Angalia zana mpya kwa ajili ya tukio lako
Programu mpya ya Airbnb ina kila kitu unachohitaji ili kusimamia tukio lako. Zana zako za kukaribisha wageni zinakusaidia kurahisisha ratiba, kuvutia nafasi zinazowekwa, kuwasiliana na wageni, kuelewa mapato na kupata vidokezi kuhusu ukadiriaji na tathmini.
Utapata zana zilizopangwa kwenye vichupo hivi 5 wakati umeingia kwenye akaunti kama mwenyeji.
Leo
Kichupo kipya cha Leo ndicho unachokiona unapofungua programu. Unaweza kuona maelezo ya nafasi iliyowekwa kwa ufupi ili kusaidia kupanga siku yako na kutoa ukarimu wa kipekee.
- Badilisha kati ya mionekano ya nafasi zilizowekwa za leo na nafasi zilizowekwa zinazokaribia ili ujue ni nani unayemkaribisha na wakati gani.
- Jiandikie maelezo kuhusu nafasi zilizowekwa, kama vile vikumbusho kuhusu matukio au maombi maalumu.
- Pata vidokezi kuhusu mambo ya kufanya kwa kila nafasi iliyowekwa, kama vile kutoa maelezo muhimu ili kuwasaidia wageni kuwa tayari.
Kalenda
Kalenda iliyoundwa upya inajumuisha mtazamo mpya wa kila siku unaofaa. Unaweza kutathmini na kusasisha ratiba yako kwa urahisi, kila saa.
- Weka upatikanaji kwa ajili ya tukio lako na uchague matukio ambayo ungependa kurudia mara kwa mara.
- Oanisha kalenda zako za Airbnb na Google ili ufuatilie kila kitu katika sehemu moja.
- Angalia idadi ya wageni waliothibitishwa kwa kila tukio uliloratibu.
- Weka bei mahususi kwa tarehe na nyakati mahususi ili kuvutia kuwekewa nafasi.
Wageni wanaweza kuweka nafasi papo hapo kwenye siku yoyote isiyowekewa nafasi kwenye kalenda yako, kwa hivyo ni muhimu kusasisha upatikanaji wako.
Matangazo
Kichupo cha Matangazo kinakusaidia kusimamia maelezo ya tangazo lako. Unaweza kurekebisha bei zako na kuonyesha tukio kwa wageni.
- Weka mapunguzo ya muda mfupi, kwa watakaowahi na kwa kikundi kikubwa ili kuwashawishi wageni kuweka nafasi.
- Shiriki picha za tangazo zenye ubora wa juu ili kuweka matarajio wazi na kusaidia tangazo lako lionekane.
- Endelea kusasisha utaratibu wa safari yako unapofanya mabadiliko kwenye eneo au shughuli zako.
- Hariri mipangilio kama vile ukubwa wa kikundi, muda wa mwisho kuweka nafasi na ufikiaji wa mwenyeji mwenza kwenye tangazo lako.
- Weka vipengele vya ufikiaji, ikiwemo vipengele vya sauti na kuona.
Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Matukio ya Airbnb.
Ujumbe
Kichupo cha Ujumbe kinakusaidia kuwasiliana na wageni kabla, wakati na baada ya tukio. Utatuma ujumbe kwenye uzi wa kikundi ambao umeundwa kiotomatiki kwa kila tukio.
- Shiriki video au picha ili ujitambulishe kabla au ufupishe matukio ya kukumbukwa baada ya tukio.
- Mtumie mgeni ujumbe moja kwa moja ili kufuatilia maombi mahususi ikiwa inahitajika.
- Jibu maswali ya kawaida kupitia majibu ya haraka yanayoweza kufanywa kuwa mahususi ambayo yaliandikwa mapema au uunde violezo vyako mwenyewe.
- Ratibu majibu ya haraka ili kutuma maelezo muhimu kiotomatiki katika nyakati muhimu, kama vile wakati wa kuweka nafasi na siku moja kabla ya tukio.
- Wasiliana na Airbnb Usaidizi au utume ujumbe kwa mwenyeji unapotumia programu kama mgeni.
Menyu
Menyu inakupa ufikiaji wa mapato yako, vidokezi na mipangilio mingine. Utapata vidokezi mahususi na nyenzo zaidi ili kusaidia kukuza biashara yako ya kukaribisha wageni.
- Angalia mapato yako na uunde ripoti mahususi kwenye dashibodi ya mapato.
- Angalia maoni ya wageni na uone jinsi ukadiriaji wako wa jumla unavyolinganishwa na matukio yanayofanana katika sehemu ya vidokezi iliyoundwa upya.
- Simamia mipangilio ya akaunti yako na upate nyenzo za kukaribisha wageni.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.