Utaratibu wa msingi wa kukaribisha wageni kwenye Airbnb

Hii ndiyo njia ya kuanza kujipatia pesa kama Mwenyeji.
Na Airbnb tarehe 20 Nov 2019
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 8 Nov 2023

Watu huanza kukaribisha wageni kwenye Airbnb kwa sababu nyingi, kama vile kujipatia pesa na kukutana na wasafiri kutoka kote ulimwenguni. Unaweza kukaribisha wageni kwenye aina yoyote ya sehemu uliyonayo, iwe ni nyumba nzima, chumba cha ziada au nyumba ya kulala wageni. Haya ni mambo machache ya kufanya ili uanze.

Unda tangazo lako

Mojawapo ya mambo ya kwanza unayohitaji kufanya ni kuweka tangazo lako. Elezea sehemu yako kwa usahihi, shiriki mambo ya kipekee na uweke matarajio ya wazi kwa wageni. Hii ni fursa yako ya kuwavutia wageni waweke nafasi kwenye eneo lako.

  • Picha: Pakia picha nyingi za kila chumba kutoka pembe tofauti ili kuonyesha kile ambacho wageni wanaweza kufikia. Zana inayoendeshwa na Akili Bandia (AI) inaweza kukusaidia kupanga picha kulingana na chumba ili kuunda ziara ya mtandaoni. Weka maelezo kwa kila chumba, kama vile mipangilio ya kulala na vipengele vya ufikiaji.

  • Kichwa na maelezo: Jaribu kuonyesha kile ambacho wageni wanapaswa kujua kuhusu sehemu yako. Tumia lugha jumuishi ili udhihirishe kwamba unakaribisha watu wa aina zote.

  • Vistawishi: Chagua kutoka kwenye orodha ya awali ya machaguo unapowekwa. Baada ya kuchapisha tangazo lako, vinjari orodha kamili ya vistawishi na uweke kila kitu ulichonacho. Jumuisha maelezo muhimu, kama vile iwapo eneo lako lina vipengele vya ufikiaji.

  • Sheria za nyumba: Tumia sheria zako za nyumba kuweka matarajio, toa kionjo cha mtindo wako wa kukaribisha wageni na ushiriki na wageni watarajiwa taarifa muhimu kama vile sera ya kutovuta sigara.

Weka bei yako

Wewe ndiye unayechagua bei yako ya kila usiku. Bei inayopendekezwa inayoonyeshwa wakati wa Anza Kutumia Airbnb inategemea mambo kama vile mahali, vistawishi, uhitaji wa wageni na matangazo sawia. Unaweza kushikamana na bei hiyo au uweke nyingine tofauti na unaweza kuibadilisha wakati wowote.

Kuelewa uhitaji wa mahali husika kunaweza kukusaidia kupanga bei ya eneo lako kwa ushindani. Angalia bei za wastani za matangazo sawia yaliyowekewa nafasi karibu nawe moja kwa moja kutoka kwenye kalenda yako. Pia unaweza kujaribu kutumia nyenzo yetu ya Upangaji bei Kiotomatiki, ambayo hurekebisha kiotomatiki bei yako ya kila usiku kulingana na uhitaji.

Mapunguzo na promosheni zinaweza kuwavutia wageni katika hali mahususi. Hizi ni pamoja na promosheni ya tangazo jipya, ambayo inachukua punguzo la asilimia 20 kwenye bei yako ya kila usiku kwa nafasi tatu za kwanza zilizowekwa, pamoja na mapunguzo kwa ukaaji wa kila wiki na kila mwezi.

Jinsi na wakati wa kulipwa

Airbnb inamtoza kila mgeni moja kwa moja kabla hajaingia. Tunakutumia pesa unazojipatia kutokana na kukaribisha wageni takribani saa 24 baada ya muda ulioratibiwa wa kila mgeni kuingia. Muda halisi ambao fedha zitaingia kwenye akaunti yako unategemea njia ya malipo unayochagua.

Njia za kupokea malipo, malipo ya benki, PayPal, Western Union na Fast Pay, kwa kutaja chache, zinatofautiana kulingana na mahali ulipo. Unaweza kuweka njia yako ya kupokea malipo sasa kisha uibadilishe wakati wowote. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi unavyolipwa kwa kukaribisha wageni.

Jitayarishe kukaribisha wageni wako wa kwanza

Wageni wanatarajia sehemu yako iwe safi na iwe na vitu muhimu. Pia wanakutarajia utoe taarifa muhimu. Hizi hapa ni njia chache za kutayarisha sehemu yako na kuwasiliana kwa ufanisi:

  • Anzisha uzoefu rahisi. Weka maelekezo ya wazi, ya hatua kwa hatua ya kuingia na kutoka, yakiwa na picha za mchakato wa kuingia.

  • Fanya mawasiliano katika nyakati muhimu. Watumie wageni ujumbe ulioratibiwa wenye taarifa za wakati unaofaa wanapoweka nafasi, kabla ya kuingia, baada ya kuwasili na wakati wa kuondoka.

  • Kuwa mwangalifu kuhusu kufanya usafi. Unda orodha kaguzi ili ujikite kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa, burudisha kila chumba kila wakati na uangalie madoa, nywele na uchafu.

  • Weka vitu vya msingi. Wageni wanatarajia sehemu yako iwe na vistawishi muhimu kama sabuni, mashuka na taulo.

  • Ongeza vitu kadhaa vya ziada. Fikiria kutoa zawadi ya ukaribisho na kutoa vitu kama vile adapta za umeme na michezo ya ubao ili kufanya sehemu yako iwe yenye starehe zaidi.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
20 Nov 2019
Ilikuwa na manufaa?