Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Njia 10 za kutumia vizuri zaidi huduma ya kukaribisha wageni wakati wa sikukuu

  Kuanzia kupanga bei yako hadi kuweka mapambo ya sikukuu, hivi ni vidokezi vyetu bora.
  Na Airbnb tarehe 1 Okt 2019
  Inachukua dakika 4 kusoma
  Imesasishwa tarehe 23 Nov 2021

  Vidokezi

  • Zingatia sana Mkesha wa Mwaka Mpya—ni mojawapo ya usiku unaowekewa nafasi nyingi zaidi kwa mwaka!

  • Kumbuka kuzuia tarehe wakati hupatikani ili kukaribisha wageni

  • Si mapema sana kuweka bei zako za msimu wenye shughuli nyingi—wageni mara nyingi huweka nafasi mapema

  • Weka mapambo ya sikukuu ili kufanya ukaaji wa wageni wako uwe wa kukumbukwa zaidi

  Sikukuu zimekaribia. Je, uko tayari kwa ajili ya msimu wenye shughuli nyingi za kuweka nafasi? Kuanzia kunufaika na uhitaji mkubwa hadi kuweka mapambo ya sikukuu katika sehemu yako yote, kuna njia nyingi za kuutumia vizuri zaidi wakati huu wa mwaka. Hivi ni vidokezi vyetu 10 bora.

  1. Epuka pilkapilka

  Je, unajua kwamba Mkesha wa Mwaka Mpya ni mojawapo ya usiku unaowekewa nafasi nyingi zaidi kwenye Airbnb kwa mwaka? “Kwa kawaida sisi huwekewa nafasi za Mkesha wa Mwaka Mpya mapema kama mwezi Agosti,” wanasema Branka na Silvia kutoka Zagreb, Kroatia. Na si Mwaka Mpya tu. Wageni kwa kawaida hupanga mipango yao ya kusafiri miezi kadhaa mapema, kwa hivyo si mapema sana kusasisha kalenda yako kwa ajili ya msimu. Usichotaka ni mtu kuweka nafasi ya sehemu yako kabla hujapata nafasi ya kusasisha bei, upatikanaji na matakwa mengine.

  2. Panga kalenda yako

  Je, mipango yako ya sikukuu ipo? Hakikisha kwamba umezuia tarehe zozote kwenye kalenda yako wakati hutaweza—au huenda usipatikane—ili kukaribisha wageni. Na ikiwa unatangaza sehemu yako kwenye tovuti nyingine, tumia kipengele cha uoanishaji wa kalenda ili kuepuka kuwekewa nafasi mara mbili na ughairi unaohusishwa.

  3. Zingatia matukio maalumu

  Mbali na sikukuu kama vile Diwali, Hanukkah, Krismasi na Kwanzaa, baadhi ya miji ina hafla maalumu ambazo huvutia wageni wengi. Je, kuna sherehe au tamasha zozote maarufu za eneo lako zinazokaribia? Tarehe hizi zitakuwa muhimu kujua unapoweka kalenda yako. Endelea kupata habari za hivi punde kuhusu kile kinachokuja katika eneo lako kwa kuwasiliana na ofisi ya utalii ya eneo lako, kujiunga na makundi ya mitandao ya kijamii na kujisajili ukitumia programu ya matukio au tovuti.

  4. Fanya marekebisho kwenye bei

  Fanya utafiti kidogo wa soko ili kujua jinsi ya kuweka bei bora ya sehemu yako kwa ajili ya msimu. Hiyo inamaanisha kuangalia ushindani, iwe ni wenyeji wengine wa Airbnb au hoteli za eneo lako. Una chaguo jingine? Washa kipengele cha Upangaji bei Kiotomatiki, ambacho kitasasisha bei yako ya kila usiku kiotomatiki kulingana na mipangilio yako na sababu nyingine zaidi ya 70 zinazoweza kuathiri bei, ikiwemo uhitaji wa kimsimu. Hakikisha kwamba umeweka kima cha chini cha bei, ili kisiwahi kuwa chini ya nambari inayokuridhisha.

  5. Fikiria kuwahitaji wageni kuweka nafasi ya muda wa chini wa kukaa

  Mara baada ya kufahamu sikukuu zote na tarehe nyingine muhimu, fanya mipangilio iwe mahususi kwenye kalenda yako. Wenyeji wengi huchagua kuwahitaji wageni kuweka nafasi ya muda wa chini wa kukaa kwa tarehe maarufu. Kuhitaji wageni waweke nafasi ya idadi ya chini ya usiku kunaweza kumaanisha muda mfupi wa kusimamia sehemu yako—na kufanya usafi!—huku ukiongeza mapato yako.

