Kuwa mwenyeji wa tukio kwenye Airbnb

Pata mapato kwa kuwaongoza watu kwa shughuli unazozipenda.

Tukio ni nini?

Ni shughuli ambayo inazidi ziara au darasa la kawaida, iliyoandaliwa na kuongozwa na wenyeji kote ulimwenguni. Onyesha jiji lako, ufundi wako, itikadi yako, au utamaduni wako kwa kuwa mwenyeji wa tukio.

Unda shughuli, kwa namna yako

Ziara ya chakula kwa kutumia baiskeli, upigaji picha nyakati za usiku, vyakula vya tapas kwenye mashua, au yoga (pamoja na mbuzi). Unda na ubadilishe shughuli ya kipekee ambayo watu wanataka kujaribu.

Fanya ukipendacho (na ulipwe)

Chunguza sanaa ya mtaa ama urambazaji nyakati za jioni, geuza ukipendacho kuwa faida kuu. Pata mapato ya pesa bila kuihisi kuwa kama kazi.

Pata sauti kwa shughuli yako

Ongoza matembezi pamoja na mbwa wa uokoaji, au fundisha mitindo ya maadili. Ongeza uelewa wa kusudio lako kwa njia mpya kabisa.

Onyesha unachokijua

Kuna matukio ya kila aina, kama vile kupika, ufundi, kuendesha kayaki na kadhalika. Hakuna kikomo kwa yale unayoweza kufanya. Chunguza kategoria hizi zilizoonyeshwa.

Tamaduni na Historia

Elezea hadithi kuhusu alama maarufu za kijiografia katika jiji lako.

Vyakula na Vinywaji

Wakaribishe wageni katika ziara ya chakula, darasa la kupikia, tukio la eneo la kulia chakula, na mengine mengi.

Asili na nje ya nyumba

Ongoza matembezi ya nyanjani, michezo ya majini, shughuli za milimani, na mengine mengi.

Tuko na wewe, katika hatua zote

Nyenzo kama vile makala na vidokezi mahususi kwa mahitaji yako ya kukaribisha wageni, usaidizi kwa wateja wa saa 24 kwa ajili yako na wageni wako, kuangazia tukio lako na mengine mengi, ili kukusaidia kukuza biashara yako.
Kazi
Kuratibu
Malipo
Utambuzi

Viafaa vilivyoundwa kwa ajili yako

Dashibodi kukupa ufahamu, maoni kuhusu jinsi ya kuboresha, uonekanaji kwa wageni ulimwenguni kote kupitia utafutaji na vichujio, malipo rahisi, na mengi zaidi.

AirCover kwa ajili ya Wenyeji pia hushughulikia Matukio

AirCover kwa ajili ya Wenyeji unajumuisha Dola milioni 1 za Marekani ya bima ya dhima ya Matukio endapo mgeni ataumia katika Tukio la Airbnb. Inajumuishwa muda wote bila malipo ya kila wakati.

Jinsi ya kuanza

Huu hapa ni muhtasari wa mchakato, kuanzia mwanzo hadi mwisho.

1
Jifunze viwango vyetu vya ubora

Hakikisha tukio lako linakidhi viwango vyetu vya utaalam, ufikiaji wa ndani, na muunganisho.

2
Wasilisha tukio lako

Shiriki maelezo na picha zenye ubora wa juu za kile unachofikiria ili kuonyesha jinsi tukio lako litakavyokuwa.

3
Anza kukaribisha wageni

Tukio lako litatathminiwa na ikiwa litaidhinishwa, unaweza kuweka tarehe kwenye kalenda yako kisha uanze kukaribisha wageni.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, ninahitaji kuwa na nyumba ili kuwa mwenyeji wa tukio?
La. Huhitaji kuwakaribisha wageni usiku mmoja katika nyumba au sehemu yako ili uwe mwenyeji wa tukio.
Je, muda wa kujitolea ni upi?
Unaweza kukaribisha wageni mara nyingi upendavyo—jisikie huru kubadilisha tarehe na nyakati zako mpaka utakapopata kinachokufaa zaidi.
Je, ninahitaji leseni ya biashara?
Kulingana na shughuli zinazohusika, matukio mengine yanaweza kuhitaji leseni ya biashara. Hakikisha umeangalia sheria za mitaa katika eneo lako ili uamue ni leseni gani zinahitajika kwa tukio lako, hasa ikiwa kuna chakula, pombe, au usafiri unaohusika. Jifunze zaidi