Jinsi ya kutoa thamani bora
Wageni hutafuta matukio ambayo hutoa ubora wa kipekee kwa bei. Fikiria jinsi ya kufanya tukio lako liwe la kipekee zaidi na listahili bei ambayo wageni hulipa.
Kuboresha tukio
Upekee, utaalamu, uhusiano, eneo na kutegemeka, haya yote yana matokeo kwenye thamani ya jumla. Wenyeji waliopewa ukadiriaji wa juu wanasema wanavipa kipaumbele vidokezi hivi ili kutoa thamani nzuri kwa bei.
- Fanya shughuli zako ziwe mahususi. Pata maelezo kuhusu mambo yanayopendwa, lugha na kadhalika kuhusu kila kikundi kwenye kichupo cha Leo na kwenye uzi wa ujumbe wa kikundi. Zingatia kupanga shughuli kulingana na mambo wanayopenda.
- Boresha kile unachoweza. Kutoa nyenzo zenye ubora wa juu na hadithi fupi zilizofanyiwa utafiti vizuri kunaweza kusaidia sana. Hii ni kweli hata kwa maboresho madogo, kama vile kutumia viambato vya kikaboni.
- Fuatilia wageni. Tuma ujumbe wa kuwashukuru wageni na ushiriki picha na mapendekezo. Maboresho haya ya ziada yanaweza kuwasaidia wageni wajihisi wanajaliwa na wana uhusiano.
"Ninatuma ramani mahususi ya mapendekezo baada ya tukio," anasema Justin, ambaye anaandaa ziara za matembezi jijini Sydney na Brisbane, Australia. “Sioni waelekezaji wengi wa watalii wa kawaida wakifanya hivyo. Ni mahali ambapo wageni wanaona thamani kubwa."
Kuweka bei yenye ushindani
Hata matukio bora yanaweza kupata ukadiriaji wa chini ikiwa wageni hawakufikiri yalistahili bei hiyo. Haya ni mambo machache ya kuzingatia unapotathmini bei yako.
- Linganisha matukio yanayofanana. Tafuta shughuli kama zako kwenye Airbnb na tovuti nyinginezo ili kulinganisha bei za eneo husika na kuelewa kilicho cha ushindani.
- Itikia mabadiliko ya uhitaji. Fanya majaribio ya bei zako kwa nyakati tofauti, siku, misimu au matukio maalumu. Kwa mfano, wikendi zinaweza kuwa maarufu zaidi kuliko siku za wiki.
- Toa mapunguzo. Mapunguzo ya muda mfupi, kwa watakaowahi na kwa kikundi kikubwa husaidia kuwavutia wageni na kujaza tukio lako. Unapoweka zaidi ya moja, mgeni hupata punguzo lolote ambalo husababisha uokoaji mkubwa zaidi wa pesa.
"Sikuzote unapaswa kuwapa watu zaidi ya kile wanachotarajia kwa bei," anasema Evren, ambaye anaandaa ziara ya matembezi ya muziki ya Soho jijini London. "Kwangu mimi, hiyo haimaanishi kuongeza maeneo zaidi ya kuzuru. Ninazingatia kutoa mchanganyiko mzuri wa ukweli na hadithi fupi za kufurahisha ili kutoa thamani bora kwa bei."
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.