Amua bei yako ya kila usiku

Fikiria gharama zako na matangazo yanayofanana ili kuwavutia wageni wako wa kwanza.
Na Airbnb tarehe 14 Jul 2022
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 9 Jan 2025
Amua bei yako ya kila usiku
Kupanga bei yenye ushindani
Amua bei yako ya kila usiku

Inaweza kuchukua muda na marekebisho ili kupata bei ya kila usiku inayokufaa na yenye kuvutia kwa wageni. Daima unasimamia bei yako na unaweza kuibadilisha wakati wowote.

Kupanga bei yako

Unaweka bei yako ya awali unapotangaza sehemu yako kwenye Airbnb. Bei inayopendekezwa katika sehemu ya Anza Kutumia Airbnb inategemea mambo kama vile mahali, vistawishi na uhitaji wa wageni kwa matangazo yanayofanana na hilo.

Jitahidi uwezavyo kuweka uwiano kati ya gharama zako na kile ambacho wageni wako tayari kulipa. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:

  • Gharama za kukaribisha wageni, kama vile rehani, matengenezo na kodi.
  • Thamani unayotoa, kama vile vistawishi maarufu au ukaribu na vivutio vya eneo husika.
  • Jumla ya bei ambayo wageni watalipa, ikiwemo ada zozote unazopanga kutoza.

Kusasisha maelezo ya tangazo lako, picha na vistawishi husaidia kuelezea thamani unayotoa na kuweka matarajio ya wageni.

Wakati wowote unaposasisha bei yako, unaweza kubofya Bei ya mgeni kabla ya kodi ili kupata mchanganuo wa bei yako ya msingi pamoja na ada ya huduma ya mgeni. Gusa Unapata mapato ili kuona bei yako ya msingi bila kujumuisha ada ya huduma ya mwenyeji.

Kulinganisha matangazo yanayofanana

Kulinganisha bei za nyumba sawia katika eneo lako kunaweza kukusaidia kuweka bei yenye ushindani na kuvutia nafasi zaidi zinazowekwa. Ikiwa unatoa bei hiyo hiyo kila usiku, fikiria kuweka bei za siku za wiki na wikendi. Kubadilisha bei yako kulingana na usiku kunaweza kusaidia kuongeza nafasi zinazowekwa.

Ili kulinganisha matangazo sawia:

  • Nenda kwenye kichupo cha Bei cha kalenda ya tangazo lako.
  • Chagua tarehe mbalimbali hadi siku 31.
  • Gusa Angalia matangazo sawia.

Utaona bei za wastani za matangazo sawia yaliyo karibu kwenye ramani ya eneo lako. Vitufe kwenye ramani hukuruhusu kuangalia matangazo yaliyowekewa nafasi au ambayo hayajawekewa nafasi. Sababu zinazoamua ni matangazo gani yanayofanana ni pamoja na eneo, ukubwa, vipengele, vistawishi, ukadiriaji, tathmini na matangazo mengine ambayo wageni wanavinjari huku wakizingatia lako.

"Ikiwa ninaona matangazo yanayofanana ambayo yana bei ya chini na bado nina upatikanaji, nitaangalia na kuona sababu," anasema Katie, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na Mwenyeji Bingwa huko Palm Springs, California. "Ninachambua mapambo yangu, vistawishi vyangu, sera yangu ya kughairi, ada zangu za usafi. Kuna mambo mengi yanayofanya mtu mwingine apate kuwekewa nafasi kuliko mimi.”

Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.

Wenyeji walilipwa kwa ushiriki wao katika mahojiano.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Amua bei yako ya kila usiku
Kupanga bei yenye ushindani
Amua bei yako ya kila usiku
Airbnb
14 Jul 2022
Ilikuwa na manufaa?