Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mwenyeji wa Tukio

Kutumia Zoom kuandaa Matukio ya mtandaoni

Iwe ni Bingo, mwanamume anayevaa mavazi ya kike, darasa la unajimu au mafunzo ya mapishi pamoja na Mabibi wa Kiitaliano, kuna kitu kimoja ambacho Matukio yote ya mtandaoni ya Airbnb yanatumia kwa pamoja—Zoom. Mbali na kuandaa Tukio la mtandaoni kupitia Zoom, utaitumia pia kuwasilisha onyesho lako ili kuidhinishwa. Ipakue hapa.

Kurekodi onyesho lako

Kama sehemu ya mchakato wa kuwasilisha, tutakuomba utumie Zoom kurekodi onyesho la Tukio lako. Hapa kuna vidokezi kadhaa vya kufanya kurekodi kwako kuwe kuzuri.

Unaweza kutumia huduma nyingine ili kurekodi video utakayowasilisha, lakini tunapendekeza sana utumie Zoom, ili uweze kuzoea kuitumia kuandaa Tukio lako.

Kuamilisha akaunti yako mpya ya Zoom

Tukio lako litakapoidhinishwa, utakumbushwa kuamilisha akaunti mpya ya Zoom katika Mipangilio yako ya Tukio. Hii ni akaunti ya kipekee ya Zoom ambayo imeunganishwa na Tukio lako la Airbnb—akaunti hii mpya lazima itumie anwani ya barua pepe ambayo ni tofauti na akaunti yoyote ya Zoom uliyonayo tayari.

Inaweza kuchukua hadi dakika 30 baada ya kukamilisha hatua zote ndipo hali ya uamilishaji wa Zoom isasishwe.

Kukaribisha wageni

Kupata kiunganishi chako cha Zoom

Wageni wako watapokea kiunganishi cha kipekee cha Zoom kwa ajili ya kila kisa cha Tukio lako kwenye kalenda yako. Kuna njia 2 za kupata kiunganishi hicho;

  • Katika barua pepe ya uthibitisho inayotumwa kila wakati mgeni anapoweka nafasi
  • Katika barua pepe ya kumbusho inayotumwa kabla ya Tukio lako kuanza

Kuruhusu wageni waingie

Kipengele cha Chumba cha kusubiri cha Zoom hukuruhusu kudhibiti ni nani anayejiunga na Tukio lako kwa kumruhusu kila mgeni mmoja mmoja kuingia. Kwa hivyo ikiwa mgeni anashiriki kiunganishi cha Zoom na mgeni mwingine ambaye hakujumuishwa katika nafasi aliyoweka, si lazima umruhusu mgeni huyo wa ziada ambaye hakulipiwa aingie. Hata hivyo, unaweza kuomba malipo kwa ajili ya mgeni huyo wa ziada katika Kituo cha Usuluhishi.

Kutatua matatizo

Ikiwa unakabili tatizo linalohusiana na Zoom, wasiliana na Kituo cha Msaada cha Zoom. Ikiwa wageni wako wanakabili matatizo, inaweza pia kuwa muhimu kuwatumia makala hii kuhusu kuhudhuria Matukio ya mtandaoni.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili