Kujiandaa kukaribisha wageni wakimbizi kupitia Airbnb.org

Pata miongozo ya kuwakaribisha watu ambao wanaanza maisha upya katika jumuiya yako.
Na Airbnb tarehe 29 Ago 2019
Inachukua dakika 5 kusoma
Imesasishwa tarehe 25 Ago 2023

Vidokezi

Wakati wa kuhamia nchi mpya, wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi hukabiliwa na uelewa wa utamaduni mpya huku wakishughulikia mambo mengi, kama vile kujaza karatasi na kutafuta kazi. Mara nyingi, wafanyakazi wa huduma za kijamii wa washirika wasiotengeneza faida wa Airbnb.org huwasaidia wateja wakimbizi kutekeleza kazi hizi muhimu na kuwasaidia kupata makazi ya kudumu. Wakati mwingine, wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi wanalazimika kukabiliana na changamoto hizi wenyewe.

Kama Mwenyeji, unaweza kuwa sehemu ya wakati muhimu katika maisha ya mtu kwa kutoa sehemu salama na nzuri ya kukaa anapokaa kwa muda katika mazingira mapya hadi aweze kutengeneza mpango wa maisha yake ya baadaye na kurudia hali ya kawaida.

Katika makala hii, utapata vidokezi kuhusu jinsi ya kujiandaa kuwakaribisha wageni ambao wanajenga upya maisha yao. Mapendekezo haya yanategemea ushauri kutoka kwa Wenyeji wengine ambao wamewakaribisha wageni wakimbizi na kutoka kwa wafanyakazi wa huduma za kijamii wanaowasaidia wateja wakimbizi.

1. Wasilisha kwa njia dhahiri maelezo kuhusu eneo lako

Kabla ya kuweka nafasi, mfanyakazi wa shirika lisilotengeneza faida kutoka kwa mojawapo ya washirika wasiotengeneza faida wa Airbnb.org—kama vile IRC na HIAS—au mgeni mtarajiwa ambaye amepokea vocha ya kuweka nafasi iliyolipiwa anaweza kuwasiliana nawe ili kuthibitisha maelezo kuhusu sehemu yako. Ili kuwezesha jambo hili, tafadhali hakikisha kwamba maelezo ya tangazo lako yamekamilika na ni ya kisasa na ujibu mara moja maulizo yoyote.

Ni muhimu kufahamu kwamba wakati wa mgogoro wa wakimbizi, kama ule unaoathiri watu wa Ukrainia kwa sasa, uhitaji wa kupata makazi ni wa dharura na haraka. Katika visa fulani, maombi ya kuweka nafasi ya Airbnb.org yanaweza kuwa ya ukaaji wa siku 30 au zaidi, kuanzia siku moja au mbili tu baada ya mgeni kuwasiliana kwa mara ya kwanza.

Wakati wa mchakato wa kuweka nafasi, unaweza kumuuliza mgeni au mfanyakazi wa huduma za kijamii maswali na ikiwa kuna uhitaji, utaweza pia kufikia timu ya usaidizi ya Airbnb.org iliyopewa mafunzo mahususi.

2. Elewa kwamba wageni wakimbizi wanaweza kuhitaji usaidizi wa ziada

Washirika wasiotengeneza faida mara nyingi huwapa wateja wao mahitaji ya msingi kama vile chakula na usafiri na ufikiaji wa huduma muhimu kama vile huduma za afya, kuwatafutia kazi na usaidizi wa makazi ya muda mrefu.

Kutokana na kiwango kikubwa cha jitihada za makazi mapya ya wakimbizi wa Ukrainia, uhitaji wa huduma hizi za usaidizi ni mkubwa mno. Wageni wanahimizwa kwanza kujitahidi kushughulikia mambo haya ya msingi wao wenyewe, ili usaidizi uweze kutolewa kwa watu wenye uhitaji mkubwa zaidi.