  6. Pitia Sheria za Nyumba yako

  Kukiwa na sherehe zote zijazo, sasa ni wakati mzuri wa kufafanua kile ambacho wageni wanaweza na hawawezi kufanya katika sehemu yako. Je, wanaruhusiwa kuandaa karamu ya Mkesha wa Mwaka Mpya? Vipi kuhusu kuwakaribisha wanafamilia wachache kwa ajili ya chakula cha jioni cha Sikukuu ya Kutoa Shukrani? Unaweza kutaka kufanya Sheria za Nyumba yako ziwe kali zaidi au kuzilegeza wakati huu wa mwaka na kuwakumbusha wageni kwamba wanahitaji kukubaliana na sheria zako kabla ya kuweka nafasi. Ujumbe wa Mhariri: Tulisasisha Sera yetu ya Sherehe na Hafla mwezi Desemba mwaka 2019—tunakuhimiza utathmini mabadiliko hayo, hasa unapojitayarisha kuwakaribisha wageni wakati wa msimu wa sherehe.

  7. Karibisha familia

  Kwa wazazi wanaosafiri na watoto, sehemu inayofaa familia inaweza kuwa sababu ya kusherehekea. Vutia wageni wengi zaidi na ufanye uzoefu wao uwe wa kufurahisha zaidi kwa kuweka vistawishi vinavyopendwa na familia, kama vile kitanda cha mtoto, kiti ambacho mtoto hukalia anapokula, midoli na michezo ya ubao. Fikiria pia kutoa taarifa ili kuwasaidia wageni wako kunufaika zaidi na jiji lako. Mwenyeji Bingwa Elsie kutoka Nashville anaielezea katika kitabu chake cha mwongozo. "Kuwa na sehemu mahususi katika kitabu chako cha mwongozo kwa ajili ya shughuli za kufanya na watoto huleta utofauti."

  8. Weka mapambo ya sikukuu

  Je, ungependa kuwaundia wageni ukaaji wa kipekee? Acha msimu ukuhamasishe, kuanzia kuleta mapambo ya sikukuu hadi kushiriki vyakula na desturi za eneo lako. “[Guests] wanathamini sana jitihada za ziada na kujihisi 'wakiwa nyumbani',” wanasema wenyeji Kelly na Larry kutoka New Braunfels, Texas. "Ninafurahi ninapowaona kwenye baraza huku maboga yakiwa yanatoa mwangaza au karibu na mti wa Krismasi wakinywa kinywaji moto cha chokoleti kwenye vikombe nilivyowaachia."

  9. Kumbuka hali ya hewa

  Je, eneo lako hupata theluji nyingi katika msimu wa sikukuu? Au pengine majira ya joto ya eneo lako huanza mwezi Desemba. Huenda wageni wasifahamu hali ya hewa ya kawaida ya eneo lako. Fikiria kuweka vitu vyovyote muhimu kwenye sehemu yako kama vile miavuli, koleo za theluji au hata losheni ya kuzuia miale ya jua—aina hizi za vistawishi husaidia sana kuwafanya wageni wastareheke. Na kumbuka kutoa maelekezo yoyote wanayohitaji kujua. Kwa mfano, mwenyeji Monica kutoka Ormstown, Kanada, anawaambia wageni hivi: “Theluji kwenye barabara binafsi inayoelekea kwenye nyumba huondolewa na mojawapo ya matrekta yetu theluji inapokoma kundondoka; ngazi za mbele na sehemu kati ya ngazi ni jukumu la mgeni.”

  10. Usisahau kuhusu usalama

  Kuhusiana na hali ya hewa, hita zako za gesi, jenereta na dohani zinaweza kutumika zaidi katika miezi ya baridi. Matumizi hayo husababisha hatari kubwa ya mioto ya nyumbani na sumu ya kaboni monoksidi (CO). Weka vifaa kwenye sehemu yako kama vile kizima moto kimoja au zaidi, pamoja na king'ora cha moshi na kaboni monoksidi. Pia ni wazo nzuri kuhakikisha kwamba dohani na matundu ya kupasha joto yanafanyiwa matengenezo kila mwaka, kwa kuangalia vitu kama vile mizibo na kutu. Ni wakati wa mwaka wenye shughuli nyingi—chukua tahadhari kadhaa rahisi na uondoe usalama kwenye mahangaiko yako.

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Zingatia sana Mkesha wa Mwaka Mpya—ni mojawapo ya usiku unaowekewa nafasi nyingi zaidi kwa mwaka!

  • Kumbuka kuzuia tarehe wakati hupatikani ili kukaribisha wageni

  • Si mapema sana kuweka bei zako za msimu wenye shughuli nyingi—wageni mara nyingi huweka nafasi mapema

  • Weka mapambo ya sikukuu ili kufanya ukaaji wa wageni wako uwe wa kukumbukwa zaidi

  Airbnb
  1 Okt 2019
  Ilikuwa na manufaa?