Jinsi ya kutekeleza mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa Airbnb

Pata mwongozo kuhusu kutekeleza mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi.
Na Airbnb tarehe 4 Jun 2020
Inachukua dakika 7 kusoma
Imesasishwa tarehe 25 Jun 2021

Vidokezi

  • Mchakato wa kufanya usafi una hatua tano: tayarisha, safisha, takasa, hakiki na andaa upya.

  • Tunajua inaweza kuwa vigumu kufuata ratiba mpya ya kufanya usafi, kwa hivyo unaweza kupata vidokezi vya ziada, orodha kaguzi maalumu na zaidi katika sehemu ya kufanya usafi ya Kichupo chako cha Utendaji

    • Unaweza pia kurejelea kitabu cha mwongozo wa kufanya usafi wa kina kilichotengenezwa na wataalamu cha Airbnb ili kusaidia kutekeleza mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina

    • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuunda sehemu inayofaa wageni

    Kwa sababu usafi ni muhimu zaidi, Wenyeji wa malazi wanahitaji kufuata mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina wa Airbnb—na tuko hapa kukusaidia kutekeleza mchakato huo. Makala hii itakuelekeza katika hatua hizi 5, pamoja na mwongozo wa ziada, vidokezi na mazoea bora ili kukusaidia kufuata kiwango thabiti cha kufanya usafi. Mazoea haya bora yanategemea kitabu cha mwongozo wa kufanya usafi wa kina, ambacho kilitengenezwa na wataalamu wa afya na ukarimu kwa kuzingatia ustawi wako.

    Kabla ya kufanya usafi, ni muhimu kwamba wewe au wasafishaji wako wataalamu wawasiliane na mamlaka ya eneo lako kwa ajili ya miongozo kuhusu muda unaofaa wa kusubiri kabla ya kuingia kwenye sehemu. Kwa mfano, shirika la Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Marekani linapendekeza kusubiri kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo (angalau saa kadhaa) baada ya mgeni kuondoka, kabla ya kuingia kwenye sehemu kwani hii inaweza kusaidia kupunguza kuhatarishwa kwako kwa viini. Ili kuacha muda wa kutosha wa kukamilisha mchakato wa kufanya usafi, unaweza pia kufikiria kuongezea bafa ya kuweka nafasi kati ya nafasi zilizowekwa kwa kusasisha mipangilio yako kwa ajili ya wakati wa maandalizi.

    Ili kukusaidia uanze, tunashiriki mazoea bora kabisa kuhusu hatua 5 za mchakato wa kufanya usafi: andaa, safisha, takasa, hakiki kisha andaa upya.

    Hatua ya 1: Jitayarishe kufanya usafi salama

    • Ruhusu hewa iingie kwenye vyumba kabla na wakati unapofanya usafi.Mamlaka yanayosimamia sheria kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO) na Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Ugonjwa vya Marekani (CDC), hupendekeza kufungua milango na madirisha ya nje na kutumia feni za kuingiza hewa ili kuongeza mzunguko wa hewa katika sehemu hiyo kabla ya kuanza kusafisha na kutakasa. Acha hewa iingie kwenye sehemu hiyo kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo kabla na wakati wa kufanya usafi.
    • Kusanya vifaa sahihi vya kufanya usafi. Tunapendekeza utumie dawa za kuua viini na kutakasa ambazo zimesajiliwa na shirika husika la serikali (k.m. Shirika la Kemikali la Ulaya au Shirika la Kulinda Mazingira la Marekani).
    • Tathmini miongozo ya usalama kwa ajili ya kemikali zako. Soma lebo kwenye bidhaa zako kila wakati ili kuelewa viambato vyake amilifu na jinsi ya kuvitumia ifaavyo.
    • Nawa mikono kwa angalau sekunde 20 kwa sabuni na maji. Ikiwa kufanya hivyo hakuwezekani, tumia kitakasa mikono kilicho na alkoholi ya angalau asilimia 60 na urejelee wakala wa serikali yako ili kupata miongozo ya hivi karibuni zaidi.
    • Vaa mavazi ya kujikinga Kabla ya kuingia kwenye sehemu, zingatia kuvaa mavazi ya kujikinga kama vile glavu za kutumiwa mara moja na kutupwa na barakoa au vifunika uso vya kitambaa.
    • Toa taka zote. Kuanzia na hatua hii husaidia kuzuia taka chafu kuchafua sehemu hiyo baada ya kusafishwa. Hakikisha unaweka mfuko wa karatasi kwenye ndoo zote za taka, ambao utafanya iwe rahisi kutupa tishu na taka nyinginezo.
    • Kusanya mashuka yote machafu katika sehemu yote. Tumesikia kutoka kwa Wenyeji kwamba kufua nguo ni mojawapo ya shughuli zinazotumia wakati mwingi baada ya wageni kuondoka na kabla ya kuja kwa wengine. Kusanya mashuka machafu mara tu unapoingia kwenye sehemu na uepuke kuyakung'uta, kwani kufanya hivyo kunaweza kuongeza kuenea kwa viini.
    • Chomoa plagi ya umeme kabla ya kufanya usafi. Kwa usalama wako na kwa ajili ya kulinda vifaa vilivyorekebishwa, kumbuka kuchomoa plagi ya umeme ya vifaa kabla ya kufanya usafi. Vifaa vilivyotiwa plagi kwenye soketi ambavyo “vimezimwa” bado vimeunganishwa na umeme hadi plagi hiyo itakapotolewa. Unaweza pia kuzima umeme kwenye mfumo wa kukata.

