Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Kurekebisha mipangilio yako ili kukidhi mahitaji ya eneo husika

  Kufuatilia kwa karibu mielekeo ya kusafiri kunaweza kuongeza mapato yako.
  Na Airbnb tarehe 7 Okt 2019
  Inachukua dakika 4 kusoma
  Imesasishwa tarehe 14 Mei 2021

  Vidokezi

  • Kusafiri wakati wa wikendi dhidi ya siku za kazi, mabadiliko ya msimu na hafla maalumu hubadilisha mahitaji

  • Ofisi za utalii, makundi ya mitandao ya kijamii na tovuti za kukata tiketi zinaweza kukutaarifu kuhusu hafla zinazokuja

  • Ifanye kalenda yako iwe mahususi ili upandishe au ushushe bei yako

  • Tumia zana ya Upangaji bei Kiotomatiki kwa ajili ya kupanga bei kulingana na uhitaji

   • Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kuwezesha ukaribishaji wako wa wageni kwenda kiwango cha juu

   Kwa wenyeji wa Airbnb—kama ilivyo kwa biashara nyingine yoyote— kushughulikia mabadiliko ya mahitaji linaweza kuwa jambo muhimu katika mafanikio. Unaishi katika mji maarufu kwa ajili ya ski au eneo la mapumziko wakati wa kiangazi ambapo utalii unakuwa wa msimu? Je, kuna mikutano mikubwa au matamasha katika eneo lako? Usikose fursa ya kufanya eneo lako lipatikane wakati wa tarehe maarufu na zingatia kurekebisha bei yako ili kuwavutia wageni zaidi wakati wa msimu usioakuwa na wageni wengi. Hivi ni baadhi ya vidokezi vya kukusaidia uelewe sababu ambazo zinabadilisha mahitaji ya kimsimu na jinsi ya kufaidika nazo zaidi.

   Mambo 3 muhimu yanayobadilisha mahitaji

   Andaa kalenda yako mapema mwanzoni mwa mwaka ili upange likizo zinazojulikana tayari, kisha nenda zaidi ya hapo ili uangalie hafla na mielekeo ambayo inaweza kuongeza kusafiri katika eneo lako.

   Kalenda yako ya Airbnb pia itaonyesha kiotomatiki vidokezi vya kusafiri kwa eneo lako, kama vile usiku wenye mahitaji makubwa na uwezekano wa kupata mapato kuliko kawaida. Kuyafuatilia haya kwa karibu kunaweza kusaidia kuhakikisha unaelewa mielekeo ya safari na unapatikana kwa ajili ya kukaribisha wageni ikiwa unataka kufanya hivyo.

   Sababu kuu za kuzingatia:

   1. Mielekeo ya kila wiki
   Mahitaji yanaweza kubadilika kulingana na siku ya wiki. Kwa masoko mengi, wikendi ni maarufu zaidi. Lakini kwa baadhi ya maeneo yenye safari nyingi za kikazi, siku za wiki ni maarufu zaidi.

   2. Mabadiliko ya msimu
   Kulingana na mahali sehemu yako ilipo, nyakati fulani za mwaka zitakuwa maarufu zaidi. Je, eneo lako ni maarufu kutembelewa na wageni wakati wa msimu wa baridi, au watu huwa wanakusanyika hapo wakati wa kiangazi?

   3. Siku au hafla maalumu
   Mikutano, sherehe, na hafla zingine kubwa zinafanya mahitaji yawe makubwa. Kuwa na taarifa kuhusu nini kinachokuja katika eneo lako, kuwa na mawasiliano na ofisi ya utalii ya eneo lako, jiunge kwenye makundi ya mitandao ya kijamii na jisajili kwenye tovuti kadhaa za kukatisha tiketi. Magazeti na vyuo vikuu katika eneo lako pia vinaweza kuwa nyenzo nzuri.

   Fanya mipangilio yako ya bei iwe mahususi

   Mara baada ya kuwa na uelewa mzuri wa mielekeo katika eneo lako, unaweza kuweka Upangaji bei Kiotomatiki kwa siku za wiki, wikendi, na likizo, au urekebishe bei yako wakati kuna mkutano mkubwa au hafla inayokuja kwenye eneo lako. Pia unaweza kutoa mapunguzo maalumu kwa nafasi zinazowekwa katika msimu usiokuwa na wageni wengi.

