Jinsi ya kuandaa tukio shwari
Wageni wanathamini wakati mwenyeji wao amejizatiti kutoa huduma isiyo na usumbufu. Hii inamaanisha kutoa majibu, kutoa maelekezo dhahiri ya kuwasili, kuelezea tukio lako kwa usahihi na kufika kwa wakati na kuwa mwenye mpangilio.
Kuwa mwenye kutoa majibu
Tumia nyenzo za kutuma ujumbe za Airbnb ili kujibu ujumbe wa wageni papo hapo kabla na baada ya tukio.
- Tumia majibu ya haraka. Violezo hivi vya ujumbe hutoa maelezo kwenye tangazo lako na nafasi zilizowekwa na wageni ili kukusaidia kujibu haraka. Unaweza kuyahariri na pia kuratibu yatumwe kwa nyakati fulani, kama vile mara baada ya mgeni kuweka nafasi.
- Weka arifa. Kuona ujumbe wa wageni mara moja kunaweza kuboresha muda wako wa kujibu. Kuwa mwangalifu sana kabla ya mkutano wako.
"Kutoa majibu ya haraka ni muhimu sana," anasema Jib, ambaye anaandaa mafunzo ya upishi jijini Bangkok. "Kadiri unavyoweza kutatua matatizo ya wageni kwa haraka au kujibu maswali yao, ndivyo wanavyohisi kuwa utategemewa."
Kutoa maelekezo dhahiri ya kuwasili
Hakikisha wageni wanajua mahali pa kukutana ili kusaidia kuonyesha kwamba unategemeka.
- Andika maelekezo ya kina. Toa maelezo yanayofaa ili kuwasaidia wageni kupata eneo lako la mkutano na kujua jinsi ya kukutambua.
- Toa maelekezo mapema. Ratibu jibu la haraka lenye maelekezo ya kuwasili siku moja au mbili kabla ya tukio lako ili wageni wako wawe na muda wa kuuliza maswali.
Dani, ambaye huandaa ziara ya matembezi ya Brooklyn, hutuma ujumbe wa makaribisho wageni wanapoweka nafasi akielezea njia ya treni ya chini ya ardhi na mahali watakapokutana na kuondoka. "Hiyo inawapa wageni muda mwingi wa kupanga siku yao iliyosalia," anasema.
Kuelezea tukio lako kwa usahihi
Tangazo lako linapaswa kuelezea kwa kina kile ambacho wageni wanaweza kutarajia wakati wa tukio.
- Weka wenyeji wenza wowote. Nenda kwenye kalenda yako ili uweke wenyeji wenza unaoshirikiana nao kwenye awamu ambazo watakuwa wakiandaa. Hii huwasaidia wageni wajue ni nani wa kumtafuta.
- Jumuisha taarifa za kina. Wasaidie wageni kujiandaa kwa ajili ya tukio lako kwa kushiriki kila kitu wanachohitaji kujua katika maelezo na picha za tangazo lako. Kwa mfano, unaweza kuwajulisha nini cha kupakia, kama vile viatu vya matembezi ya masafa marefu na maji au kuonyesha picha za ngazi zenye mwinuko.
"Ninawajulisha wageni kwamba tutatembea kwenda sokoni, ambapo watapata sauti changamfu na harufu nzuri," anasema Graciela, ambaye huandaa mafunzo ya upishi jijini Mexico City. "Kwa njia hii, wanawasili wakiwa tayari na wenye msisimko kwa ajili ya tukio hilo."
Kuwa mwenye mpangilio na kufika kwa wakati
Kufuata utaratibu wa safari yako husaidia tukio lako liendeshwe vizuri.
- Chukua muda wa kupanga mapema. Andaa eneo lako na vifaa vyovyote ili tukio lako liwe kwenye ratiba. Kwa mfano, hakikisha eneo hilo ni safi na kuna viti na sehemu za kufanyia kazi za kutosha.
- Weka kasi inayoweza kudhibitiwa. Anza na umalize kwa wakati na ujumuishe mapumziko ili usilazimike kuharakisha shughuli.
"Nilitumia muda mwingi kupanga njia yangu," anasema Evren, ambaye anaandaa ziara ya matembezi ya muziki ya Soho jijini London. "Na kisha nilifanya mazoezi ili kuhakikisha kwamba inafanya kazi."
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.