Airbnb 2022
Toleo la Mei

Tunakuletea Airbnb mpya

Safu mbili za picha nzuri za tangazo zinaonyesha nyumba katika Aina za Airbnb ambazo ni Kasri, Jangwa, Ubunifu, Ufukwe na Mashambani. Mojawapo ya matangazo yanaonyeshwa kwenye skrini ya simu ya mkononi, yakionyesha jinsi matangazo yatakavyoonekana kwenye programu ya Airbnb.

Watu wanaweza kubadilika zaidi kuliko hapo awali kuhusu mahali na wakati wanaposafiri. Ili kuwasaidia wanufaike na fursa hizi mpya, tunawaletea mabadiliko yetu makubwa zaidi katika muongo mmoja, ikiwemo njia mpya kabisa ya kutafuta, njia bora ya kukaa muda mrefu na kiwango cha ulinzi kisicho na kifani.

Njia mpya ya kutafuta

Tunakuletea muundo mpya kabisa, unaotegemea Aina za Airbnb, ili kuwasaidia wageni wetu wachunguze ulimwengu wa Airbnb kwa urahisi na kugundua maeneo ambayo wasingeyajua ili watafute.

Kompyuta mpakato iliyofunguliwa na simu ya mkononi zinaonyesha ukurasa mpya wa mwanzo wa Airbnb, ambapo picha za tangazo kutoka kwenye Kitengo cha Ubunifu cha Airbnb zinaonyeshwa. Safu ya ikoni kwenye sehemu ya juu ya ukurasa inaonyesha aina tofauti ambazo mgeni anaweza kuchunguza.

Aina za Airbnb. Imebuniwa ili kuwasaidia wageni wagundue nyumba za kipekee.

Wenyeji wetu hutoa mamilioni ya nyumba za kipekee duniani kote. Aina za Airbnb huzipanga kwenye mkusanyo kukiwa na zaidi ya aina 50 za nyumba zilizochaguliwa kwa ajili ya mtindo wake, eneo au shughuli za karibu. Zinajumuisha:

Kukutana na Kitengo cha Ubunifu

Wageni sasa wanaweza kugundua kwa urahisi nyumba zaidi ya 20,000 zilizochaguliwa kwa sababu ya usanifu na sehemu zake za ndani ambazo ni maarufu, ikiwemo kazi bora za wasanifu majengo kama vile Frank Lloyd Wright na Le Corbusier.

Nyumba ya matofali ya kuvutia ya Frank Lloyd Wright iko katika mazingira ya asili yenye madirisha yanayotoka sakafuni hadi darini yanayofunika upande mmoja mzima.
Frank Lloyd Wright
Mwenyeji ni Marika
Mnara wa saruji wa Le Corbusier una urefu unaoelekea kwenye anga ya bluu —Muundo wake unaunda maumbo ya kijiometri angani, huku sanamu ya bluu ya mtu aliyevaa suti ikionekana kutoka sakafuni.
Le Corbusier
Mwenyeji ni Elodie
Sehemu ya ndani ya nyumba ya Taalman Architecture inaonyesha dari ya mbao, sakafu za mawe na mahali pa kuotea moto ambapo pamening'inia kwenye dohani yake.
Usanifu Majengo wa Taalman
Mwenyeji ni Linda
Nyumba kama ya kontena iliyotengenezwa kwa chuma cha rangi ya chungwa imeonyeshwa kwenye anga wazi, mkalitusi ukiwa unaonekana kwenye mandhari ya mbele.
Robert Nichol & Sons
Mwenyeji ni Dayget
Nyumba nyeupe, ya kisasa iliyobuniwa na Steven Holl, imepigwa picha wakati wa jioni na kuangazwa kwa joto kutoka ndani.
Steven Holl
Mwenyeji ni Sarah
Sehemu ya ndani yenye mapambo machache ingawa ina mwonekano wa kupendeza wa sehemu ya kulia chakula imepigwa picha, katika nyumba iliyobuniwa na William Turnbull Jr.
William Turnbull Jr.
Mwenyeji ni Miju
Nyumba ya Cameron Anderson Architects iko chini ya mwezi mpevu. Madirisha yake na mlango mkubwa ulio wazi unaonyesha sehemu ya ndani ya mbao yenye joto, wakati matuta ya chuma yenye mikunjo ya kuta zake za nje yanaonyesha mbalamwezi.
Cameron Anderson Architects
Mwenyeji ni Rick na Steph
Jengo la kushangaza la rangi ya pipi waridi lenye madirisha ya kipekee, lililobuniwa na Ricardo Bofill, linatofautishwa na anga angavu ya bluu
Ricardo Bofill
Mwenyeji ni Hans

Jinsi tunavyounda Aina za Airbnb

Imechaguliwa miongoni mwa nyumba milioni sita

Wenyeji wa Airbnb hutoa mkusanyiko mkubwa zaidi wa nyumba za kipekee ulimwenguni, kuanzia nyumba za kwenye miti hadi vijumba, katika zaidi ya miji 100,000 katika nchi 220.

Imechambuliwa kupitia uchanganuzi wa kiotomatiki wa kikompyuta

Tunatathmini matangazo kwenye Airbnb kupitia uchanganuzi wa kiotomatiki wa kikompyuta ili kuchambua vichwa, maelezo yaliyoandikwa, tathmini za wageni, maelezo mafupi ya picha na takwimu nyinginezo.

