Kuamua ni wageni wangapi wanaoweza kukaa katika eneo lako

Jaribu kutumia vidokezi hivi ili kujua ni nani anayeweza kutoshea vizuri katika sehemu yako.
Na Airbnb tarehe 14 Jul 2022
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 16 Nov 2022

Mojawapo ya mambo ya kwanza ambayo wageni watarajiwa wanataka kujua kuhusu eneo fulani ni ukubwa wake. Kwa kubainisha idadi ya wageni unaoweza kuwapatia malazi na idadi ya vitanda, vyumba vya kulala na mabafu yanayopatikana, unaweza kuwasaidia watu waamue ikiwa sehemu yako inawafaa.

Utaweza kufanya mengi zaidi baada ya kuchapisha tangazo lako, ikiwemo kushiriki aina za vitanda na vistawishi ambavyo kila chumba cha kulala kinavyo, kama vile viango na mito ya ziada. Kwa sasa, unaweza kuzingatia idadi ya wageni ambao ungependa kuwakaribisha katika sehemu yako.

Ikiwa huna uhakika, jaribu vidokezi hivi:

  • Hesabu idadi ya vitanda ulivyonavyo. Fikiria ni watu wangapi wanaoweza kulala vizuri kwenye kila kitanda.
  • Hesabu idadi ya mabafu uliyonayo. Fikiria ni watu wangapi wanaoweza kushiriki sehemu hizo kwa starehe.
  • Weka idadi ya juu ya wageni inayokuridhisha. Kwa sababu tu eneo lako linaweza kutoshea idadi fulani ya watu, hiyo haimaanishi kwamba lazima uwe na wageni wengi kiasi hicho.
  • Jaribu kutowashangaza wageni. Ikiwa idadi ya vitanda vyako inajumuisha makochi, magodoro yenye matakia, magodoro yanayojazwa hewa au mipangilio mingine ya kawaida ya kulala, hakikisha unaelezea vitu hivyo katika hatua zijazo, kama vile unapoweka maelezo ya tangazo lako au maelezo ya picha. Kuandika ikiwa una kitanda cha mtoto au vitanda vya ghorofa vyenye vitalu kunaweza kusaidia pia.
  • Usifanye makisio yasiyohakikishwa. Kwa mfano, watu wawili wanaosafiri pamoja huenda hawajapanga kulala kwenye kitanda kimoja.

Unapokuwa tayari, tumia vitufe vya kujumlisha na kuondoa ili kuweka idadi ya juu ya wageni wako na kutambua idadi ya vitanda, vyumba vya kulala na mabafu yanayopatikana. Kaunta ya bafu inaruhusu bafu nusu (ambayo yana choo na sinki lakini hayana bomba au beseni la kuogea).

Kumbuka, unaweza kufanya mabadiliko kwenye taarifa zako, ikiwemo idadi ya vitanda na wageni wanaoruhusiwa, wakati wowote ikiwa hali yako au mahitaji yako yanabadilika.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
14 Jul 2022
Ilikuwa na manufaa?