Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Pata tathmini ya kwanza ya nyota 5

Fahamu jinsi ukadiriaji na tathmini zinavyofanya kazi kwenye Airbnb.
Na Airbnb tarehe 13 Mei 2025
Imesasishwa tarehe 13 Mei 2025

Ukadiriaji na tathmini huchapishwa kwenye tangazo lako na husaidia wageni kuamua ikiwa huduma yako inawafaa. Maoni mazuri ya wageni hukusaidia kujenga chapa yako kwenye Airbnb na yanaweza kusababisha kuwekewa nafasi zaidi na mapato ya juu.

Kuelewa jinsi tathmini zinavyofanya kazi

Wageni wanahamasishwa kuandika tathmini mara baada ya huduma kukamilika. Maoni yao hukusaidia kutoa huduma bora zaidi. Wanaombwa watoe:

  • Ukadiriaji wa jumla. Wageni wanakadiria huduma yako kwa kipimo cha nyota 1 hadi 5. Wastani wa ukadiriaji wako wa jumla unaonekana kwenye tangazo lako, katika matokeo ya utafutaji na kwenye wasifu wako.
  • Ukadiriaji wa kina. Wageni hutoa maoni mahususi zaidi kwa kukadiria ukarimu, uaminifu na thamani. Ikiwa unatoa huduma kwenye biashara yako au sehemu ya umma, kama vile mitindo ya nywele kwenye saluni yako au kipindi cha yoga ufukweni, wataombwa pia wakadirie eneo hilo.
  • Tathmini ya umma. Hii inaonekana kwenye wasifu wako na katika sehemu ya tathmini ya tangazo lako. Ukijibu tathmini ya umma, jibu lako litaonekana chini yake.
  • Ujumbe wa faragha. Maoni haya hayaonekani kwenye tangazo lako, ni kwa ajili yako tu.

Mara baada ya kupata tathmini 3 za kwanza, utafungua vidokezi kuhusu maoni ya wageni. Tumia menyu ili kufikia sehemu ya vidokezi kwenye programu ya Airbnb.

Kuzingatia ubora

Zana za kukaribisha wageni za Airbnb zinaweza kukusaidia kuzidi matarajio ya wageni.

Toa huduma bora. Fikiria jinsi ya kufanya huduma unazotoa kuwa mahususi ili kuwasaidia wageni wajihisi wanajaliwa na wamekaribishwa.

  • Wasiliana na wageni kwenye kichupo cha Ujumbe ili kuuliza kuhusu mapendeleo ya wageni, kujibu maswali na kuunda huduma mahususi zinazotolewa.
  • Tumia majibu ya haraka ili kufanya iwe mahususi na kutuma ujumbe wa makaribisho kwa urahisi baada ya kuweka nafasi na ujumbe wa kufuatilia baada ya huduma.
  • Jumuisha marekebisho ya ziada yanayofanya huduma unayotoa ionekane kuwa ya kipekee zaidi.

Hakikisha kila kitu kinaendeshwa vizuri. Onyesha kwamba unategemeka kwa kuwa tayari, kuweka matarajio wazi na kujibu ujumbe wa wageni papo hapo kabla na baada ya kila huduma.

  • Andaa vifaa vyovyote mapema na ikiwa unasafiri kwenda kwa mgeni, zingatia njia yako ili uwasili haraka. Tumia kalenda yako ya Airbnb kuratibu muda kati ya nafasi zilizowekwa kwa ajili ya usafiri na usanidi.
  • Ratibu ujumbe utakaotumwa kwa nyakati fulani, kama vile siku moja kabla ya huduma, ili mgeni wako ajue nini cha kutarajia.
  • Washa arifa katika programu ya Airbnb na katika mipangilio ya kifaa chako ili usipitwe na ujumbe wowote.
  • Ikiwa unatoa huduma kwenye nyumba ya mtu mwingine, acha sehemu hiyo kama ulivyoipata.

Toa thamani kubwa. Bei yenye ushindani ni jambo muhimu kuhusiana na thamani. Unaweza kuweka bei zako au kuweka mapunguzo kwenye kichupo cha Matangazo.

  • Weka angalau huduma 3 kwa bei tofauti ili kuwapa wageni machaguo zaidi na kusaidia kufikia malengo yako ya mapato. Mazoea bora ni kuainisha huduma zinazotolewa katika bei ya kuingia, ya kawaida na ya juu.
  • Fikiria kuanza na bei ambayo iko chini kidogo na utathmini tena baada ya kujenga sifa yako kwenye Airbnb kupitia ukadiriaji na tathmini nzuri.
  • Weka mapunguzo ya muda mfupi, kwa watakaowahi na kwa kikundi kikubwa ili kusaidia kuwavutia wageni.
  • Vinjari Airbnb na tovuti nyinginezo kwa ajili ya huduma kama zako ili kulinganisha bei za eneo husika kuwa zenye ushindani.

Mbali na vidokezi hivi vya ukarimu, kumbuka Sheria za Msingi za Mwenyeji na Sera za Usalama za Kukaribisha Wageni za Airbnb. Zinaelezea matarajio ya msingi kuhusu kutoa huduma salama na zenye ubora wa juu.

Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Huduma kwenye Airbnb.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
13 Mei 2025
Ilikuwa na manufaa?