Je, ungependa kutumia mpango wa malipo kupitia Klarna? Fahamu ikiwa unastahiki kuanza.
Ili ustahiki mpango wa malipo wa Klarna, unapaswa:
Klarna huthibitisha taarifa zako binafsi na hufanya ukaguzi wa ustahiki ili kubaini ikiwa inaweza kukupa mpango wa malipo. Ikiwa kulipa kwa awamu kupitia Klarna kunapatikana, utakuwa na chaguo kwenye ukurasa wa kukamilisha malipo ili kulipia nafasi uliyoweka kikamilifu wakati wa kuweka nafasi au kulipa kwa awamu kupitia Klarna.
Ikiwa huna Klarna kama chaguo au mpango mmoja tu wa Klarna unatolewa (kwa mfano, lipa kwa malipo 4) lakini si mwingine (kwa mfano, lipa kila mwezi) ni kwa sababu machaguo tofauti ya malipo hutolewa kulingana na muda na thamani ya nafasi iliyowekwa na nchi unayoishi.
Upatikanaji wa Klarna nchini Marekani pia ni kulingana na jimbo. Mipango ya malipo ya Klarna inapatikana pia kwa wageni ambao ni wakazi wa Kanada, pamoja na Australia, New Zealand, Uingereza na nchi mahususi barani Ulaya na inazinduliwa katika nchi mbalimbali.
Kumbuka: Nchini Marekani, Pay Monthly hutolewa kwa kushirikiana na WebBank na haipatikani huko West Virginia. Kutokana na sheria za jimbo, huko Hawaii, ufadhili wa fedha wa Pay Monthly unapatikana tu kwa ajili ya ununuzi wa zaidi ya USD 1,500. Klarna kwa sasa haipatikani katika Wilaya za Marekani (bila kujumuisha Pweto Riko). |
Ukaguzi wa kustahiki mpango wa malipo unatekelezwa na Klarna. Airbnb haina ushawishi wowote kuhusu matokeo ya ukaguzi wa kustahiki unaofanywa na Klarna. Ikiwa ombi lako la mkopo limekataliwa na Klarna, bado unaweza kulipia nafasi iliyowekwa kwa kutumia njia nyingine ya malipo.
Ni muhimu kutambua kwamba ofa ya mpango wa malipo wa Klarna kwa safari moja si hakikisho la kupewa mpango wa malipo wa Klarna kwa safari nyinginezo au kwa tozo zozote za ziada kwa sababu ya ombi la kubadilisha nafasi iliyowekwa.
Klarna haipatikani kwa sasa kwa ajili ya Matukio ya Airbnb au sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja.
Hata hivyo, ikiwa una nafasi iliyowekwa ya usiku 28 au zaidi, angalia machaguo ya mpango wa malipo kwa ajili ya sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja.
Je, unahitaji msaada zaidi? Wasiliana na huduma kwa wateja wa Klarna ili upate usaidizi wa haraka.