Zimepangwa na Airbnb

Wanatimu wa upangaji wa Airbnb hutathmini matangazo na kuchagua kwa makini picha zilizoonyeshwa. Kisha kila aina hupitia tathmini ya mwisho ili kukagua uthabiti na ubora wa picha.

Tunakuletea kukaa kwenye Nyumba Mbili

Watu wengi wanaenda safari ndefu kuliko hapo awali. Ili kuwapa machaguo mengi hata zaidi wanapopanga, tumeanzisha huduma ya Kukaa kwenye Nyumba Mbili, kipengele kipya cha ubunifu kinachogawanya safari kati ya nyumba mbili tofauti, sasa wageni wanaweza kupata wastani wa matangazo asilimia 40 zaidi wanapotafuta sehemu hizo za kukaa za muda mrefu.

Njia bora ya kukaa muda mrefu

Skrini ya simu ya mkononi inayoonyesha Kukaa Kwenye Nyumba Mbili. Skrini inasema: "Gawanya wakati wako kati ya Norrebro na Gammelholm" kisha inaonyesha bei ya safari hiyo. Hapa chini kuna picha mbili za nyumba hizo. Picha ya Norrebro inaonyesha chumba cha kulia chakula kilicho na rafu kubwa ya vitabu ya rangi ya kijivu na shada la taa za kisasa. Picha ya Gammelholm inaonyesha chumba kingine cha kulia chakula, hiki kikiwa na mwangaza mkubwa wa jua. Kila picha ina maelezo ya tarehe, ambayo yanaonyesha wazi kwamba mgeni atakaa siku 12 huko Norrebro, ikifuatiwa na siku 18 katika nyumba ya Gammelhorm.

Nyumba mbili katika eneo moja

Wageni wanapotafuta sehemu ya kukaa ya muda mrefu katika eneo moja, tutampa chaguo la kugawanya safari yake kati ya nyumba mbili tofauti katika eneo hilo.

Skrini ya simu ya mkononi inayoonyesha Kukaa kwenye Nyumba Mbili kutoka kwenye Aina ya Hifadhi za Taifa. Skrini inasema "Gawanya wakati wako kati ya Ziona na Grand Canyon," pamoja na bei ya safari iliyopendekezwa. Hapa chini kuna picha mbili zilizopangwa pembeni. Picha ya Zion inaonyesha hema lenye nafasi kubwa, linalong'aa chini ya anga lenye giza. Picha ya Grand Canyon inaonyesha bwawa la nje lenye mandhari ya milima. Kila picha ina maelezo ya tarehe, ambayo yanaonyesha wazi kwamba mgeni atakaa siku 4 huko Zion, ikifuatiwa na siku 3 huko Grand Canyon.

Nyumba mbili katika aina moja

Sehemu za Kukaa kwenye Nyumba Mbili pia hutolewa katika aina 14 tofauti, ikiwemo Kupiga Kambi, Hifadhi za Taifa, Kuteleza Mawimbini na kadhalika, ili wageni wafurahie nyumba zinazofanana au shughuli katika maeneo mawili. Kwa mfano, mgeni anayechunguza Aina ya Hifadhi za Taifa anaweza kupata sehemu ya Kukaa kwenye Nyumba Mbili inayopendekeza nyumba karibu na Zion na nyingine karibu na Grand Canyon.

Tukio moja lililounganishwa vizuri

Skrini ya simu ya mkononi inayoonyesha Kukaa kwenye Nyumba Mbili. Skrini inasema "Kaa Roma Norte na La Condesa," bei ya safari na picha za sehemu mbili za baraza zinazong'aa, zenye rangi nyingi, lakini tofauti huko Mexico City. Chini kuna kitufe kilichoandikwa "Ramani."

Uoanishaji wa kiweledi

Nyumba mbili zinapangwa kiweledi, zikilingana na eneo, aina ya nyumba na vistawishi.

Skrini ya simu ya mkononi inayoonyesha ramani ya Mexico City. Nyumba mbili zilizoonekana kwenye skrini iliyotangulia zinaonyeshwa na ikoni nyeusi zinazoonyesha tarehe za kila ukaaji. Mstari mweusi wenye uelekeo wa tao unaonyesha jinsi nyumba hizo zinavyokaribiana. Picha ndogo inarudia picha za baraza hizo mbili zenye rangi nyingi zinazohusiana na sehemu hii ya Kukaa Kwenye Nyumba Mbili.

Ramani iliyohuishwa

Sehemu za Kukaa kwenye Nyumba Mbili zimeunganishwa kwenye ramani na michoro iliyohuishwa inayoonyesha wazi umbali kati ya nyumba hizo na mfuatano wa sehemu hizo za kukaa.

Skrini ya simu ya mkononi inaonyesha picha ya sehemu ya kukaa ya Roma Norte, pamoja na taarifa muhimu za kuweka nafasi. Chini ya skrini kuna kitufe kinachomwalika mgeni "Kuweka nafasi."

Kuweka nafasi kwa urahisi

Mara baada ya mgeni kuchagua sehemu ya Kukaa kwenye Nyumba Mbili, anaongozwa kupitia mtiririko rahisi kutumia ili kuweka nafasi ya kila nyumba, moja baada ya nyingine.