Jinsi ya kukuza uhusiano
Wenyeji waliopewa ukadiriaji wa juu waeleza wanavyokuza mwingiliano wa wageni.
Na Airbnb tarehe 13 Mei 2025
Imesasishwa tarehe 13 Mei 2025
Wageni wanathamini fursa za mwingiliano halisi na wewe na wageni wengine. Unda nyakati kabla, wakati na baada ya tukio ili kuwapa hisia ya uhusiano na kujisikia nyumbani.
Kuhimiza mwingiliano wenye maana
Tengeneza muda katika utaratibu wa safari yako kwa ajili ya wageni kuwa na uhusiano nawe, wao kwa wao na jumuiya yako. Hiyo inaweza kujumuisha shughuli zilizopangwa na zisizopangwa.
- Panga kianzisha-mazungumzo. Fikiria kidokezi cha haraka, kama vile kuwauliza wageni walikotoka. Graciela, ambaye anaandaa mafunzo ya upishi jijini Mexico City, wakati mmoja alikuwa na wageni wa kimataifa waliogundua kuwa wao ni majirani. "Utangulizi huo rahisi uligeuka kuwa uhusiano usiotarajiwa," anasema.
- Acha kikundi kichangamane. Unaweza kuwaalika wageni kujadili mada au kusimulia hadithi ili kuwasaidia kufahamiana. "Ninakutana na watu wa ajabu wenye masimulizi ya ajabu ya maisha," anasema Alan, ambaye anaandaa ziara ya Maporomoko ya Niagara. "Na wanapendelea kufanya matukio ya kukutana na watu. Wanahitaji sana uhusiano huo wa binafsi.”
- Tambulisha jumuiya yako. Wasaidie wageni kuungana na wakazi, iwe imepangwa au haikutarajiwa. Ruthy, ambaye anaandaa ziara ya chakula jijini Lisbon, anasema yeye ndiye gundi inayowaunganisha wageni na jumuiya. "Wageni wanapenda tunapowatambulisha kwa bibi mtaani."
Ukifanya mabadiliko ili kuwapa wageni muda wa kuungana, sasisha utaratibu wa safari yako ili wajue nini cha kutarajia.
Kuongoza mazungumzo
Endelea kushirikiana na wageni wako kwenye kichupo cha Ujumbe kabla na baada ya tukio.
- Ratibu ujumbe wa makaribisho. Anzisha uzi wa ujumbe wa kikundi kwa kuweka utangulizi. Waulize kile wanachotarajia kupata kutokana na tukio hilo na ikiwa mtu yeyote anasherehekea tukio maalumu.
- Pata maelezo kuhusu kila kikundi. Endelea kushiriki kwenye gumzo ili kusaidia kukuza uhusiano bora wa ana kwa ana. Utapata pia maelezo kuhusu wageni wako kwenye kichupo cha Leo, ikiwemo mambo wanayopenda na walikotoka.
- Fuatilia baadaye. Shiriki picha, video na mapendekezo na uwahimize wageni wafanye vivyo hivyo. Hii inaweza kusaidia kuimarisha uhusiano ambao wageni walifanya na kuweka tukio hilo akilini wakati wanaombwa watoe ukadiriaji na tathmini.
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
13 Mei 2025
Ilikuwa na manufaa?