Kufungua nyumba wakati wa shida kupitia Airbnb.org

Saidia jumuiya na upate beji kwa kukaribisha wageni au kutoa mchango.
Na Airbnb tarehe 7 Des 2020
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 24 Ago 2023

Vidokezi

  • Airbnb.org ni shirika huru lisilotengeneza faida ambalo limehamasishwa na ukarimu wa Wenyeji

  • Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa za bila malipo au zenye punguzo au michango ya mara kwa mara wanastahiki beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org

Uwezo wako kama Mwenyeji wa kufanya watu wajisikie wamekaribishwa kwenye sehemu yako hutuhamasisha kila siku. Tunajivunia jinsi jumuiya yetu ya Wenyeji imeunga mkono Airbnb.org, shirika lisilotengeneza faida lililoanzishwa mwaka 2020 ili kuendeleza kazi iliyoanzishwa na mipango ya Open Homes na sehemu za kukaa za Mstari wa Mbele.

Tangu mwaka 2012, mmefungua nyumba zenu kwa zaidi ya watu 100,000, wakiwemo wakimbizi, watafuta hifadhi, wahudumu wa dharura walio kwenye mstari wa mbele kupambana na janga la COVID-19 na watu waliohamishwa wanaokimbia maafa ya asili ulimwenguni kote.

Kazi ya Airbnb.org inawezekana kutokana na ukarimu wa Wenyeji ambao hutoa sehemu za kukaa na wafadhili ambao hutoa fedha za kuwasaidia watu wakati wa shida.

Kupata beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org

Tunasherehekea ukarimu wa Jumuiya ya Wenyeji kwa kutoa beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org. Wenyeji wanaweza kuunga mkono Airbnb.org na kupata beji kwa:

  • Kujisajili ili kukaribisha wageni kwenye sehemu za kukaa za dharura bila malipo au kwa punguzo

  • Kuwa mfadhili wa mara kwa mara

Kukaribisha wageni kwenye sehemu za kukaa za dharura

Beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org inatambua Wenyeji ambao wana angalau tangazo moja amilifu kupitia Airbnb.org ambalo linatoa sehemu za kukaa za dharura za bila malipo au zenye punguzo. Kutoa sehemu ya kukaa ya Airbnb.org kunamaanisha kuwapa makazi watu waliohamishwa, wakimbizi au wengine wanaohitaji malazi ya muda wakati wa shida.

Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha wageni kwa kusudi zuri

Kutoa mchango mara kwa mara

Unaweza pia kupata beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org kwa kujisajili ili kutoa asilimia ya malipo unayopokea kwa Airbnb.org kila mara. Au, ukipenda, unaweza kutoa mchango wa mara moja bila kufuzu kupata beji.

Pata maelezo zaidi kuhusu kutoa mchango kutoka kwenye malipo unayopokea.

Kupata majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, Airbnb.org ina uhusiano gani na Open Homes na sehemu za kukaa za Mstari wa Mbele?
Mwaka 2020, mipango ya Open Homes na sehemu za kukaa za Mstari wa Mbele za Airbnb ilibadilika kuwa Airbnb.org, shirika lisilotengeneza faida la 501(c)(3). Ingawa Airbnb ina wanajumuiya sawa na Airbnb.org, shirika hilo lisilotengeneza faida ni shirika huru lenye bodi huru ya wakurugenzi.

Je, Beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org inaonekana wapi?
Beji hiyo inaonekana kwenye wasifu wako wa Mwenyeji na kurasa za matangazo yako. Iwapo ungependa kuficha beji yako, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Je, beji inaathiri tangazo langu katika utafutaji?
Beji inasherehekea uungaji mkono wako wa ukarimu wa Airbnb.org. Haiathiri jinsi matangazo yanavyoonekana katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb na wageni hawawezi kuchuja utafutaji wao wa beji za Airbnb.org kwa wakati huu.

Je, beji hiyo inaathiri beji au hadhi yangu ya Mwenyeji Bingwa?
Beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org haiathiri beji au hadhi yako ya Mwenyeji Bingwa. Beji hiyo itaonekana kando ya beji yako ya Mwenyeji Bingwa.

Je, nitapoteza beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org iwapo nitaacha kukaribisha wageni au kutoa mchango kwenye Airbnb.org ?
Ndiyo, lakini beji itaonekana tena iwapo utaanza tena kukaribisha wageni kupitia Airbnb.org au kutoa mchango kwa Airbnb.org. Unaweza kuondoa tangazo la nyumba yako kutoka kwenye Airbnb.org au kuondoa kwa muda au kusitisha mchango wako wa mara kwa mara wakati wowote.

Je, Airbnb inasaidia vipi?
Airbnb imejizatiti kufadhili gharama za uendeshaji za Airbnb.org, kwa hivyo michango yote inaweza kwenda moja kwa moja kwa washirika wasiotengeneza faida na watu wanaohudumiwa na Airbnb.org.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Airbnb.org ni shirika huru lisilotengeneza faida ambalo limehamasishwa na ukarimu wa Wenyeji

  • Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa za bila malipo au zenye punguzo au michango ya mara kwa mara wanastahiki beji ya Muunga Mkono wa Airbnb.org

Airbnb
7 Des 2020
Ilikuwa na manufaa?