Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sheria

Miongozo ya Alama ya Biashara

Airbnb inahisi jukumu kubwa katika kuhudumia Jumuiya yake, ikiwemo Wenyeji, wageni, washirika na wengine wanaotumia au kukutana na tovuti na huduma zetu. Sehemu ya kuhudumia Jumuiya yetu inajumuisha kulinda alama zetu za biashara na chapa. Hatutaki Jumuiya yetu au mtu mwingine yeyote achanganyikiwe ikiwa kitu fulani kinaidhinishwa, kinadhibitiwa au kinasimamiwa na sisi. Miongozo hii imebuniwa ili kulinda chapa yetu na pia kukusaidia kushiriki habari kuhusu Airbnb kwa kuwajibika.

Miongozo hii ni sehemu ya Masharti yetu ya Huduma. Kwa kutumia huduma yoyote ya Airbnb, unakubaliana na Miongozo hii, Masharti yetu ya Huduma na sera zetu nyingine.

1. Alama za biashara za Airbnb

Alama za biashara za Airbnb zinajumuisha jina la Airbnb, nembo ya Airbnb, nembo ya Bélo, beji ya Mwenyeji Bingwa na Aircover, pamoja na maneno yote, kauli mbiu, ikoni, nembo, michoro, ubunifu na viashiria vingine vinavyotambulisha Airbnb au huduma au bidhaa zake. Tumeweka juhudi nyingi katika kuhakikisha kwamba kila kitu tunachokupa ni chenye ubora wa juu na chapa yetu inawakilisha juhudi hizo. Hii ndiyo sababu tunalinda bidhaa zetu kabisa kwa kusajili alama zetu za biashara na mwonekano wa bidhaa nchini Marekani na ulimwenguni kote. Huruhusiwi kutumia nembo ya Airbnb, nembo ya Bélo au alama zozote za biashara au ikoni za Airbnb isipokuwa uwe na ruhusa ya maandishi kutoka kwa Airbnb.

2. Kutumia jina la Airbnb

Ingawa huwezi kutumia alama yoyote ya biashara ya Airbnb bila ruhusa, unaweza kuzungumza kuhusu Airbnb au kutumia jina la Airbnb kuelezea kwa ukweli huduma unayotoa. Ikiwa ni wewe, tafadhali kumbuka kuzingatia miongozo ifuatayo:

  Iweke iwe ya kweli na yenye maelezo

  Fanya

  • Unaweza kutaja "Airbnb" pekee kwa njia ambayo inaelezea kwa uaminifu na kwa usahihi uhusiano wako na Airbnb au maudhui yako
  • Tumia "Airbnb" katika matini ya kiini (si kwa mfano, katika vichwa na vichwa vya habari) katika ukubwa, aina, rangi na mtindo unaofanana na matini ya kiini yaliyosalia pekee

  Usifanye

  • Usirejelee "Airbnb" kwa njia ambayo inadokezea ushirikiano, udhamini au kuidhinishwa.
  • Usitumie neno "Airbnb" zaidi ya inavyohitajika ili kuelezea kwa ukweli uhusiano wako na Airbnb katika maudhui yako. Ikiwa usemi au sentensi ina maana sawa bila neno "Airbnb," liondoe.

  Mifano

   Ya kweli na yenye maelezo

   Ina tatizo, inapotosha

   Sisi ni Kampuni ya Usimamizi wa Nyumba inayosimamia matangazo mengi kwenye Airbnb

   Sisi ni Kampuni ya Usimamizi ya Airbnb

   Tunatoa huduma za kufanya usafi wa kitaalamu kwa nyumba zilizotangazwa kwenye Airbnb

   Huduma za kufanya usafi wa kitaalamu kwenye Airbnb

   Tunajishughulisha na nyumba zilizotangazwa kwenye Airbnb

   Wataalamu wa Airbnb

   Vidokezi vyangu kuhusu Kuwa Mwenyeji wa Airbnb

   Semina ya Wenyeji wa Airbnb

   Epuka kuchanganyikiwa

   Fanya

   • Kubali na utumie jina, nembo na utambulisho wa chapa, ikiwemo rangi na fonti (au aina ya umbo) ambayo ni tofauti na alama za biashara na vipengele vya chapa vya Airbnb

   Usifanye

   • Usitumie nembo ya Bélo katika muundo wowote, ikiwemo kivyake au kwa kuchanganya na jina lolote la biashara, alama ya biashara, jina la akaunti ya mitandao ya kijamii au neno la kawaida
   • Usitumie "Airbnb," "Air," "bnb" au maneno kama hayo, katika jina la tovuti yako, jina la biashara, jina la bidhaa, alama za biashara, usajili wa kikoa, akaunti za mitandao ya kijamii, vipengele vya utambulisho wa chapa, n.k.
   • Usionyeshe rangi ya kipekee ya Airbnb ya Rausch katika maudhui yako, ikiwemo katika alama zako za biashara, nembo, ubunifu au vipengele vingine vya chapa

   Mifano

   Safi!

   Hapana...

   Nyumba ya Kupangisha ya Kisiwani ya Bob’s Best

   Airbnbike

   Kufanya Usafi Katika Nyumba ya Kupangisha ya Red's

   Sunbnb

   Likizo katika Anna’s Island

   Sun BnB

   rentmyskihaus.com

   Bikebandb au Bikeb&b

   Nyumba za Kupangisha za Bike and Stay

   nicebnb.com

   STR Management Co

   airmansion

   Kwa kampuni za usimamizi wa nyumba

   Ikiwa ungependa kutangaza kampuni yako ya usimamizi wa upangishaji wa muda mfupi, miongozo iliyo hapo juu inakuhusu pia. Tafadhali kumbuka pia kutojiita "Kampuni ya Usimamizi ya Airbnb," au kudai "uhusiano wa kipekee" na Airbnb ambao unaweza kuwachanganya watumiaji kuamini kwamba una uhusiano na Airbnb. Unaweza kutaja kwamba unasimamia au kuhudumia nyumba zilizotangazwa kwenye Airbnb, lakini Airbnb haipaswi kuwa lengo la tovuti yako au nyenzo nyingine za matangazo.

   Ikiwa una tovuti, lazima ujumuishe ufichuzi unaoonekana wazi kwenye tovuti yako kama ifuatavyo, "[name of your company] ni kampuni huru ya tatu na haijaidhinishwa au kuhusishwa na Airbnb au washirika wake." Ikiwa una kikokotoo cha mapato, fomu ya mawasiliano au unasaji mwingine wowote wa data ya mtumiaji kwenye tovuti yako, tafadhali onyesha kanusho hilo kwa uwazi chini ya kitufe cha CTA.

   Kwa washirika

   Washirika lazima wawe na ruhusa ya maandishi ili watumie alama zetu za biashara. Ikiwa una ruhusa ya kutumia alama zetu za biashara, unahitajika kufuata miongozo ya hivi karibuni ya chapa iliyotolewa na mwasiliani wako wa Airbnb ambaye anaweza kujibu maswali yoyote kuhusu miongozo hii au ya ziada.

   Je, makala hii ilikusaidia?

   Makala yanayohusiana

   Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
   Ingia au ujisajili