Kujadili ubaguzi kwenye Maswali na Majibu kwa ajili ya Wenyeji wa Airbnb

Wenyeji wanashiriki mitazamo anuwai kuhusu kutambua upendeleo na kujenga jumuiya.
Na Airbnb tarehe 1 Apr 2019
video ya dakika 7
Imesasishwa tarehe 14 Jun 2022

Vidokezi

  • Wenyeji wanataka kufikia taarifa muhimu kuhusu wageni wao

  • Wasiwasi umeibuka kuhusu uwezekano wa picha kutumiwa vibaya kwa njia ambayo inakiuka sera yetu ya kutobagua

  • Sera ya picha ya wasifu ya mgeni wa Airbnb ni njia ya kusawazisha wasiwasi huu

Katika Airbnb, mara kwa mara tunaandaa vikao na wenyeji wetu ili kuwa na mazungumzo muhimu kuhusu mada ambazo ni muhimu zaidi kwao. Iwe tunajadili kuhusu ukadiriaji wa eneo au tathmini za wenyeji, vikao hivi vyote vina mambo machache yanayofanana—vinazungumzia ukweli, vina uwazi na vinaweza kushughulikia mada ngumu.

Kutambua mitazamo anuwai kutoka kwenye jumuiya ya wenyeji

Mwezi Oktoba mwaka 2018, Airbnb ilibadilisha jinsi picha za wasifu za wageni zinavyoonyeshwa ili kuhimiza ufanyaji maamuzi usio na upendeleo katika mchakato wa kuweka nafasi. Sasa, picha za wasifu za wageni zinaonyeshwa tu baada ya nafasi iliyowekwa kuthibitishwa.

Katika kikao cha Maswali na Majibu cha Wenyeji jijini London mwezi Aprili mwaka 2019, wenyeji walijadili matokeo ya mabadiliko haya, ambayo yalisababisha majadiliano makinifu kuhusu upendeleo na ubaguzi. Iwe tunazifahamu au la, sisi sote tuna imani na upendeleo kuhusu makundi tofauti ya kijamii na aina tofauti za watu. Na hata ingawa tunajaribu sana kutoegemea upande wowote, wakati mwingine upendeleo—iwe tunaufahamu au hatuufahamu—hutusababisha tufanye maamuzi ambayo yanaathiri wengine.

Baadhi ya wenyeji walionyesha wasiwasi kuhusu mabadiliko hayo, wakisisitiza jinsi picha zinavyoweza kuchangia katika kuwapa taarifa kuhusu wageni wao. Lakini wengine wengi, kama Dennis, walipongeza mabadiliko hayo, wakibainisha jinsi picha zinavyoweza kuchangia ubaguzi.

“Wageni wengi wamekuja kwangu na kusema, ‘Sababu iliyonifanya nikuchague [uwe mwenyeji wangu] ni kuwa nilijua kwamba sitakataliwa kwa sababu ya jinsi nilivyo,’” Dennis anasema.

Laura Chambers, ambaye alikuwa Meneja Mkuu wa Airbnb wakati huo, alifunga majadiliano hayo kwa kukiri kwamba mazungumzo kuhusu ubaguzi ni tata na yenye changamoto, lakini pia ni muhimu. Inaweza kuwa vigumu kuzungumza kuhusu ubaguzi, lakini tunapaswa kukabiliana nao moja kwa moja—tukiwa pamoja—kabla ya kupambana nao.

Kuelewa jinsi picha za wasifu za wageni zinavyofanya kazi kwenye Airbnb

Sote tuna upendeleo. Lakini kampuni kama vile Airbnb zinaweza kusaidia kuunda nyenzo ambazo zinasaidia kuzuia watu kufanya maamuzi yenye upendeleo—ndiyo sababu tuliahidi mwaka 2016 kutathmini jinsi tunavyoonyesha picha za wasifu za wageni katika mchakato wa kuweka nafasi. Sasa picha za wasifu za wageni hazionyeshwi kwa wenyeji hadi baada ya nafasi iliyowekwa kuthibitishwa, hatua ambayo huwahimiza wenyeji kufanya maamuzi yasiyo na upendeleo.

Tulifikia uamuzi huu baada ya kushiriki katika mazungumzo kadhaa na wenyeji na wageni. Ingawa wageni wengi hutoa picha, baadhi yao walituambia kwamba hawataki kushiriki picha yao wenyewe wakati wa kuweka nafasi. Pia tunatambua wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa picha kutumiwa vibaya kwa njia ambayo inakiuka sera yetu ya kutobagua.

Wakati huo huo, wenyeji wametuambia kwamba wanathamini picha za wasifu kwa sababu zinaweza kuwasaidia wenyeji na wageni kufahamiana kabla ya safari kuanza na kuwasaidia wenyeji kuwatambua wageni wanapoingia. Zaidi ya hayo, tumeona jinsi picha zinavyoweza kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha uaminifu na kukuza jumuiya.

Sera tuliyo nayo leo ilibuniwa ili kujaribu kukidhi mahitaji ya wenyeji na wageni. Lengo letu ni rahisi: kuunda ulimwengu ambapo mtu yeyote anaweza kujisikia nyumbani mahali popote. Kuonyesha picha ya mgeni kwa wenyeji baada ya kukubali nafasi iliyowekwa ni njia yetu ya kujaribu kuleta usawaziko unaofaa. Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko haya

Ili kuwapa wenyeji kama wewe udhibiti zaidi katika mchakato huu na kukusaidia kujenga uaminifu na wageni kabla ya safari, unaweza:

Hatua hizi zinaweza kusaidia kuwawezesha wenyeji wakati bado zinajaribu kupunguza ubaguzi. Sisi pia tumeunda zana za kujielimisha zinazoeleza aina tofauti za upendeleo na dhana potofu, jinsi zinavyoweza kuathiri uzoefu wa mwanajumuiya kwenye tovuti ya Airbnb na kile unachoweza kufanya ili kuzishinda.

Lakini bado kuna kazi nyingi za kufanywa na tunajua kwamba hii ni mojawapo tu ya majadiliano mengi muhimu. Tutaendelea kukutana na wenyeji ili kupata maelezo kuhusu jinsi tunavyoweza kushirikiana ili kusaidia kufanya watu wa asili zote wajisikie salama, wameheshimiwa na wamekaribishwa.

Vidokezi

  • Wenyeji wanataka kufikia taarifa muhimu kuhusu wageni wao

  • Wasiwasi umeibuka kuhusu uwezekano wa picha kutumiwa vibaya kwa njia ambayo inakiuka sera yetu ya kutobagua

  • Sera ya picha ya wasifu ya mgeni wa Airbnb ni njia ya kusawazisha wasiwasi huu

Airbnb
1 Apr 2019
Ilikuwa na manufaa?