Jinsi ya kuweka bei zako kwenye Airbnb
Airbnb inakupa ufikiaji wa nyenzo za kukaribisha wageni na mamilioni ya wageni ili kusaidia kukuza biashara yako. Daima unadhibiti bei yako na unaweza kuibadilisha wakati wowote.
Upangaji bei kwenye Airbnb
Kama mtaalamu aliyeimarika katika uwanja wako, unaelewa umuhimu wa kutoa huduma zenye ubora wa juu kwa bei yenye ushindani. Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia unapoweka bei zako kwenye Airbnb.
- Huduma zinazofanana: Vinjari Airbnb na tovuti nyinginezo kwa ajili ya huduma kama zako ili kuona kile ambacho wenyeji wengine wanatoza.
- Bei ya utangulizi: Fikiria kuanza na bei ya chini ili kuwavutia wageni wako wa kwanza kwenye Airbnb. Unaweza kufanya mabadiliko unapojenga chapa na sifa yako kupitia ukadiriaji na tathmini nzuri za wageni.
- Ada ya Airbnb: Hesabu ada ya huduma ambayo Airbnb inatoza wenyeji kwa kila nafasi inayowekwa, ambayo utaona unapoweka bei yako. Ada hiyo inaturuhusu kutoa nyenzo za kukaribisha wageni, kutoa huduma kwa wateja saa 24 na kuwafikia mamilioni ya wageni kupitia Huduma kwenye Airbnb.
Kuweka bei tofauti
Kuainisha huduma zinazotolewa katika bei ya kuingia, ya kawaida na ya juu kunawapa wageni machaguo zaidi na kunaweza kukusaidia kufikia malengo yako ya mapato.
Bei yako inapaswa kuonyesha muundo, uchangamano na upekee wa kila huduma inayotolewa. Kwa mfano, mpiga picha nchini Marekani anaweza kutoa kipindi cha nusu saa ambacho kinagharimu chini ya USD 50, kipindi mahususi cha picha ambacho kinagharimu kati ya USD 50 na USD 150 na kipindi cha familia ambacho kinagharimu zaidi ya USD 150.
Wageni wanaotafuta huduma kwenye Airbnb wataona bei yako ya chini zaidi kwenye matokeo ya utafutaji. Huduma inayotolewa ya kiingilio inaweza kusaidia kuwavutia wageni wa mara ya kwanza na kufanya wapendezwe na huduma nyingine unazotoa.
Utakuwa na chaguo la kutoza bei kwa kila mgeni au bei isiyobadilika. Hii itatumika kwa huduma zote unazotoa.
- Bei kwa kila mgeni: Bei yako kwa kila mtu inajumuisha ada zote na bakshishi. Unaweza pia kuweka bei ya chini kwa kila nafasi iliyowekwa. Kumbuka kwamba bei ya chini inaweza kuvutia wageni wengi zaidi na kusababisha mapato ya juu. Kwa mfano, nchini Marekani, wageni 4 wakiweka nafasi kwa USD 60 kila mmoja jumla yake ni USD 240, huku wageni 8 wakiweka nafasi kwa USD 45 kila mmoja jumla yake ni USD 360.
- Bei isiyobadilika: Jumla ya bei yako inajumuisha ada zote na bakshishi kwa idadi yoyote ya wageni, hadi kima cha juu ulichoweka kwa ajili ya huduma inayotolewa.
Kuweka mapunguzo
Njia bora ya kudumisha ushindani wa bei yako ni kutoa mapunguzo kwa ajili ya aina tofauti za uwekaji nafasi.
- Kwa muda mfupi: Toa punguzo la asilimia 5 hadi asilimia 50 kwa bei yako kwa siku 30 ili kuwashawishi wageni wako wa kwanza kuweka nafasi.
- Watakaowahi: Toa punguzo la asilimia 20 kwa wageni wanaoweka nafasi zaidi ya wiki 2 mapema ili kuwavutia wageni wanaopanga mapema.
- Kikundi kikubwa: Weka punguzo la kikundi ili ufikie uwezo wako wa juu kwa haraka.
Mapunguzo yako yanatumika kila wakati mgeni anapoweka nafasi ya huduma. Unapoweka zaidi ya moja, mgeni hupata punguzo lolote ambalo husababisha uokoaji mkubwa zaidi wa pesa. Hawezi kupokea mapunguzo mengi kwenye nafasi ileile iliyowekwa.
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Huduma kwenye Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.