Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya

Njia zinazoweza kubadilika za kutafuta

Tafuta sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja

Unatafuta kukaa kwa muda mrefu zaidi? Tumeanzisha njia rahisi zaidi ya kutafuta sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja. Matangazo yanayokubali ukaaji wa kuanzia mwezi mmoja (usiku 28 au zaidi) yanaweza kutoa faida nyingi, kuanzia vistawishi vinavyowafanya wageni wajihisi wako nyumbani hadi bei za punguzo.

Jinsi inavyofanya kazi

Wageni wanaweza kuchagua kichupo cha Miezi ili kuweka tarehe yao ya kuanza na wabadilishe kwa urahisi urefu wa ukaaji wao kwa kutumia simu ya kibunifu.

Anza mapema kama siku ya sasa, wiki au mwezi au uchague tarehe maalumu ya kalenda, kisha utumie simu kuchagua utakaa miezi mingapi. Hata inawezekana kuchagua tarehe zinazoweza kubadilika za kuanza na kumaliza.

Matokeo ya utafutaji ya sehekmu za kukaa kuanzia mwezi mmoja yataonyesha viwango vya wastani vya kila mwezi na kurasa za tangazo zitaangazia vistawishi maarufu kwa ajili ya ukaaji wa muda mrefu pamoja na vichujio vinavyolingana na vile vya utafutaji. Wakati wa kuangalia tathmini za tangazo, zile kutoka kwa wageni waliokaa usiku 28 au zaidi kwa ujumla zitaonyeshwa kwanza.

Tafuta kulingana na Aina

Je, umefunganya na hujui uende wapi? Ikiwa wageni wanahitaji kuhamasishwa, wanaweza kuvinjari Aina za Airbnb ambazo ni makusanyo kulingana na mtindo wa kipekee wa sehemu ya kukaa, eneo au ukaribu na shughuli, ili kuwasaidia kupata sehemu ya kukaa (na mtindo) inayowafaa. Wageni wanaweza kugundua njia zinazoweza kubadilika zaidi za kusafiri—kuvinjari mamilioni ya nyumba ambazo hawakujua kwamba zilikuwepo.

Ikiwa wageni wanataka kukaa kwenye nyumba wanayotamani ya usanifu majengo (fikiria Frank Lloyd Wright), wanaweza kuangalia aina ya Ubunifu, makusanyo ya nyumba zaidi ya 20,000 zilizochaguliwa kwa ajili ya muundo na sehemu zake za ndani zilizo maarufu. Ikiwa wageni wanataka kukaa katika mazingira ya asili, wanaweza kuvinjari aina ya Hifadhi za Taifa ili kupata nyumba karibu na maeneo kama vile Hifadhi ya Taifa ya Zion na Grand Canyon.

Jinsi inavyofanya kazi

Ikiwa mgeni anatafuta mahali mahususi anakoenda, matokeo yake ya utafutaji yatajumuisha matangazo yote. Aidha, Aina zitaonyeshwa na kufanya iwe rahisi zaidi kugundua nyumba nzuri zilizo ndani ya eneo lao la utafutaji (au nje kidogo tu).

Ikiwa hawatafuti mahali mahususi wanakoenda, uteuzi wa Aina unaweza kuonekana kulingana na misimu, eneo na utafutaji wowote wa wageni wa hapo awali.

Tafuta kulingana na Kukaa Kwenye Nyumba Mbili

Je, ungependa kugawanya ukaaji wa muda mrefu kati ya nyumba mbili tofauti?

Wageni wanaweza kujaribu kutumia kipengele cha Kukaa Kwenye Nyumba Mbili, kinachounganisha sehemu mbili mfululizo za kukaa kwa kipindi cha tarehe zao na kuwaruhusu kuchunguza nyumba tofauti, vitongoji au hata maeneo tofauti ya kuzuru, wakati wa safari yao.

Kwa mfano, ikiwa wanavinjari aina ya Kuteleza Mawimbini, kipengele cha Kukaa Kwenye Nyumba Mbili kinaweza kuwaonyesha jozi ya nyumba huko Santa Barbara na La Jolla na kisha kuonyesha umbali kati ya sehemu zote mbili za kukaa kwenye ramani ili wajue mahali nyumba zote mbili zilipo (na sehemu ipi ya kukaa ni ya kwanza). Mara baada ya kuchagua Kukaa Kwenye Nyumba Mbili, wanaelekezwa kupitia kiolesura ambacho ni rahisi kutumia ili waweke nafasi ya kila sehemu ya kukaa, nyumba moja baada ya nyingine.

Soma zaidi kuhusu jinsi ya kuweka nafasi ya Kukaa Kwenye Nyumba Mbili.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili