Jinsi ya kuchagua na kuweka picha zenye ubora wa juu
Wageni mara nyingi hutegemea picha ili kuamua nini cha kuwekea nafasi kwenye Airbnb. Picha za tukio lako zinapaswa kuvutia, kuweka matarajio wazi na kuunda msisimko.
Kuzingatia ubora
Kila picha unayoshiriki inapaswa kuwa yenye ubora wa juu. Kila picha inapaswa kuwa na udhahiri wa pikseli 800 x 1,200 na ukubwa wa faili wa hadi megabaiti 10. Unaweza kupata matokeo haya ukitumia kamera nyingi za simu mahiri.
Wasilisha picha ambazo:
- Umezipiga au umetumia kwa ruhusa
- Zina rangi, si nyeusi na nyeupe
- Zina mwanga wa kutosha, ikiwezekana kwa mwanga wa asili
- Ni rahisi katika utungaji na mandharinyuma
- Zimelengwa, huku kitu kinacholengwa kikiwa katikati
- Ni mchanganyiko wa maelezo ya karibu na utungaji mpana
Usiwasilishe picha ambazo:
- Ni nyeusi au zinazotumia mmweko mkali
- Zina ukungu, chembechembe au udhahiri mdogo
- Zimehaririwa, kuchujwa au kupotoshwa sana
- Ni picha za kujipiga au ulizojiweka tayari kwa ajili ya kupigwa
- Kolaji
- Matoleo mengi ya picha sawa
- Za nembo au chapa
Ikiwa unahitaji picha zaidi, fikiria kuwaomba marafiki au wanafamilia wapige picha kwa kuzingatia vidokezi hivi. Au waombe wageni watume picha zao bora na kukupa ruhusa ya kuzitumia kwenye tangazo lako.
Kuweka picha nzuri
Wasilisha picha 5 au zaidi, nyingi kadiri unavyohitaji ili kuamsha hamu na kuweka matarajio wazi.
Picha zinaonyeshwa katika maeneo 3 kwenye matangazo ya tukio: gridi, utaratibu wa safari yako na matunzio ya picha. Pia utachagua picha ya jalada inayovutia, ambayo wageni wanaiona katika matokeo ya utafutaji kwenye Airbnb.
Tutatathmini picha unazowasilisha na kuidhinisha picha zinazofikia viwango vyetu. Haya ndiyo mambo unayopaswa kuwasilisha kwa kila sehemu.
Gridi. Picha nne zilizo kwenye sehemu ya juu ya tangazo lako zinaunda kile kinachoitwa gridi. Jumuisha picha za:
- Wageni wakishiriki katika shughuli kuu
- Ukiongoza tukio
- Maelezo muhimu, kama vile picha ya karibu ya mavazi au kiambato
- Eneo hilo, kama vile picha ya pembe pana inayoweka mpangilio
Utaratibu wa safari yako. Utaratibu wa safari yako ni ajenda fupi ambayo huwasaidia wageni kuamua iwapo tukio linafaa. Picha za utaratibu wa safari ni ndogo, kwa hivyo chagua mandhari rahisi zilizo na mandharinyuma isiyo na mapambo. Jumuisha picha za:
- Matukio yanayolingana na maelezo yako yaliyoandikwa
- Watu, vitu na maelezo mengine ambayo ni rahisi kuelewa
Matunzio ya picha. Wageni wanaweza kuona picha zote unazoshiriki katika matunzio ya picha. Matunzio yako yanapaswa kuonyesha kinachofanya tukio kuwa la kuvutia na la kukumbukwa. Jumuisha picha za:
- Wageni wanaoingiliana nawe, wenyeji wenza wowote na wageni wengine
- Shughuli zilizopigwa picha kutoka pembe tofauti, ikiwemo mitazamo ya wageni
- Vitu vyovyote ambavyo wageni wanaweza kutarajia kwenda nazo nyumbani kama kumbukumbu
Hakikisha una ruhusa ya kutumia picha zozote unazowasilisha na kwamba picha hizo zinaonyesha tukio hilo kwa usahihi.
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.