Kama Mwenyeji, unaweza kuchagua kutoa mwongozo kuhusu nyenzo za eneo lako ili kuwasaidia wageni wako wazoee jumuiya yao mpya, ingawa hilo halihitajiki.

"Niliangalia mambo kwa uhalisia kama mama," anasema Mwenyeji Sarah wa Vancouver, Kanada. “Je, walihitaji nguo? Je, tuweke chakula kwenye friji? Je, watataka msaada wa kununua chakula?" Alituma maswali haya kwa mfanyakazi wa huduma za kijamii wa wageni wake, ambaye alijibu ujumbe huo kwa kusema kwamba familia ambayo atakaribisha inaweza kufurahia mablanketi ya ziada na midoli kwa ajili ya watoto.

Akiwa na urithi wa Ukrainia na uzoefu wake wa awali wa kukaribisha wakimbizi kupitia Airbnb.org, Mwenyeji Adam wa Ontario, Kanada, alikuwa tayari kuwapa makazi watu waliokimbia mgogoro nchini Ukrainia. Mbali na kukaribisha wageni kwenye sehemu yake mwenyewe na nyumba anazosimamia, Adam anasema kwamba anafurahi kuwasaidia wageni kujenga upya maisha yao kwa kuwaunganisha na utamaduni na jumuiya ya Ukrainia katika eneo lake, kama vile maduka, makanisa na madarasa ya maendeleo ya kitaalamu katika kituo cha jumuiya cha Ukrainia cha eneo lake. "Nitamuuliza, ‘Ulikuwa unafanya nini ukiwa nchini mwako?' na kujaribu kumwelekeza kwa njia inayofaa,” anasema.

3. Zingatia faragha

Kiwango cha faragha ambacho kila mtu au familia anapendelea kitatofautiana, kama vile ilivyo kwa mgeni mwingine yeyote wa Airbnb. Kutambua maeneo ya nyumba yako ambapo wageni wanaweza kupumzika faraghani au kuungana kama familia—pango, ua wa nyuma au sehemu nyingineyo—kunaweza kurahisisha muda wa mabadiliko na kuwasaidia wajisikie wamekaribishwa.

"Familia [tuliyokaribisha] iliweza kuwa ya kujitegemea au iliyotangamana kadiri ilivyotaka," Sarah anasema. "Tulikuwa wenye urafiki iwapo tuliwaona kwenye bustani au wakiweka mboga, lakini tuliwapa nafasi ya kufanya mambo yao wenyewe."

4. Zingatia itifaki za afya na usalama za COVID-19

Airbnb imeanzisha miongozo na mipango ya kuwasaidia Wenyeji kutoa ukaaji salama. Haya hapa ni baadhi ya mambo muhimu:

  • Vaa barakoa na uepuke mikusanyiko unapohitajiwa kufanya hivyo na sheria na miongozo ya eneo lako
  • Fuata mchakato wa kufanya usafi wa kina wa hatua 5 wa Airbnb baada ya mgeni kutoka na kabla ya mwingine kuingia
  • Usisafiri au kukaribisha wageni ikiwa hivi karibuni umekaribiana na mtu aliyeambukizwa au ikiwa una dalili za COVID-19
Pata maelezo zaidi kuhusu matakwa ya afya na usalamaya COVID-19 ya Airbnb

5. Pata nyenzo zaidi

Wageni wakimbizi wanaweza kuwa wamekumbwa na shida kubwa kama sehemu ya safari yao. Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu yale ambayo wakimbizi wanapitia, angalia nyenzo hizi zilizopendekezwa na washirika wetu wasiotengeneza faida:

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je, wale wanaokimbia Ukrainia wanaweka vipi nafasi ya sehemu zao za kukaa za muda?
Mara baada ya mtu au familia kutambuliwa kuwa anahitaji makazi ya muda, mfanyakazi wa shirika lisilotengeneza faida anaweza kumsaidia kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa au mgeni huyo anaweza kupokea vocha ya kuweka nafasi, inayomwezesha kuweka nafasi ya malazi ya muda mwenyewe.

