Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Ninawezaje kuhariri au kuondoa njia ya malipo?

  If an existing payment method on your account is incorrect (ex: an expired credit card), you can update it or add a new payment method.

   Hariri njia ya malipo kwa ajili ya malipo yanayokuja

   Ikiwa una nafasi iliyowekwa iliyopo yenye malipo yaliyoratibiwa kwa tarehe ya baadaye, kama vile nafasi iliyowekwa ya muda mrefu, unaweza kubadilisha njia ya malipo kwa ajili ya malipo hayo ya siku zijazo yaliyoratibiwa, au ulipe mapema.

   1. Nenda kwenye Safari kisha uchague safari unayotaka kubadilisha
   2. Chini ya Umeweka nafasi gani, chagua nafasi uliyoweka
   3. Chini ya Maelezo ya malipo, bofya Pata risiti na usimamie malipo
   4. Katika Maelezo yako ya malipo, nenda kwenye Malipo yaliyoratibiwa kisha uchague Badilisha maelezo ya malipo
   5. Badilisha njia yako ya malipo kisha uchague wakati ambao ungependa kulipa
   6. Bofya Wasilisha

   Ondoa njia ya malipo

   Unaweza kuondoa njia ya malipo kutoka kwenye akaunti yako isipokuwa kama inatumiwa kwenye nafasi iliyowekwa inayosubiri au iliyo amilifu.

   1. Nenda kwenye Mipangilio ya akaunti > Malipo na kutuma malipo
   2. Karibu na njia ya malipo, bofya kitufe chenye nukta tatu
   3. Bofya Ondoa

   Weka njia ya malipo

   Unaweza kuweka kadi ya mkopo au kadi ya benki au njia nyingine ya malipo kwenye akaunti yako.

   1. Nenda kwenye Mipangilio ya akaunti > Malipo na kutuma malipo
   2. Bofya Weka njia ya malipo

   Weka njia ya malipo chaguo-msingi

   Unaweza kuchagua ni njia gani ya malipo ionekane kwanza kwenye orodha yako ya njia za malipo zilizopo.

   1. Nenda kwenye Mipangilio ya akaunti > Njia za malipo
   2. Pembeni ya njia ya malipo, bofya ikoni ya nukta tatu
   3. Bofya Weka Chaguo-msingi
   Ulipata msaada uliohitaji?

   Makala yanayohusiana