    Kumbusho la usalama: Fikiria kuvaa mavazi masafi ya kujikinga kabla ya kuingia kwenye sehemu. Kurejelea lebo zote za usalama kunaweza pia kukusaidia kuelewa jinsi ya kutumia kemikali za kufanyia usafi ifaavyo.

    Hatua ya 2: Safisha kwa kuondoa vumbi na uchafu

    Kusafisha ni wakati unaondoa vijidudu na uchafu kutoka kwenye sehemu mbalimbali—kwa mfano, kutumia kitambaa chenye sabuni kufuta kaunta ya jikoni au sehemu ya juu ya jiko. Ni muhimu ukamilishe hatua hii kabla ya kutakasa sehemu yako.

    • Fua mashuka kwenye mpangilio wa juu zaidi wa joto uliopendekezwa na mtengenezaji. Kumbuka kunawa mikono yako kabla ya kushughulikia mashuka yoyote safi.
    • Osha vyombo vyote na uondoe kila kitu kwenye mashine ya kuosha vyombo Ni muhimu kuosha vyombo vinavyotumiwa na wageni ili kusaidia kuhakikisha viwango vya usafi. Ikiwa huna mashine ya kuosha vyombo, osha vyombo kwa kutumia maji moto na sabuni ya kuoshea vyombo inayoondoa bakteria. Ili kusaidia kuepuka maambukizi ya kuenea, anza kwa kupita katika kila sehemu ya nyumba na ukusanye vyombo katika kila chumba.
    • Pangusa sehemu na ufagie au ufyonze vumbi kwenye sakafu. Wakati wa kupangusa anza kutoka juu hadi chini ili kuhakikisha kuwa hakuna ishara za uchafu zinazoonekana. Fagia sakafu zote ambazo ni ngumu na ufyonze vumbi kwenye mazulia.
    • Safishasehemu ngumu kwa sabuni na maji. Futa kila sehemu ili kuondoa uchafu, grisi, vumbi na viini. Sehemu ngumu ni pamoja na vitu kama vile kaunta, meza, sinki, makabati na sakafu. Unapopiga deki, anzia kwenye kona ya nyuma ya chumba hicho kuelekea mbele kisha mwaga maji kwenye sinki ambalo bado halijasafishwa.

    • Safishasehemu laini kulingana na maelekezo ya mtengenezaji. Sehemu laini hujumuisha vitu kama vile zulia, matandiko na makochi. Ikiwa zimechafuka, ondoa kwa uangalifu uchafu au masizi yoyote yanayoonekana, kisha safisha kwa kutumia bidhaa za kufanya usafi zinazofaa. Ikiwa inawezekana, safisha vifaa kwa mashine kulingana na maelekezo ya mtengenezaji.

    Kumbusho la usalama: Ili kusaidia kuzuia kuenea kwa viini, usiguse uso wako wakati unafanya usafi.