   Kwa kawaida tunapata maombi ya kuweka nafasi kwa ajili ya mkesha wa Mwaka Mpya mapema mwezi Agosti, kwa hivyo panga mapema bei zako za likizo.
   Branka and Silvia,
   Zagreb, Kroatia

   Fikiria kutumia zana ya Upangaji bei Kiotomatiki

   Je, njia rahisi ya kurekebisha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ni ipi? Washa kipengele cha Upangaji bei Kiotomatiki. Zana hii inasasisha bei yako ya kila usiku kiotomatiki kulingana na mipangilio yako na sababu zaidi ya 70 zinazobadilisha bei, kuanzia matakwa ya kimsimu hadi idadi ya tathmini nzuri ambazo tangazo lako limezipata. Zingatia tu kwamba wewe ndiye unadhibiti bei yako na kwamba zana ya Upangaji bei Kiotomatiki haitazingatia kila kitu ambacho kinaathiri bei ambayo wageni wapo tayari kuilipia, kama vile mandhari ya kupunga hewa au kiwango cha ukarimu unachotoa kwenye uzoefu wa wageni.

   Ikiwa unatumia zana ya Upangaji bei Kiotomatiki, hakikisha unaweka kiwango cha bei ya chini ili bei yako isishuke chini ya tarakimu ambayo unaitaka.

   Onekana wakati mahitaji yapo chini

   Kunapokuwa na vipindi vya mahitaji ya chini, matangazo mengi katika soko lako hayatawekewa nafasi. Zingatia kuwavutia wageni kwenye tangazo lako kwa kuweka promosheni au kushusha bei yako. Airbnb inadokeza bei zinazovutia, zile ambazo zipo chini kuliko kawaida kwa tangazo, na kuzionyesha kuwa ni promosheni nzuri. Promosheni nzuri kabisa hata zinatumwa kwa barua pepe kwa wageni ambao wanatafuta lakini bado hawajaweka nafasi.

   Jaribu mbinu hizi za mwenyeji

   Kujua kiasi cha kutoza na hata wakati gani wa kusasisha bei yako, linaweza kuwa jambo la sanaa kidogo. Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo wenyeji wamezijaribu:

   • Panga mapema. "Kwa kawaida tunapata maombi ya kuweka nafasi kwa ajili ya mkesha wa mwaka mpya kuanzia mapema mwezi Agosti, kwa hivyo kuwa mwangalifu na uweke mapema bei zako za sikukuu" —Branka na Silvia kutoka Zagreb, Kroatia
   • Tumia matakwa ya kiwango cha chini cha usiku. "Ninaweka bei za likizo kwa kiwango cha chini cha usiku nne, na Mkesha wa Mwaka Mpya unakuwa na bei ya juu kabisa." —Letti kutoka Atascosa, Texas
   • Weka bei za juu kwa tarehe za mbali. "Inamaanisha kalenda yangu inaweza kuwa wazi kwa ajili ya kuwekewa nafasi lakini kalenda yangu isijae haraka sana. Pia inatoa fursa kwa wageni ambao wanataka kuweka nafasi mapema kabla ya wakati (na kulipia bei kubwa) wafanye hivyo. " —Paul kutoka London
   • Fanya Upangaji bei Kiotomatiki ufanye kazi kwa ajili yako. "Daima unaweza kujiwekea bei mahususi kwa tarehe au vipindi maalumu ili kufuta Upangaji bei Kiotomatiki ." —Emiel kutoka Leeuwarden, Uholanzi
   • Nufaika zaidi na mahitaji ya chini. “Ninapendekeza ushushe bei kwa misimu yenye wageni wachache kuzigawanya katikati kidogo. Au utumie muda kwa ajili ya maboresho/ matengenezo kwa kuwa wageni watakuwa wengi tena na hakutakuwa na muda. ” —Sandra kutoka Daylesford, Australia
   • Tarajia kujaribu na kufanya makosa. "Mwongozo wako bora ni ikiwa eneo lako linawekewa nafasi na tathmini nzuri," -Jeff na Jess kutoka Durham, North Carolina

   Ukiwa na vidokezi na zana hizi, na utendaji kidogo unaweza kunufaika zaidi na bei yako kila siku ya mwaka.

    Vidokezi

    • Kusafiri wakati wa wikendi dhidi ya siku za kazi, mabadiliko ya msimu na hafla maalumu hubadilisha mahitaji

    • Ofisi za utalii, makundi ya mitandao ya kijamii na tovuti za kukata tiketi zinaweza kukutaarifu kuhusu hafla zinazokuja

    • Ifanye kalenda yako iwe mahususi ili upandishe au ushushe bei yako

    • Tumia zana ya Upangaji bei Kiotomatiki kwa ajili ya kupanga bei kulingana na uhitaji

     • Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kuwezesha ukaribishaji wako wa wageni kwenda kiwango cha juu
     Airbnb
     7 Okt 2019
     Ilikuwa na manufaa?