Pata tathmini ya kwanza ya nyota 5
Ukadiriaji na tathmini husaidia wageni kuamua iwapo tukio lako linawafaa. Tathmini nzuri zinaweza kusababisha kuwekewa nafasi zaidi na zenye mapato ya juu.
Kuwekewa nafasi za kwanza
Tumia nyenzo za kupanga bei kwenye kichupo chako cha Matangazo na mipangilio ya upatikanaji kwenye kalenda yako ili uanze.
- Weka mapunguzo. Kutoa mapunguzo ya muda mfupi, kwa watakaowahi na kwa kikundi kikubwa kunaweza kukusaidia kuanza kuwekewa nafasi na kudumisha bei yako kuwa yenye ushindani.
- Fungua upatikanaji wako. Chagua muda wa mapema zaidi ambao wageni wanaweza kuweka nafasi kwenye tukio lako. Kalenda yako imewekwa kuwa haipatikani kwa chaguomsingi.
- Punguza muda wa mwisho. Kuruhusu wageni waweke nafasi karibu na mwanzo wa tukio lako kunaweza kusaidia kuvutia nafasi zaidi zinazowekwa.
- Zipe kipaumbele nyakati zenye shughuli nyingi. Tafiti siku na nyakati maarufu kwa ajili ya matukio katika eneo lako, kama vile wikendi au sikukuu. Unaweza kuratibu matukio kutokea mara moja, kila siku au kila wiki.
Kuelewa jinsi tathmini zinavyofanya kazi
Maoni ya wageni hukusaidia kutoa huduma bora zaidi na kujenga sifa yako kama mwenyeji. Wageni wanaombwa watoe:
- Ukadiriaji wa jumla. Wageni wanakadiria kila tukio kwa kipimo cha nyota 1 hadi 5. Wastani wa ukadiriaji wako wa jumla unaonekana kwenye tangazo lako, katika matokeo ya utafutaji na kwenye wasifu wako.
- Ukadiriaji wa kina. Wageni hutoa maoni mahususi zaidi kwa kukadiria upekee, utaalamu, uhusiano, eneo, kutegemeka na thamani.
- Tathmini ya umma. Hii inaonekana kwenye wasifu wako na katika sehemu ya tathmini ya tangazo lako. Ukijibu tathmini ya umma, jibu lako litaonekana chini yake.
- Ujumbe wa faragha. Maoni haya hayaonekani kwenye tangazo lako, ni kwa ajili yako tu.
Mara baada ya kupata tathmini 3 za kwanza, utafungua vidokezi kuhusu maoni ya wageni. Tumia menyu ili kufikia sehemu ya vidokezi kwenye programu ya Airbnb.
Kuzingatia ubora
Wenyeji waliopewa ukadiriaji wa juu waeleza wanavyozidi matarajio ya wageni katika ukadiriaji wa kina.
Mbali na vidokezi hivi vya ukarimu, kumbuka Sheria za Msingi za Mwenyeji na Sera za Usalama za Kukaribisha Wageni za Airbnb. Zinaelezea matarajio ya msingi kuhusu kutoa matukio salama na yenye ubora wa juu.
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.