

Yajaira Sosa

Maisha yangu yalihusu ukarimu kwa muda mrefu kabla ya kuanza kukaribisha wageni kwenye Airbnb mwaka 2015. Mimi ni Kiongozi wa Jumuiya katika Jamhuri ya Dominika na ninashirikiana na Wenyeji wengine.
Tazama wasifu

Nyuma ya beji

Bodi ya Ushauri ya Wenyeji ni uwakilishi anuwai na jumuishi wa jumuiya yetu ya wenyeji.
  • Miaka 129 ya jumla ya uzoefu wa kukaribisha wageni
  • Uwakilishi anuwai wa jinsia, mbari, kabila, mwelekeo wa kingono na hali ya kijamii na kiuchumi
  • Wigo kamili wa uzoefu wa maisha
  • Asili tofauti za kitamaduni, zilizo na makao katika nchi 15
  • Mabingwa katika maeneo kadhaa muhimu ya kuzingatia, ikiwemo uendelevu, uanuwai, ufikiaji na sera

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Ni nini kusudi la Bodi ya Ushauri ya Wenyeji?

Bodi ya Ushauri ya Wenyeji husaidia kushawishi sera, mipango na huduma zinazohusiana na Wenyeji. Bodi pia itatoa maoni kuhusu jinsi Mfuko wa Wenyeji wa Airbnb unavyotumiwa kusaidia jumuiya ya Wenyeji.

Ninaweza kutarajia nini kutoka kwenye Bodi ya Ushauri ya Wenyeji?

Bodi ya Ushauri ya Wenyeji inawakilisha sauti ya jumuiya ya Wenyeji kupitia uongozi wa Airbnb. Bodi ina jukumu muhimu katika kuelekeza mustakabali wa Airbnb.

Bodi ya Ushauri ya Wenyeji iliteuliwa vipi?

Wenyeji waliteuliwa kulingana na uzoefu wao, umahiri wa kukaribisha wageni na mchango mkubwa katika kuboresha jumuiya zao.