    Hatua ya 3: Takasa kwa kutumia dawa ya kuua viini

    Kutakasa ni pale unapotumia kemikali ili kupunguza idadi ya viini na bakteria. Wakati wa hatua hii, tunawahitaji Wenyeji watakase sehemu zote zinazoguswa mara nyingi. Kwa mfano, Wenyeji wanaweza kutakasa vitasa vya milango, swichi za taa na makabati kwa kunyunyizia kemikali ya kuua viini kwenye sehemu hizi.

    • Mara baada ya sehemu ngumu kuwa imesafishwa, inyunyizie kwa kutumia dawa ya kuua viini.Weka mkazo kwenye kutakasa sehemu zote zinazoguswa mara nyingi katika sehemu hiyo (kama vile vitasa vya mlango na swichi za taa). Hakikisha unatakasa vifaa vya kielektroniki kulingana na maelekezo ya kufanya usafi ya mtengenezaji.
    • Acha dawa ya kuua viini isalie katika hali ya unyevunyevu kwa muda uliowekwa. Lebo ya bidhaa itaelezea muda unaohitajika wa kusalia katika hali ya unyevunyevu kwa kemikali hizo ili kutakasa sehemu ifaavyo. Hii inazipa kemikali wakati wa kutosha wa kuua viini vingi kadiri iwezekanavyo.
    • Acha sehemu zikauke kwa hewa. Ikiwa sehemu zinakauka kabla ya muda wa unyevu kukaa mahali, hakuna uhakikisho kwamba bidhaa hiyo imeua viini vilivyoandikwa kwenye lebo.

    Ukumbusho wa usalama: Kurejelea lebo zote za usalama husaidia kuhakikisha unatumia kwa usahihi kemikali za kufanya usafi.


    Hatua ya 4: Hakiki orodha kaguzi zako za chumba kwa chumba

    Utaweza kufikia orodha kaguzi mahususi za kufanya usafi kulingana na maelezo ya tangazo lako. Hakikisha unarejelea mazoea bora katika kila orodha kaguzi ya chumba kwa chumba na ushiriki na timu yako ya kukaribisha wageni au wataalamu wa kufanya usafi.

    • Chunguza kwa umakini ili kuhakikisha kuwa sehemu zote zinazoguswa sana zilitakaswa. Shughulikia kitu chochote ambacho kinaweza kuwa kilisahaulika.
    • Andika matatizo yoyote ya matengenezo au vitu vinavyokosekana. Unapokuwa ukikagua ukamilishaji, andika vitu vyovyote vinavyohitaji kubadilishwa, kujazwa tena au kuongezewa.

    Hatua ya 5: Andaa upya chumba

    Ili kusaidia kuzuia maambukizi ya kuenea, ni muhimu kukamilisha usafishaji na utakasaji wa chumba kabla ya kukiandaa upya kwa ajili ya mgeni anayefuata.

    • Tupa na usafishe vifaa vyako vya kufanyia usafi. Tupa mbali bidhaa zozote za kutumika mara moja na kutupwa kama vile vifutio vya dawa ya kuua viini. Hakikisha pia unasafisha zana zingine ambazo zilitumika. Fua vitambaa vyovyote vya kufanyia usafi kwa mpangilio unaofaa wa joto la juu zaidi kadiri iwezekanavyo.
    • Ondoa kwa usalama vazi lolote la kujikinga mara baada ya kukamilisha kufanya usafi. Tupa au usafishe vazi lolote la kujikinga kulingana na miongozo yake ya matumizi.
    • Nawa mikono kwa angalau sekunde 20 kwa sabuni na maji. Ikiwa kufanya hivyo hakuwezekani, tumia kitakasa mikono kilicho na alkoholi ya angalau asilimia 60 na urejelee wakala wako wa serikali ili kupata miongozo ya hivi karibuni zaidi.
    • Tathmini kwa kutazama kila chumba ili kuhakikisha hatua husika imepangwa kwa ajili ya mgeni anayefuata. Jione wewe kama mgeni anayeingia kwenye sehemu hiyo kwa mara ya kwanza.
    • Andaa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya wageni wako. Tumesikia kutoka kwa wageni kwamba wanataka wawe na uwezo wa kufanya usafi wao wenyewe wanapokuwa katika sehemu yako. Wawezeshe wageni wako kwa kuandaa vifaa vya kufanyia usafi ambavyo wanaweza kuvitumia, kama vile kitakasa mikono, taulo za karatasi za kutumika mara moja na kutupwa, dawa ya kuua viini ya kunyunyiza au vifutio na sabuni ya ziada ya mkono.
    • Jaza hifadhi ya vifaa vyako vya kufanyia usafi Hakikisha unaangalia tarehe za kuisha muda wa matumizi na ujaze tena vifaa vyovyote ambavyo umetumia ili uwe tayari kwa ajili ya wageni wanaofuata.

