Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mgeni

Kutumia vichujio vya utafutaji

Wakati mwingine unataka tu kuvinjari. Wakati mwingine, unajua hasa unachotaka. Vichujio vya utafutaji ni njia nzuri ya kupunguza machaguo yako unapotafuta sehemu ya kukaa. Ikiwa unaweza kubadilika, unaweza kuchagua tarehe na aina za sehemu ili kukusaidia ulenge utafutaji wako.

Anza na mambo ya msingi

Kwa matokeo sahihi zaidi, kila wakati anza utafutaji wako kwa kuchagua:

  • Mahali uendako
  • Tarehe za kuingia na kutoka
  • Idadi ya wageni na wanyama vipenzi

Tafuta sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja

Tumeanzisha njia rahisi zaidi ya kutafuta sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja. Gusa Miezi ili kubainisha urefu wa ukaaji wako na ubadilishe kwa urahisi tarehe zako za kuanza na kumaliza. Rekebisha tarehe zako za kuanza na za kumaliza kwa hadi usiku 14 ili kuvinjari matangazo anuwai zaidi yanayopatikana.

Vichujio maarufu

Kwa kuchagua Vichujio kwenye ukurasa wa matokeo ya utafutaji, utapata vichujio maarufu, kama vile:

  • Aina ya sehemu: Kuanzia vyumba vya pamoja hadi nyumba nzima, pata maelezo zaidi kuhusu aina za sehemu za kukaa.
  • Kiwango cha bei: Tumia kipimo cha kuteleza ili kupunguza utafutaji wako ndani ya kiwango chako cha bei. Kumbuka kwamba sehemu nyingi za kukaa ni za kipekee na sifa tofauti zinaweza kuathiri bei ya kila usiku.
  • Kuweka Nafasi Papo Hapo: Pata sehemu unazoweza kuwekea nafasi bila kusubiri Mwenyeji athibitishe.

Unaweza pia kutumia Aina za Airbnb kuchuja kulingana na matangazo ya kipekee. Chagua kutoka kwenye aina kama vile minara ya taa, nyumba za mbao au boti.

Kumbuka: Kwa sasa, kupangilia si kipengele cha utafutaji cha Airbnb, lakini unaweza kuchuja kulingana na bei ili upate maeneo yanayofaa kiwango fulani cha bei. 

Vichujio zaidi

Unataka kupata maelezo mahususi zaidi? Hapa kuna vichujio zaidi vya kukusaidia kuchagua eneo sahihi.

Vyumba na vitanda

Vyumba vya kulala, mabafu, vitanda, chagua idadi inayofaa kikundi chako.

Aina ya nyumba

Ni ukaaji wako, kwa hivyo ni kitu gani unachokipenda? Tafuta vila, hosteli, fleti na kadhalika.

Vistawishi

Baadhi ya watu wanahitaji jiko linalofanya kazi, wengine wanataka runinga na wengine wanataka maegesho ya bila malipo. Chagua kile unachohitaji ili uwe na starehe.

Machaguo ya kuweka nafasi

Punguza utafutaji wako ili upate maeneo ambayo yana Sera za Kuweka Nafasi Papo Hapo, kuingia mwenyewe au kughairi bila malipo.

Vifaa

Bwawa? Chumba cha mazoezi? Una machaguo.

Ufikiaji

Je, unahitaji mlango usio na ngazi au vyuma vya kujishikilia katika bafu? Chagua vipengele kwa ajili ya starehe na usalama.

Lugha ya Mwenyeji

Chagua Wenyeji wanaozungumza lugha unayoijua.

Sheria za nyumba

Je, unataka sehemu inayoruhusu wanyama vipenzi? Je, unapanga kuwa na wageni wowote wakazi wakati wa ukaaji wako? Tafuta maeneo yenye sheria zinazokufaa.

Sehemu za kukaa zenye ubora wa juu

Chagua kutoka kwenye aina kama vile:

  • Vipendwa vya wageni: Nyumba zinazopendwa zaidi kwenye Airbnb, kwa mujibu wa wageni.
  • Luxe: Nyumba za kipekee zilizo na ubunifu wa hali ya juu, zilizokaguliwa kwa ubora.

Kumbuka: Kwa wakati huu haiwezekani kutafuta kulingana na neno kuu.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili