Simamia nyumba kwenye Airbnb ukisaidiwa na mwenyeji mwenza

Mtandao wa Wenyeji Wenza hufanya iwe rahisi kupata na kufanya kazi na mwenyeji mwenza mkazi mwenye ubora wa juu ili kusaidia kusimamia nyumba yako.

Wenyeji wenza wana rekodi thabiti

  1. 2x

    Matangazo ya wenyeji wenza yanapata pesa takribani mara mbili zaidi, kwa wastani, kuliko yale ambayo hayana wenyeji wenza katika nchi moja ¹
  2. 4.87

    Ukadiriaji wa wastani wa wenyeji wenza, ikilinganishwa na kampuni kubwa za usimamizi wa nyumba (4.63)²
  3. Asilimia 74

    Wenyeji wenza ambao pia ni Wenyeji Bingwa, baadhi ya wenyeji waliopewa ukadiriaji wa juu, wenye uzoefu zaidi kwenye Airbnb³
  4. Asilimia 86

    Wenyeji wenza wanaosimamia Kipendwa cha Wageni, baadhi ya nyumba zinazopendwa zaidi kwenye Airbnb, kulingana na wageni³
¹Kulingana na makadirio ya mapato ya matangazo mapya amilifu yaliyowekwa kupitia Mtandao wa Wenyeji Wenza ikilinganishwa na matangazo mengine mapya amilifu katika nchi ileile kufikia tarehe 31 Machi, 2025.

²Ukadiriaji wa mwenyeji mwenza unategemea tathmini za wageni kwa matangazo wanayokaribisha wageni au kushirikiana kukaribisha wageni, si huduma za kipekee za mwenyeji mwenza. Wasimamizi wa nyumba nyingi ni wale wenye matangazo amilifu zaidi ya 30 kwenye Airbnb ulimwenguni kote kufikia tarehe 31 Machi, 2025. Wenyeji wenza wanaweza kukaribisha wageni kwenye nyumba chache.

³Kufikia tarehe 31 Machi, 2025.

Wenyeji wenza wanahudumia nyumba yako na wageni

Pata usaidizi wa huduma kamili ambao unakidhi mahitaji yako.

Kuandaa tangazo

Kuweka bei na upatikanaji

Nafasi zilizowekwa

Kumtumia mgeni ujumbe

Usaidizi kwenye eneo

Kufanya usafi

Kupiga picha

Usanifu wa ndani

Leseni na vibali

Huduma za ziada

Wenyeji wenza wanajua jumuiya yako

Msaada wa ana kwa ana

Wenyeji wenza wanaweza kushughulikia matengenezo ya kawaida na kujibu haraka ikiwa matatizo yoyote yatatokea.

Maarifa kuhusu eneo husika

Wenyeji wenza wanaweza kukusaidia kuelewa sheria za eneo lako, ikiwemo leseni au vibali muhimu.

Ukuaji wa biashara

Wenyeji wenza ni wenyeji wazoefu wanaoelewa jinsi ya kuwavutia wageni katika eneo lako.

Hujui uanzie wapi?

Tupe maelezo machache na tutawasiliana nawe ili kujibu maswali yoyote na kukusaidia kupata mwenyeji mwenza anayekidhi mahitaji yako.

Kwa kuchagua "Pata msaada", unakubali kuwasiliana na Airbnb na washirika wake kuhusu Mtandao wa Wenyeji Wenza kupitia barua pepe au simu na unakubali Sera ya Faragha ya Airbnb na unakubaliana na Masharti ya Ziada ya Mtandao wa Wenyeji Wenza.

Maswali yaulizwayo mara kwa mara

Tafuta wenyeji wenza katika maeneo yako