    Ukumbusho wa usalama: Daima weka bidhaa za kemikali mbali na watoto.

    Jizatiti kwa ajili ya viwango vya juu vya kufanya usafi

    Kwa kuwa sasa unaujua mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi, ni wakati wa kubadilisha utaratibu wako wa sasa na kutumia mbinu hizi kwa kila chumba kwenye sehemu yako. Tunajua linaweza kuwa jambo gumu kutumia utaratibu mpya wa kufanya usafi, kwa hivyo tumetengeneza kitabu cha mwongozo wa kina wa kufanya usafi ambao unajumuisha mwongozo unaoungwa mkono na wataalamu, vidokezi vya usalama na orodha kaguzi ili kukusaidia uweke mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina katika vitendo. Tunawataka Wenyeji wa sehemu za kukaa wafuate mchakato wa hatua 5 wa Airbnb wa kufanya usafi wa kina kila baada ya ukaaji kukamilika.

    Mara baada ya Wenyeji kujizatiti kufuata mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi, kujizatiti kwao kufanya usafi wa kina kutaonyeshwa kwenye ukurasa wa tangazo lao ili kuwajulisha wageni kuwa wamekubali kufuata kiwango thabiti cha kufanya usafi.

    Tafadhali zingatia kwamba matakwa ya kufanya usafi yanaweza kufanyiwa mabadiliko kadiri muda unavyokwenda kulingana na mwongozo wa wataalamu unavyobadilika. Kulingana na sayansi inayobadilika, mchakato wa hatua 5 wa Airnb wa kufanya usafi wa kina na kitabu cha mwongozo wa kina wa kufanya usafi hulenga kuweka kipaumbele kwenye afya na ustawi wa Wenyeji na wageni.

    Tunajua kuwa kuanzisha mchakato mpya katika utaratibu wako huchukua muda, kwa hivyo tunatengeneza elimu na sifa za bidhaa ili kukusaidia ukamilishe viwango hivi vya kufanya usafi. Angalia sehemu ya kufanya usafi ya kichupo chako cha Vidokezi ili kupata elimu, vidokezi na orodha kaguzi mahususi. Kwa mwongozo wa kina, unaweza pia kupakua kitabu cha mwongozo wa kufanya usafi.
    Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina hutoa matakwa rahisi kwa ajili ya kusafisha nyumba yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutekeleza hatua hizo, tafadhali rejelea Kitabu chote cha mwongozo wa kufanya usafi cha Airbnb. Kama Mwenyeji, unaweza kuchukua hatua za ziada ili ujilinde, ulinde timu yako na wageni wako; na daima unapaswa kuomba ushauri na kufuata sheria au miongozo yoyote ya eneo husika. Airbnb haiwajibiki kwa majeraha au ugonjwa wowote unaotokana na kufuata mchakato huu wa kufanya usafi. Kwa miongozo ya kufanya usafi na sheria mahususi zinazohusu eneo lako unakokaribisha wageni, tafadhali alamisha Makala haya ya Kituo cha Msaada.

    Vidokezi

    • Mchakato wa kufanya usafi una hatua tano: tayarisha, safisha, takasa, hakiki na andaa upya.

    • Tunajua inaweza kuwa vigumu kufuata ratiba mpya ya kufanya usafi, kwa hivyo unaweza kupata vidokezi vya ziada, orodha kaguzi maalumu na zaidi katika sehemu ya kufanya usafi ya Kichupo chako cha Utendaji

      • Unaweza pia kurejelea kitabu cha mwongozo wa kufanya usafi wa kina kilichotengenezwa na wataalamu cha Airbnb ili kusaidia kutekeleza mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina

      • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuunda sehemu inayofaa wageni
      Airbnb
      4 Jun 2020
      Ilikuwa na manufaa?