Jinsi ya kufafanua aina ya sehemu unayokaribisha wageni

Pata maelezo kuhusu aina tofauti za nyumba na vidokezi vya kuchagua moja.
Na Airbnb tarehe 14 Jul 2022
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 14 Jul 2022

Vidokezi

  • Chagua aina ya nyumba ya jumla ambayo husaidia kuweka matarajio ya wageni

  • Unaweza kuweka maelezo zaidi katika hatua inayofuata

Ukarimu mzuri huanza kwa kuweka matarajio yaliyo wazi kuhusu nyumba yako. Unaweza kuwasaidia wageni kupata tangazo lako kwa kutambulisha aina ya eneo ambalo unakaribisha wageni.

Katika hatua hii, unataka kuchagua aina ya nyumba, kama vile nyumba au fleti, ambayo inaelezea vizuri sehemu yako kwa ujumla. Tutakuomba utoe maelezo mahususi zaidi katika hatua inayofuata.

Hivi ndivyo Airbnb inavyofafanua kila aina ya nyumba ya jumla:

  • Fleti: Kwa kawaida iko katika jengo lenye nyumba nyingi ambapo watu wengine wanaishi, ikiwemo kondo na roshani
  • Nyumba: Jengo huru ambalo linaweza kushiriki maeneo ya nje au kuta, kama vile nyumba za mjini na majengo yenye fleti mbili
  • Sehemu ya ziada: Kwa kawaida kwenye nyumba ya pamoja iliyo na mlango wa kujitegemea, ikiwemo nyumba za kulala wageni na vyumba vya wageni
  • Sehemu ya kipekee: Majengo ya kuvutia au yasiyo ya kawaida, kama vile nyumba ya kwenye mti, hema la miti au nyumba ya shambani
  • Kitanda na kifungua kinywa: Biashara ya utalii inayowapa wageni kifungua kinywa huku Mwenyeji akiwa kwenye eneo hilo
  • Hoteli mahususi: Biashara ya utalii yenye mtindo wa kipekee au sura inayobainisha utambulisho wake

    Ikiwa sehemu yako inatoshea zaidi ya aina moja ya nyumba, chagua ile unayodhani ni sahihi zaidi.

    Kwa mfano, hebu tuseme unaweka tangazo la studio ndogo yenye starehe katika ua wako wa nyuma. Unaweza kuchagua Sehemu ya ziada (Nyumba ya kulala wageni) au Sehemu ya kipekee (Kijumba), kulingana na aina ya sehemu unayodhani inafanana nayo sana.

    Hakuna jibu lisilo sahihi hapa, maadamu unawapa wageni hisia ya kweli ya nini cha kutarajia ikiwa wataweka nafasi kwenye eneo lako. Tutakuomba uweke maelezo mengine katika hatua inayofuata na unaweza kubadilisha machaguo yako baada ya kuchapisha tangazo lako.

    Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

    Vidokezi

    • Chagua aina ya nyumba ya jumla ambayo husaidia kuweka matarajio ya wageni

    • Unaweza kuweka maelezo zaidi katika hatua inayofuata

    Airbnb
    14 Jul 2022
    Ilikuwa na manufaa?