Airbnb Vyumba, kipengele kipya kabisa cha vyumba vya kujitegemea

Unaweza kushiriki na wageni maelezo zaidi kukuhusu kwenye Safu yako Mpya ya Mjue Mwenyeji.
Na Airbnb tarehe 17 Jan 2024
video ya dakika 4
Imesasishwa tarehe 17 Jan 2024

Maelezo ya mhariri: Makala haya yalichapishwa kama sehemu ya Airbnb 2023 Toleo la Kiangazi. Taarifa zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu toleo letu la hivi karibuni.

Airbnb ilianza kama njia ya bei nafuu kwa wasafiri kukaa katika nyumba ya mtu mwingine. Kwa miaka mingi, Wenyeji wa vyumba vya kujitegemea wameleta watu pamoja na kuwasaidia wageni kuchunguza maeneo mapya kama wenyeji wakazi.

Leo, watu wanataka kusafiri kwa bei nafuu, hasa ukizingatia uchumi wa sasa. Na baada ya miaka ya upweke wakati wa janga la ugonjwa, wanatafuta njia za kuungana na wengine na kuwa na uzoefu wa kweli.

Ndiyo sababu tunawaletea Airbnb Vyumba, kipengele kipya kabisa cha vyumba vya kujitegemea. Maboresho hujumuisha:

  • Safu ya Mjue Mwenyeji, ili wageni waweze kukujua kabla ya kuweka nafasi

  • Aina mpya ya Vyumba na vichujio vya utafutaji vilivyoundwa upya ambavyo hufanya iwe rahisi kwa wageni kugundua vyumba vya kujitegemea

  • Maelezo mapya yanayohusiana na faragha kwa starehe ya kila mtu

Mjue Mwenyeji

Wageni wametuambia wanataka kujua ni nani ambaye watakuwa wakishiriki naye sehemu kabla ya kuweka nafasi ya chumba cha kujitegemea. Safu yako ya Mjue Mwenyeji sasa inakupa njia zaidi za kujitambulisha kwa wageni. Pia huleta maelezo kwenye wasifu wako na kuyaangazia katika utafutaji na kwenye tangazo lako.

Mabadiliko ya kwanza utakayoyaona ni kwamba picha yako ya wasifu inaonekana kwenye kona ya picha yako kuu ya tangazo. Mgeni anaweza kugusa au kubofya ili kwenda kwenye safu yako ya Mjue Mwenyeji na maelezo machache ambayo umeshiriki kuhusu wewe mwenyewe.

Jina lako, miaka ukikaribisha wageni, ukadiriaji wa nyota na idadi ya tathmini za wageni zinaonekana upande wa juu wa safu yako ya Mjue Mwenyeji. Chini ya hapo, sehemu mpya za wasifu wako hukuruhusu kushiriki mambo kama vile mahali unapoishi, mambo unayopenda, jina la mnyama kipenzi, ukweli wa kufurahisha, na kinachofanya kukaa kwako kuwe maalumu.

Unaweza kuchagua picha na taarifa unayoshiriki kwa kuhariri wasifu wako. Pia, unaweza kugundua sehemu zilizotangulia za wasifu wa Mwenyeji zina muundo mpya, kwa hivyo ni wazo zuri kuhakikisha kazi yako, lugha na mahali ulipo zinaonekana jinsi unavyotaka zionekane.

Pata vidokezi vya kupiga picha nzuri ya safu ya Mjue Mwenyeji

Aina ya Vyumba

Ni rahisi kwa wageni kuona tangazo lako kupitia Aina mpya ya Vyumba iliyo juu ya ukurasa wa kwanza. Kichujio cha utafutaji kilichobuniwa upya pia hufanya iwe rahisi kubadilisha kati ya vyumba vya kujitegemea, nyumba nzima, na aina zote za sehemu. Bei ya wastani ya chochote ambacho mgeni huchagua huonyeshwa kwenye kichujio.

Kuanzia tarehe 3 Mei, tangazo lako linahitaji kukidhi vigezo hivi vyote ili kujumuishwa katika Aina ya Vyumba:

  • Mgeni ana chumba chake cha kulala cha kujitegemea kikiwa na mlango.

  • Mgeni anaweza kufikia bafu la kujitegemea au la pamoja.

  • Mgeni anaweza kufikia angalau sehemu moja ya pamoja, kama vile jiko, sebule, au ua wa nyuma.

  • Wenyeji wanatumia majina yao kwenye tangazo lao, badala ya majina ya biashara au majina mengine.

  • "Chumba cha kujitegemea" kinachaguliwa kama tangazo au aina ya chumba katika mipangilio yako ya tangazo.

  • Chumba cha kujitegemea si chumba cha pamoja, hoteli, risoti, hema, gari la malazi, nyumba ya kujitegemea (kama vile nyumba isiyo na ghorofa ya ua wa nyuma) au aina nyingine yoyote ya nyumba iliyo kwenye orodha hii.

Matangazo ambayo hayakidhi vigezo hivi vipya hayataonyeshwa kwa wageni kama Vyumba katika utafutaji au kwenye kurasa za matangazo. Unaweza kuchagua aina mpya ya tanganzo au usasishe tangazo lako ili likidhi vigezo hivi. Ikiwa ungependa tangazo lako liwekwe, au kuondolewa kwenye, Aina ya Vyumba, unaweza kutuma ombi kwenda Usaidizi wa Jumuiya.

Faragha na starehe

Wageni ambao huvinjari matangazo ya chumba cha kujitegemea mara nyingi huchunguza ili kupata maelezo ambayo huwasaidia kuhisi starehe na wapo salama. Ili kukusaidia kuweka matarajio, tumeweka taarifa hii juu kwenye ukurasa wako wa tangazo:

  • Ikiwa mlango wa chumba cha kulala una ufunguo. Wageni wanatarajia kuwa na uwezo wa kufunga mlango wao. Ikiwa chumba chako cha kujitegemea hakina kufuli, fikiria kuliweka.

  • Iwe bafu ni la kujitegemea, maalumu, au la pamoja. Kwa matangazo yote kwenye Airbnb, wageni wanahitaji ufikiaji wa bafu ambalo lina sinki, vyoo, na bomba la mvua au beseni la kuogea. Tangazo lako sasa linaweza kuangazia endapo bafu la mgeni wako ni la kujitegemea kwenye chumba, maalumu (la kujitegemea lakini linafikiwa kupitia sehemu ya pamoja, kama vile ukumbi), au linatumiwa pamoja na wengine.

  • Nani mwingine anaweza kuwa kwenye nyumba hiyo. Wageni wanataka kujua endapo watakutana na wengine wakati wa ukaaji wao, kama vile wageni wengine, wanafamilia au wanaoishi nao. Unaweza kuepuka matarajio yasiyolingana kwa kuweka maelezo kuhusu ni nani anayeweza kuwa hapo.

  • Ni kiwango gani cha mwingiliano wa kijamii cha kutarajia. Wageni mara nyingi hufurahia kutumia muda na Wenyeji, ambao wanaweza kuwasaidia kujua wanakoenda kama wenyeji wakazi. Unaweza kuonesha ni muda gani unapenda kutumia na wageni wakati wa ukaaji wao.

Ili kusasisha maelezo haya, nenda kwenye sehemu ya Vyumba na Sehemu kwenye tangazo lako.

Airbnb Vyumba na maboresho 25 kwa ajili ya Wenyeji yanaanza kutoka wiki hii kama sehemu ya Airbnb 2023 Toleo la Kiangazi.

Airbnb
17 Jan 2024
Ilikuwa na manufaa?