Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Pata hamasa na Airbnb Plus

  Onekana tofauti na muundo wa hali ya juu kabisa wa mambo ya ndani na ukarimu.
  Na Airbnb tarehe 15 Jan 2020
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 21 Apr 2021

  Vidokezi

  • Airbnb Plus ni mpango wa mwaliko maalum kwa ajili ya sehemu na ukarimu wa hali ya juu kabisa

  • Pata msukumo kutokana na msisitizo wa wenyeji wa Airbnb Plus kuhusu kuingia kwa urahisi, muundo wa kufikiria, na kutoa raha zote za nyumbani

  • Vinjari nyumba za Plus kupata msukumo wa kubuni

  • Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kuwezesha ukaribishaji wako wa wageni kwenda ngazi ya juu

  Labda umesikia juu ya Airbnb Plus, au umeona beji ya Plus kwenye tangazo katika eneo lako. Tangazo linapataje hadhi hiyo, na inamaanisha nini haswa? Haya hapa ni mambo unayopaswa kujua.

  Inavyofanya kazi
  Airbnb Plus ni mpango wa mwaliko maalum kwa ajili ya sehemu zilizobuniwa kwa hali ya juu kabisa na ukarimu wa kipekee. Ikiwa umealikwa kwenye mpango au la, matangazo ya Airbnb Plus yanaweza kuwa chanzo bora cha msukumo. Wenyeji wa Airbnb Plus huzingatia sana maelezo ambayo hufanya wageni wahisi kukaribishwa na starehe — njia nzuri kwa kila mwenyeji kuzingatia. Haya ni mambo kadhaa ambayo wenyeji wa Airbnb Plus hufanya vizuri:

  Kuingia kirahisi

  Kuingia vizuri kunatangualia ukaaji mzuri. Ndiyo sababu kila nyumba ya Airbnb Plus ina mwenyeji aliye tayari anapohitajika ili kuwasalimu wageni au kisanduku cha funguo au mfumo wa kuingia bila ufunguo unaowezesha wageni kuingia kwa urahisi kwenye nyumba hiyo wenyewe. Njia nyingine ya kuhakikisha kuingia bila shida kwa wageni wako ni kujumuisha maelekezo ya kuingia.

  Iliyobuniwa kwa uzingativu

  Ubunifu wa mambo ya ndani ni eneo ambalo wenyeji wa Airbnb Plus hufanya vyema sana. Nyumba zao mara nyingi huwa na urembo wa kipekee, na utu mwingi na hali ya mshikamano katika eneo lote. Wenyeji wa Airbnb Plus hupata njia nyingi za kufanya maeneo tofauti kwenye nyumba kuwa mazuri na ya kufurahisha. Fikiria: kona ya kupendeza ya kukaa wakati wa kusoma, baa nzuri ya kahawa, au oasisi ya nje.

  Unahitaji msukumo kwa ajili ya sehemu yako? Vinjari matangazo ya Airbnb Plus kuona njia zote sehemu iliyobuniwa kwa umakini inaweza kuvutia.

  Ikiwa na zana zote muhimu

  Moja ya ahadi za sehemu za Airbnb Plus ni kwamba hutoa starehe zote za nyumbani, kutoka kwa Wi-Fi ya kasi hadi Runinga za kidijitali. Mifano michache ni pamoja na:

   • Maji yaliyochujwa au ya chupa
   • Jiko lililo na vifaa kamili vya kupikia ikiwa ni pamoja na mafuta, viungo, vyombo, na vyombo ya kulia chakula
   • Mashuka laini
   • Pasi na kikausha nywele

   Inatunzwa vizuri

   Nyumba za Airbnb Plus zinahakikiwa kwa ajili ya ubora. Zinahitajika kuwa safi sana na kufanya kazi kikamilifu, kutoka bustani nzuri za nje hadi mabafu masafi. Mahitaji machache yanayohitajika:

    • Vifaa vyote vinafanya kazi
    • Milango ya vyumba vya kulala katika sehemu zote za pamoja zina kufuli zinazofanya kazi
    • Kila nafasi kwenye nyumba ni nadhifu, safi na haina msongamano
    Kidokezi: Fanya maeneo yawe ya kufurahisha zaidi. Fikiria: kona ya kupendeza ya kukaa wakati wa kusoma, baa nzuri ya kahawa, au oasisi ya nje.

    Ukarimu wa hali ya juu kabisa

    Wenyeji wa Airbnb Plus wanawekewa vigezo vya hali ya juu vya ukarimu kama vile vya Wenyeji Bingwa: Lazima udumishe ukadiriaji wa wastani wa wageni wa 4.8 au zaidi bila kughairi katika mwaka uliopita (isipokuwa kama kulikuwa na sababu zisizozuilika). Wakati nyumba za Airbnb Plus zinapata hadhi zao kwa mwaliko tu, mpango wa Mwenyeji Bingwa unapatikana kwa wenyeji wote wa Airbnb na unatoa faida nyingi za aina yake.

    Kwa kuzingatia ukarimu wa hali ya juu kabisa, na kwa msukumo mdogo wa kubuni kutoka nyumba za Airbnb Plus, unaweza kupangilia tangazo lako kwa kiwango cha juu!

    Vidokezi

    • Airbnb Plus ni mpango wa mwaliko maalum kwa ajili ya sehemu na ukarimu wa hali ya juu kabisa

    • Pata msukumo kutokana na msisitizo wa wenyeji wa Airbnb Plus kuhusu kuingia kwa urahisi, muundo wa kufikiria, na kutoa raha zote za nyumbani

    • Vinjari nyumba za Plus kupata msukumo wa kubuni

    • Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kuwezesha ukaribishaji wako wa wageni kwenda ngazi ya juu
    Airbnb
    15 Jan 2020
    Ilikuwa na manufaa?