Jinsi ya kuchagua eneo linalofaa
Wenyeji waliopewa ukadiriaji wa juu waeleza kinachofanya eneo liwe halisi na la kipekee.
Na Airbnb tarehe 13 Mei 2025
Imesasishwa tarehe 13 Mei 2025
Wageni wanapenda kutumia muda katika maeneo ambayo huwasaidia kujihusisha na utamaduni wa eneo husika. Onyesha jinsi eneo lako lilivyo na umuhimu maalumu na kwa nini ulilichagua.
Kupata huduma inayokufaa
Eneo lako lazima angalau liwe lenye starehe, safi na salama. Linapaswa pia kuwa na maana kwa shughuli hiyo.
- Simulia historia. Elezea historia na urithi mkubwa wa eneo hilo ili kusaidia kukazia kwa nini ni muhimu. Debora, ambaye anaandaa madarasa ya upishi nyumbani kwake jijini Rome, anashiriki mapishi, nyimbo na mila nyingine ambazo bibi yake alimrithisha. "Kila kitu tunachofanya kina simulizi," anasema.
- Lifanye liwe la eneo husika. Tafuta maeneo ambayo wageni hawangeweza kupata mahali pengine popote. Ruby, ambaye anaandaa ziara ya vyakula jijini Lisbon, anasema anawapeleka tu wageni kutembelea biashara za familia za eneo husika, kama vile duka dogo la vitobosha. "Inashangaza," anasema.
Kulenga uhalisi
Chagua eneo la kukumbukwa ambalo linaonyesha utamaduni wa eneo husika.
- Toa ufikiaji wa ndani. Tembelea maeneo ambayo wageni hawangeweza kuingia wenyewe. Teresa, ambaye anaandaa mafunzo ya kuonja mvinyo jijini Lisbon, anajaribu kuongeza "jambo lisilotarajiwa," kama vile kutafuta maeneo ambayo umma hauruhusiwi kuwepo au kwenda nje ya saa za kawaida. "Hii inaleta hisia ya ugunduzi," anasema.
- Zingatia sifa ya eneo. Mandhari, sauti na ladha huchangia hisia kali ya eneo. "Mazingira yanahitaji kukusafirisha papo hapo," anasema Graciela, ambaye anaandaa mafunzo ya upishi jijini Mexico City. "Wageni wanajua ikiwa watapata huduma nzuri ndani ya dakika chache baada ya kuwasili."
Kukaribisha wageni katika eneo ambalo ni halisi na linafaa shughuli yako kunaweza kusaidia kusababisha ukadiriaji na tathmini bora.
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
13 Mei 2025
Ilikuwa na manufaa?