Wenyeji wanaweza kuarifiwa wakati wa mchakato wa kuweka nafasi wakati ombi la kuweka nafasi ni la makazi ya dharura kupitia Airbnb.org.

Je, nitarajie kutoa makazi kwa wageni wakimbizi kwa muda gani?
Sehemu za kukaa za Airbnb.org kwa kawaida huwekewa nafasi ya siku kadhaa hadi wiki kadhaa. Hata hivyo, kadiri mamilioni ya watu wanavyokimbia Ukrainia, ndivyo mashirika yasiyotengeneza faida na mashirika ya serikali yanavyoshughulikia idadi kubwa ya maombi ya msaada na kusababisha ukaaji wa siku 30 au zaidi kwa baadhi ya wageni.

Baadhi ya miji imeondoa vikomo vya muda wa kukaa kwa ajili ya makazi ya wakimbizi—ili kujua kanuni zinazotumika katika eneo lako, tafadhali wasiliana na mamlaka husika za eneo lako.

Ni nini kinachotokea baada ya ukaaji wa mgeni mkimbizi kumalizika?
Wakati wa ukaaji wa muda wa mgeni mkimbizi, huenda anapanga hatua zinazofuata za kuanzisha maisha yake katika eneo jipya, ikiwemo kupata malazi ya muda mrefu.

Wageni wana ufikiaji wa moja kwa moja wa timu mahususi ya usaidizi ya Airbnb.org, ambao hufanya kazi kwa karibu na mashirika yasiyotengeneza faida ya eneo husika kwa ajili ya usaidizi wa ziada ikiwa inahitajika.

Kutokana na kiwango cha mgogoro wa Ukrainia kisicho na kifani, mashirika yasiyotengeneza faida lazima yaweke kipaumbele katika kutoa usaidizi wa ziada kwa watu binafsi wanaotathmini kama wenye uhitaji mkubwa. Kwa wakati huu, haiwezekani kuhakikisha kwamba kila mgeni ataweza kupokea usaidizi wa muda mrefu.

Iwapo mgeni atahitaji makazi ya ziada ya muda mwishoni mwa ukaaji wake, anaweza kuwasiliana na Airbnb.org ili kuomba hadi wiki mbili za malazi ya ziada.

Je, watu wanastahiki vipi kupata sehemu za kukaa za dharura?
Airbnb.org mara nyingi hufanya kazi na mashirika yasiyotengeneza faida na mashirika ya kuwezesha kupata makazi mapya yanayojishughulisha na kuitikia migogoro na makazi mapya ya wakimbizi ili kuwezesha usaidizi katika eneo husika, ikiwemo kutathmini mahitaji na ustahiki wa wageni watarajiwa.

Wageni wa Airbnb.org wanaoweka nafasi ya malazi ya muda wenyewe wanahitajika kufungua akaunti ya Airbnb, ambayo inaweza kujumuisha ukaguzi wa uthibitishaji wa utambulisho.

Je, kukaribisha wageni kupitia Airbnb.org kunaathiri vipi hadhi yangu ya Mwenyeji Bingwa?
Kwa tathmini ya Mwenyeji Bingwa ya tarehe 1 Aprili, 2022 (ikiwemo takwimu kuanzia tarehe 1 Aprili, 2021 hadi tarehe 31 Machi, 2022):

  • Nafasi zilizowekwa za Airbnb.org zitaongezwa kwenye idadi yako ya jumla ya ukaaji.
  • Nafasi zilizowekwa za Airbnb.org hazitaathiri mambo mengine yanayozingatiwa wakati wa tathmini za Mwenyeji Bingwa za kila robo mwaka, ikiwemo tathmini, ughairi na utoaji wa majibu.

Uko tayari kuanza? Jiunge na jumuiya inayoendelea kukua ambayo hufungua nguvu ya kushiriki vitu wakati wa uhitaji kupitia Airbnb.org.

Vidokezi

Airbnb
29 Ago 2019
Ilikuwa na manufaa?