Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Kuweka bei kwa ajili ya ukaaji wa muda mrefu

Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi yanaweza kusaidia kuongeza kiwango cha utafutaji na uwekaji nafasi.
Na Airbnb tarehe 11 Mei 2021
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 17 Mei 2023

Karibu usiku mmoja kati ya usiku tano uliowekewa nafasi kwenye Airbnb ni sehemu ya ukaaji ambayo ni usiku 28 au zaidi.* Kukaribisha wageni kwenye sehemu za kukaa za kila wiki na kila mwezi mara nyingi huleta manufaa kama vile:

  • Viwango vya juu vya ukaaji na idadi ya chini ya wageni wanaoondoka

  • Kuwatumia wageni ujumbe mara chache na haja ya kuwasimamia

  • Mapato thabiti kuliko ukaaji wa muda mfupi

Wageni wanaopenda kukaa muda mrefu huwa wanatafuta maeneo yenye mapunguzo. Wenyeji wanaweza kuweka punguzo la kila wiki kwa ajili ya nafasi zilizowekwa za usiku saba au zaidi au punguzo la kila mwezi kwa ajili ya nafasi zilizowekwa za usiku 28 au zaidi.

Kuweka mapunguzo haya kunaweza kusaidia kuboresha nafasi ya tangazo lako kwenye matokeo ya utafutaji, ambapo punguzo lako la kila wiki au kila mwezi linaonyeshwa pembeni mwa bei yako ya awali.

Kuzingatia mahitaji ya eneo husika na gharama zako

Kabla ya kuweka punguzo, unaweza kuangalia mahitaji ya eneo husika. Ikiwa unakaribisha wageni katika eneo ambalo linavutia umati wa watu, fikiria ikiwa kubadilisha bei yako kwa miezi fulani kunaweza kusaidia vizuri mkakati wako wa kupanga bei.

Unaweza pia kuzingatia gharama za kawaida kama vile:

  • Kodi au marejesho ya mkopo wa nyumba. Kiasi hiki kinaweza kuwa msingi wa kuweka punguzo lako la kila wiki au kila mwezi.

  • Gharama za matumizi ya nyumbani. Kiasi unacholipa kwa ajili ya huduma za umma (maji, gesi, umeme), huduma zilizoratibiwa za mara kwa mara kama vile kufanya usafi na utunzaji wa bustani na vitu unavyochagua kuwapa wageni (sabuni ya ziada, vifaa vya kupikia, n.k.) kinaweza kujumuishwa kwenye bei yako.

  • Gharama za matengenezo. Pesa unazowekeza katika sehemu yako ili kuifanya iwe ya kustarehesha zaidi kwa ajili ya wageni, kuanzia matengenezo hadi ukarabati, zinaweza kujumuishwa kwenye bei yako.

"Ni wazo zuri kuongeza kipato unachopata kwa mwezi kupitia wageni wanaolipa bei yako ya kila usiku," anasema Oliver, Mwenyeji Jijini New York. "Kisha unaweza kurekebisha punguzo lako la kila mwezi ili lilingane na jumla hiyo, jambo ambalo husaidia kufanya mapato yako yawe ya kuaminika zaidi."

Kuweka punguzo la kila wiki au kila mwezi

Unaweza kuongeza mapunguzo kwa kutumia nyenzo za kupanga bei katika kalenda yako. Chagua aikoni ya mipangilio iliyo upande wa juu kulia. Katika kichupo cha Bei, nenda kwenye Mapunguzo kisha uchague Kila Wiki au Kila Mwezi.

Utapata punguzo lililopendekezwa kulingana na tangazo lako na uhitaji wa matangazo kama hayo katika eneo lako. Sogeza kitelezeshi kati ya asilimia 0 na 99 ili urekebishe punguzo na ufuatilie jinsi linavyobadilisha bei yako ya wastani ya kila wiki au kila mwezi. Unaweza pia kuingiza nambari wewe mwenyewe mbele ya alama ya asilimia. Unapomaliza, bofya Hifadhi ili kuweka punguzo unalotaka.

Ili kuangalia jinsi punguzo linavyoathiri mapato yako, chagua maneno "bei ya mgeni" chini ya bei yako ya kila wiki au kila mwezi. Utapata mchanganuo wa bei, ambao unaorodhesha bei ya kila usiku, ada, mapunguzo yoyote au ofa, kodi, na mapato yako.

Unaweza pia kutoa mapunguzo kwa wageni wanaoweka nafasi mapema sana, au karibu sana na tarehe zao za kuwasili. Nenda kwenye sehemu iliyoandikwa "Mapunguzo zaidi" katika kichupo cha Bei. Weka idadi ya miezi kwa watakaowahi au siku kwa wasafiri wa dakika za mwisho na asilimia ambayo ungependa kupunguza kwenye uwekaji nafasi huo.

*Kulingana na takwimu za ndani za kimataifa za Airbnb, ukaaji wa usiku 28 au zaidi ulichangia asilimia 21 ya usiku uliowekewa nafasi mwaka 2022 na asilimia 18 ya usiku uliowekewa nafasi katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2023.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
11 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?