Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Toleo la mwezi Mei mwaka wa 2022 la Airbnb: Habari ya hivi karibuni kuhusu Matukio

Kile ambacho Wenyeji wa Matukio wanahitaji kujua kuhusu mabadiliko kwenye programu na tovuti ya Airbnb.
Na Airbnb tarehe 11 Mei 2022
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 11 Mei 2022

Vidokezi

  • Tumebuni upya vipengele kwenye tovuti na programu yetu—mabadiliko yetu makubwa zaidi katika muongo mmoja

  • Matukio ya ana kwa ana na ya Mtandaoni sasa yanaonekana wakati wageni wanatumia upau wa utafutaji au sehemu ya eneo

  • SEO na mitandao ya kijamii zinaweza kuwa nyenzo muhimu za kuwaelekeza wageni kwenye tangazo lako

Kila sehemu ya kukaa na Tukio kwenye Airbnb ni ya kipekee. Lakini utafutaji wa kawaida wa usafiri unaweza kufanya iwe vigumu kuzipata. Hiyo ni kwa sababu wakati watu wanalazimika kuweka eneo na tarehe mahususi kwenye kisanduku cha utafutaji, wanapata tu matokeo yanayolingana na kile wanachoandika kwenye kisanduku hicho.

Kama sehemu ya Toleo la mwezi Mei mwaka wa 2022 la Airbnb, tunakuletea programu na tovuti mpya kabisa iliyoundwa kwa kuzingatia Aina za Airbnb. Wageni wanapovinjari Airbnb, wanapewa zaidi ya aina 50 ambazo huweka matangazo kwenye makusanyo yaliyopangwa kulingana na mtindo, eneo au ukaribu wao na shughuli ya usafiri.

Tovuti na programu ya Airbnb zilibuniwa upya ili kusaidia matangazo kugunduliwa na wageni wengi wa aina mbalimbali mapema katika mipango yao ya safari. Hapa kuna baadhi ya majibu kwa maswali ya kawaida kuhusu jinsi hii inavyowaathiri Wenyeji wa Matukio.

Ni nini kinachobadilika?

Kwa wageni wanaotumia kivinjari cha wavuti, Aina za Matukio na Matukio ya Mtandaoni sasa zinaonekana wanapobofya kisanduku cha utafutaji ili kuchagua tarehe au mahali wanakoenda.

Wageni wanaotumia programu ya simu ya mkononi wanaweza kupata Matukio kwa kubofya kisanduku cha utafutaji cha juu ili kuchagua tarehe au mahali wanakoenda.

Wageni wanawezaje kutafuta Matukio?

Wageni wanapokuwa kwenye Airbnb.com, wanaweza kubofya kwenye sehemu ya utafutaji ili kubadilisha utafutaji wao kutoka Sehemu za Kukaa kwenda Matukio au Matukio ya Mtandaoni.

Wageni wanaotumia programu ya simu ya mkononi wanaweza kubofya kwenye upau wa utafutaji ili kubadilisha kutoka Sehemu za Kukaa kwenda Matukio au Matukio ya Mtandaoni. Matukio ya Mtandaoni hayawezi kutafutwa kwenye toleo la iOS kwa wakati huu.

Wageni wanapoweka nafasi ya sehemu ya kukaa, bado wataonyeshwa Matukio ya karibu katika sehemu ya Safari ya Airbnb.com na programu ya simu ambayo wanaweza kuvinjari.

Unaweza kuwasaidia vipi wageni kupata Tukio lako?

Njia moja unayoweza kusaidia kuwaelekeza wageni kwenye Tukio lako ni kutumia maneno yanayotafutwa mara kwa mara kwenye tangazo lako. Kwa mfano, kuweka maneno muhimu ya utafutaji kwenye kichwa na maelezo ya tangazo lako kunaweza kufanya iwe rahisi kwa wageni wanaotafuta maneno hayo kupata Tukio lako.

Unaweza pia kutangaza Tukio lako kwenye mitandao ya kijamii. Hizi ni njia chache ambazo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kueneza ujumbe kuhusu tangazo lako:

  • Chapisha kwa umma na mara kwa mara ili kuwafikia watu wengi kadiri iwezekanavyo

  • Jumuisha kiunganishi cha Tukio lako, ili wageni waweze kuweka nafasi kwa urahisi

  • Wahimize wageni wakutambulishe pamoja na #airbnbexperiences au #airbnbonlineexperiences— na wanapofanya hivyo, hakikisha kwamba unapenda, unatoa maoni na kushiriki maudhui yao

Pata maelezo zaidi kuhusu Toleo la mwezi Mei mwaka wa 2022 la Airbnb

Vidokezi

  • Tumebuni upya vipengele kwenye tovuti na programu yetu—mabadiliko yetu makubwa zaidi katika muongo mmoja

  • Matukio ya ana kwa ana na ya Mtandaoni sasa yanaonekana wakati wageni wanatumia upau wa utafutaji au sehemu ya eneo

  • SEO na mitandao ya kijamii zinaweza kuwa nyenzo muhimu za kuwaelekeza wageni kwenye tangazo lako

Airbnb
11 Mei 2022
Ilikuwa na manufaa?