Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Habari za hivi punde kuhusu COVID-19
  Ili upate machaguo ya kughairi na kurejesha fedha, chagua nafasi iliyowekwa kwenye ukurasa wa Safari. Sera yetu ya sababu zisizozuilika inatumika tu kwenye nafasi fulani zilizowekwa. Tunatoa habari za hivi punde tarehe 1 na 15 ya kila mwezi.

  Ninawezaje kuweka nafasi kwenye Airbnb?

  Unapoweka nafasi katika eneo kwenye Airbnb, unafanya mipango ya ukaaji katika nyumba ya mtu. Kila mwenyeji ana mtindo wake wa kukaribisha wageni, kuanzia na jinsi anavyopenda kujua wageni wake. Baadhi ya wenyeji hutaka kuidhinisha uwekaji nafasi, na wengine huridhika kukuruhusu kuweka nafasi katika eneo lao papo hapo bila kusubiri kibali.

  1. Kamilisha Wasifu Wako

  Katika hali yoyote, ni muhimu kujua kwamba Airbnb ni jumuiya inayotegemea uaminifu. Kamilisha wasifu wako kabla uombe kuweka nafasi na mwenyeji, ili aweze kujua kidogo kukuhusu anapothibitisha. Wasifu wako unapaswa kujumuisha picha na uthibitisho, hasa kwa sababu baadhi ya wenyeji wanahitaji wageni wawe na picha ya wasifu au Kitambulisho Kilichothibitishwa ili kuweka nafasi.

  2. Pata Eneo Sahihi

  Na matangazo ya kipekee zaidi ya 800,000 duniani kote, utataka kuhakikisha eneo unalochagua lina kila kitu unachohitaji kwa safari nzuri na ya kukumbukwa.

  Wakati unatafuta eneo, hakikisha kuwa umejumuisha tarehe zako na idadi ya wageni ili kupata bei sahihi zaidi. Soma tathmini, maelezo, sheria za nyumba, na vistawishi kwa kila eneo ili uone ikiwa ni sawa kwa safari yako. Unaweza wakati wote kuwasiliana na mwenyeji ikiwa una maswali yoyote kuhusu nyumba yake.

  3. Iwekee nafasi!

  Umepata eneo kamilifu, na sasa ni wakati wa kulifanya rasmi. Hapa ndipo njia ya kuweka nafasi iliyopendekezwa na mwenyeji itaamua jinsi utakavyothibitisha uwekaji nafasi wako.

  • Kushika Nafasi Papo Hapo

   Kwa wenyeji ambao hawataki kuidhinisha kila uwekaji nafasi, utaona kibonyezo kwenye tangazo lao kinachosema Kushika Nafasi Papo Hapo. Jinsi jina linavyopendekeza, unaweza kuthibitisha uwekaji nafasi kwenye maeneo haya moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu Kushika Nafasi Papo Hapo.

  • Omba Kuweka nafasi

   Wenyeji wengi wanapendelea kuidhinisha uwekaji nafasi kabla ya kutamatisha. Katika kesi hii, utaona kibonyezo kwenye tangazo lao kinachosema Omba Kuweka nafasi. Ili kuwasilisha ombi la kuweka nafasi, utahitaji kuweka maelezo yako ya malipo. Wenyeji wana saa 24 kukubali ombi lako, na kuweka nafasi kwako kunathibitishwa moja kwa moja wanapofanya hivyo. Jifunze zaidi kuhusu kuwasilisha ombi la kuweka nafasi.

  • Idhini za awali na Ofa Maalumu

   Ukiamua kuwasiliana na mwenyeji ili kuuliza maswali kabla ya kujaribu kuweka nafasi, mwenyeji anaweza kuitikia ujumbe wako kwa kukukaribisha kuweka nafasi na idhini ya awali au Ofa Maalumu. Idhini ya awali ni mwaliko wa kumalizia kuweka nafasi za tarehe na idadi ya wageni ulioandika katika ujumbe wako. Ofa Maalumu humpa mwenyeji fursa ya kutoa bei maalum, tarehe, na maelezo mengine ya kuweka nafasi kabla ya kuweka nafasi. Pata maelezo zaidi kuhusu kuweka nafasi ya idhini ya awali au Ofa Maalumu.

  Makala yanayohusiana
  Ulipata msaada uliohitaji?