Jinsi ya kuweka bei yako
Airbnb inakupa ufikiaji wa nyenzo za kukaribisha wageni na mamilioni ya wageni ili kusaidia malengo yako ya mapato. Kuweka bei yenye ushindani kunaweza kusaidia tukio lako lionekane na kuwahimiza wageni waweke nafasi.
Daima unadhibiti bei yako na unaweza kuibadilisha wakati wowote.
Upangaji bei kwenye Airbnb
Kuanza na bei ya chini kwa ajili ya tukio jipya kunaweza kukusaidia kuwavutia wageni wako wa kwanza na ukadiriaji na tathmini za mapema. Unaweza kurekebisha bei yako baada ya muda ili kufikia malengo yako ya mapato.
Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia unapoweka bei yako kwenye Airbnb.
- Gharama zako: Fahamu kiasi unachohitaji ili kulipia gharama kama vile muda wako, vifaa na leseni.
- Matukio yanayofanana: Tafuta shughuli kama zako kwenye Airbnb na tovuti nyinginezo ili kulinganisha bei za eneo husika na uone bei ipi ni ya ushindani.
- Ada ya huduma: Hesabu ada ya huduma ambayo Airbnb inatoza wenyeji kwa kila nafasi inayowekwa, ambayo utaona unapoweka bei yako. Ada hiyo inaturuhusu kutoa nyenzo za kukaribisha wageni, kutoa huduma kwa wateja saa 24 na kuwafikia mamilioni ya wageni kupitia Matukio ya Airbnb.
Kuweka bei yako
Weka idadi yako ya juu ya wageni kulingana na shughuli, eneo na ukubwa unaofaa wa kikundi kwa ajili ya kukuza uhusiano. Kiwango hiki cha juu kitatumika kila wakati unapotoa tukio.
Weka kima cha chini cha bei yako kwa kila mgeni na kikundi binafsi.
- Bei kwa kila mgeni: Hiki ndicho kiasi ambacho utamtoza kila mgeni ili ajiunge kwenye tukio hilo. Bei yako lazima ijumuishe ada zote na bakshishi. Kutoa bei ya chini kunaweza kuvutia wageni wengi zaidi na kusababisha mapato ya juu. Kwa mfano, nchini Marekani, wageni 4 wakiweka nafasi kwa USD 60 kila mmoja jumla yake ni USD 240, huku wageni 8 wakiweka nafasi kwa USD 45 kila mmoja jumla yake ni USD 360.
- Kima cha chini cha kikundi binafsi: Hiki ndicho kiasi cha chini cha jumla ambacho utatoza kwa kikundi binafsi. Hakuna mtu mwingine anayeweza kuweka nafasi ya tarehe na muda huo mahususi.
Utaona kiasi utakachojipatia unapoweka bei yako wakati wa kuweka mipangilio.
Kuweka mapunguzo
Njia bora ya kudumisha ushindani wa bei yako ni kutoa mapunguzo kwa ajili ya aina tofauti za uwekaji nafasi.
- Kwa muda mfupi: Toa punguzo la asilimia 5 hadi asilimia 50 kwa bei yako kwa siku 30 ili kuwashawishi wageni wako wa kwanza kuweka nafasi.
- Watakaowahi: Toa punguzo la asilimia 20 kwa wageni wanaoweka nafasi zaidi ya wiki 2 mapema ili kuwavutia wageni wanaopanga mapema.
- Kikundi kikubwa: Weka punguzo kwa kikundi ili ufikie uwezo wako wa juu kwa haraka.
Mapunguzo yako yanatumika kila wakati mgeni anapoweka nafasi ya tukio. Unapoweka zaidi ya moja, mgeni hupata punguzo lolote ambalo husababisha uokoaji mkubwa zaidi wa pesa. Hawezi kupokea mapunguzo mengi kwenye nafasi ileile iliyowekwa.
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.