Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Shughuli zilizopigwa marufuku

  Airbnb hairuhusu shughuli haramu na tabia nyingine ambazo zinaweza kuidhuru jumuiya yetu.

  Kile tunachoruhusu

  • Umiliki na matumizi binafsi ya bangi: Katika maeneo ambapo ni halali na haikiuki sheria zozote za nyumba, watu wazima wanaweza kutumia bangi.
  • Kulima bangi: Ambapo inaruhusiwa kisheria na ndani ya mipaka ya eneo husika, ulimaji na usindikaji wa bangi au msokoto unaofanywa na Mwenyeji kwenye sehemu yake unaweza kutokea ikiwa umefichuliwa.

  Kile ambacho haturuhusu

  • Kuwatumia watoto vibaya kingono: Kumlazimisha, kumdanganya au kumshawishi mtu aliye chini ya umri wa miaka 18, bila kujali sheria za eneo husika, ashiriki katika shughuli za ngono, iwe ni ana kwa ana au mtandaoni, kumekatazwa.
  • Biashara haramu ya kusafirisha binadamu: Kuandikisha, kuhifadhi, kusafirisha, kuhamisha au kumpokea mtu kwa nguvu, ulaghai au shuruti kwa madhumuni ya kazi au matumizi mabaya ya ngono hakuruhusiwi.
  • Kazi ya ukahaba wa kutembelewa nyumbani: Sehemu ya kukaa, Tukio au sehemu inayoizunguka hazipaswi kutumiwa kwa huduma za ngono za kulipiwa, kama vile ukandaji mwili wa ashiki au ukahaba.
  • Kununua ngono: Wageni hawapaswi kuomba na Wenyeji hawapaswi kutangaza au kutoa huduma za ngono za kulipiwa.
  • Ponografia ya biashara: Sehemu ya kukaa, Tukio au sehemu inayoizunguka hazipaswi kutumiwa kutengeneza ponografia ya biashara, picha au video.
  • Dawa haramu: Dawa haramu au zilizozuiliwa kama vile bangi, opieti, opioidi, koka na kokeni, vichocheo vya aina ya amfetamini, vigandishaji vya mfumo mkuu wa neva na halusinojeni hazipaswi kuwapo au kutumiwa kwenye sehemu ya kukaa, Tukio au sehemu inayoizunguka isipokuwa iwe kwa maelekezo ya daktari kwa ajili ya matibabu.
  • Uzalishaji au utengenezaji wa dawa za kulevya: Sehemu ya kukaa, Tukio au sehemu inayoizunguka hazipaswi kutumiwa kuzalisha au kutengeneza dawa haramu kutoka kwenye malighafi na/au mimea.
  • Kilimo cha dawa za kulevya: Sehemu ya kukaa, Tukio au sehemu inayoizunguka hazipaswi kutumiwa kukuza au kupanda mimea ambayo inatumiwa kutengeneza dawa haramu, isipokuwa bangi.
  • Usambazaji wa dawa za kulevya: Sehemu ya kukaa, Tukio au sehemu inayoizunguka hazipaswi kutumiwa kuuza, kutoa zawadi, kusafirisha au kusambaza dawa za kulevya ikiwemo bangi, hata ikiwa ni halali kufanya hivyo katika eneo lako.

  Tuko hapa kukusaidia

  Ikiwa wewe au mtu mwingine anahisi kutishiwa au kutokuwa salama au kushuku utumiaji mbaya wa watoto kingono au biashara haramu ya binadamu, tafadhali kwanza wasiliana na mamlaka za kutekeleza sheria za eneo husika ili kupata msaada. Aidha, ikiwa unashuhudia au unapitia uzoefu wa tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.

  Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kwa sera za jumuiya ya Airbnb.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana