Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya
Mgeni

Upatanisho wa Airbnb wa Ubishani kwa ajili ya Tathmini

Kadiri jumuiya ya Airbnb na huduma zinavyoendelea kukua, tunaendelea kujizatiti kusasisha sera hii pale inapohitajika ili kusaidia kuhakikisha kwamba tathmini zinaonyesha mambo halisi na ya kweli ambayo wenyeji na wageni wetu wamepitia.

Tunaamini kwamba mfumo mzuri wa tathmini ni ule unaoheshimu na kulinda maoni ya kweli ya jumuiya yetu. Kwa sababu hiyo, tunachukulia kwa uzito sana uondoaji wa tathmini yoyote. Unaweza kusoma Sera ya Tathmini ya Airbnb kikamilifu, lakini kwa ufupi, hii inamaanisha kwamba tathmini inaweza kuondolewa iwapo:

Upatanishi wa upendeleo

Jumuiya yetu hufaidika zaidi wakati tathmini zinaonyesha picha isiyo na upendeleo ya uzoefu wa mwanajumuiya. Airbnb huondoa tathmini wakati zinaonyesha upendeleo usiofaa - kwa mfano, kwa sababu mtathmini anajaribu kumdhulumu mtu anayetathminiwa, ana mgongano wa maslahi, au anashindana na mtu anayetathminiwa.

Kudhulumu au kuondoa kichocheo

Jaribio lolote la kutumia tathmini au majibu ya tathmini ili kumlazimisha mtu afanye jambo ambalo si lazima afanye ni matumizi mabaya ya tathmini na haturuhusu jambo hilo.

Watu wanaotumia Airbnb hawaruhusiwi kuunganisha tathmini nzuri na ahadi za fidia au kutishia kuandika tathmini mbaya ikiwa matokeo yanayotarajiwa hayakutimizwa. Ukiukaji unaweza kusababisha kuzuiwa, kusimamishwa, au kukomeshwa kwa akaunti yako ya Airbnb.

Sera hii inapiga marufuku:

  • Wageni kutishia kutumia tathmini au ukadiriaji katika jaribio la kumlazimisha mwenyeji kurejesha fedha, fidia ya ziada, au tathmini nzuri ya kutendeana sawa.
  • Wenyeji kumtaka mgeni aandike tathmini nzuri au ukadiriaji, au kurekebisha tathmini kwa kubadilishana na kurejeshewa sehemu ya fedha, au tathmini ya kutendeana sawa. Wenyeji pia hawawezi kutoa sehemu ya kukaa bila malipo au yenye punguzo kwa kubadilishana na mgeni kurekebisha tathmini iliyopo.
  • Wenyeji au wageni kumwomba mtu achukue hatua mahususi zinazohusiana na tathmini kwa kubadilishana na utatuzi wa mabishano.

Sera hii haipigi marufuku:

  • Mgeni kuwasiliana na mwenyeji akiwa na shida kabla ya kuandika tathmini.
  • Mwenyeji au mgeni kuomba kurejeshewa fedha au malipo ya ziada na kuandika tathmini - ambapo tathmini hiyo haitumiwi kama tishio la kubadilisha matokeo ya utatuzi.
  • Mwenyeji kumwomba mgeni aandike tathmini nzuri ya kweli au ukadiriaji unaoonyesha uzoefu mzuri.
  • Mwenyeji au mgeni kurekebisha tathmini ndani ya muda uliowekwa wa kurekebisha.

Mgongano wa masilahi

Tutaondoa tathmini katika hali ambapo kuna dalili kwamba nafasi hiyo iliwekwa kwa lengo tu la kuongeza ukadiriaji wa jumla wa mtu, au katika hali ambapo tunashuku kwamba ukaaji huo haukufanyika kamwe.

Kukubali nafasi bandia zilizowekwa kwa kubadilishana na tathmini nzuri, kutumia akaunti ya pili ili kujitathmini mwenyewe au tangazo lako mwenyewe, au kutoa kitu cha thamani kwa kubadilishana na tathmini nzuri, hakuruhusiwi. Ukiukaji unaweza kusababisha kuzuiwa, kusimamishwa, au kukomeshwa kwa akaunti yako ya Airbnb.

Tathmini za washindani

Tathmini zinazoandikwa na washindani (kwa mfano, biashara shindani, matangazo, au matukio) kwa lengo la kuwashawishi wengine wasiweke nafasi kwenye matangazo au matukio hayo au kuelekeza biashara kwenye matangazo au matukio mengine, haziruhusiwi. Ukiukaji unaweza kusababisha kuzuiwa, kusimamishwa, au kukomeshwa kwa akaunti yako ya Airbnb.

Ukiukaji wa marufuku ya sherehe

Tunaweza kuondoa tathmini katika hali fulani ambapo mgeni hajakidhi matarajio yaliyoainishwa katika Sera yetu ya Sherehe na Matukio wakati wa ukaaji wake. Tunawategemea wenyeji wetu kuchukua hatua za kujaribu kuikomesha sherehe kabla haijawa tatizo la usalama au kero kwa jumuiya jirani. Hata hivyo, tunatambua kwamba kuvunja sherehe kunaweza kusababisha tathmini mbaya isivyo haki kwa mwenyeji. Ili kuhimiza uingiliaji kati na kupunguza athari za tathmini za kibaguzi, tathmini ya mgeni inaweza kuondolewa wakati mwenyeji ametoa hati za kutosha zinazothibitisha kwamba ukiukaji mkubwa wa Sera ya Sherehe na Matukio umefanyika. Hata hivyo, tathmini hizi hazitaondolewa ikiwa zina taarifa muhimu ambayo itakuwa muhimu sana kwa mgeni wa siku za baadaye.

Kupatanisha kwa ajili ya kufaa

Tathmini huwapa wanajumuiya taarifa na vidokezi ambavyo huwasaidia kufanya maamuzi bora ya kuweka nafasi. Tathmini husaidia zaidi wakati watathmini wanasimulia kwa usahihi mambo waliyopitia na kutoa maoni yao ya kweli.

Katika visa ambapo tathmini ina taarifa isiyohusiana na mambo uliyopitia kama mwenyeji au mgeni, au inazingatia kitu ambacho hakiwezi kudhibitiwa na mtu anayetathminiwa, timu yetu ya upatanishi itapima kufaa kwa tathmini hiyo kwa kuchanganua:

  1. Je, tathmini inasimulia mambo ambayo mtathmini alipitia na kutoa maoni yake binafsi?
  2. Je, tathmini hiyo ni yenye msaada kwa wanajumuiya wengine wa Airbnb? Je, inatoa taarifa muhimu kuhusu mwenyeji au mgeni, tangazo, au tukio ambayo inaweza kuwasaidia wengine kufanya maamuzi ya ufahamu zaidi ya kuweka nafasi?

Ikiwa Airbnb itatambua kwamba tathmini hiyo ina taarifa ambayo haimhusu mwenyeji au mgeni, tangazo, au tukio, tathmini hiyo inaweza kuondolewa. Tathmini ambazo zina taarifa nyingi zisizo na uhusiano pia zinaweza kuondolewa, lakini katika hali tu ambapo taarifa ambayo inahusika haitarajiwi kutoa taarifa ya maana kuhusu uamuzi wa kuweka nafasi wa wanajumuiya wengine.

Mifano ya ukiukaji wa mambo husika na hali zisizo za ukiukaji

Haihusiki: "Siwaamini madereva wa teksi katika jiji hili, wanatumia njia mbovu zaidi!"

Inahusika: "Siwaamini madereva wa teksi katika jiji hili, wanatumia njia mbovu zaidi! Zaidi ya hayo, niliwasili kwenye nyumba hii na ilikuwa katika hali mbaya kabisa na mwenyeji hakushughulikia kamwe wasiwasi wangu."

Haihusiki: "Mgeni huyu alikuwa mwongo sana. Huyu si daktari wa kweli kabisa."

Inahusika: "Mgeni aliwasili kama amechelewa kisha akanifokea kwa sababu sikuamka haraka ili kumkaribisha. Alikuwa mkorofi na alikasirika upesi kwa muda wote aliokuwa hapa. Ninachukia sana tabia zake za kulala."

Upatanishi wa nafasi zilizowekwa ambazo zimeghairiwa

Airbnb hukuruhusu kuchapisha tathmini kwa ajili ya nafasi yoyote iliyowekwa ambayo imeghairiwa baada ya saa 06:00 usiku kwenye siku ya kuingia. Tunafanya hivyo ili kukusanya maoni kuhusu pindi muhimu zaidi za kusafiri, iwe hiyo inamaanisha maoni kuhusu mawasiliano, ukiukaji wa sheria za nyumba, matatizo kwenye nyumba wakati wa kuingia, n.k.

Ukiamua kuandika tathmini kwa ajili ya nafasi iliyowekwa ambayo imeghairiwa, tunaomba kwamba maoni yako yaendane na kile ambacho umejionea mwenyewe. Katika visa ambapo Airbnb inaweza kuthibitisha kwamba tathmini iliandikwa kwa ajili ya nafasi iliyowekwa ambayo ilighairiwa na tathmini hiyo ina taarifa ambayo haihusu jumuiya yetu (kwa mfano, usumbufu kuhusu kufutwa kwa safari ya ndege, nk), tathmini hiyo inaweza kuondolewa.

Nafasi zilizowekwa ambazo zimeghairiwa

Nyakati nyingine, wageni wanaweza kupewa chaguo la kuchapisha tathmini za nafasi fulani zilizowekwa ambazo zilighairiwa baada ya saa 6:00 usiku siku ya kuingia.

Ukiamua kuandika tathmini ya nafasi fulani iliyowekwa ambayo ilighairiwa, tunakuomba uweke maoni yanayohusiana na yale uliyopitia mwenyewe, iwe inamaanisha maoni kuhusu mawasiliano, ukiukaji wa sheria za nyumba, matatizo kwenye nyumba wakati wa kuingia na kadhalika. Kumbuka kwamba ikiwa hukuingia, huenda usiwe na maoni yanayofaa ya kutoa kuhusu eneo, vistawishi au thamani. Tathmini iliyoandikwa ya nafasi iliyowekwa ambayo ilighairiwa inaweza kuondolewa iwapo taarifa iliyotolewa haina umuhimu kwa jumuiya yetu (kwa mfano, mafadhaiko kuhusu kughairiwa kwa ndege, n.k.) au ikiwa mgeni alighairi nafasi aliyoweka kwa sababu ya hali zisizohusiana na yale aliyopitia kwenye Airbnb.

Je, makala hii ilikusaidia?