Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Kupambana na chuki, unyanyasaji na ubaguzi

Tunataka Wenyeji na wageni wetu wawe na sehemu za kukaa na Matukio yasiyokuwa na unyanyasaji na ubaguzi.

Kile ambacho haturuhusu

  • Uonevu na dhuluma: Hakuna mtu anayepaswa kutendewa kwa namna isiyofaa, kama vile uonevu, udhalilishaji wa mtandaoni, dhuluma au kunyemelewa.
  • Kunyima huduma kwa sababu za kibaguzi: Wenyeji hawapaswi kumnyima mgeni huduma kwa sababu mgeni huyo ni wa kundi au jamii fulani, kama vile rangi au dini, kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Kutobagua.
  • Matendo ya kibaguzi: Wenyeji hawapaswi kutumia huduma, sheria na tabia tofauti kwa mgeni kwa sababu mgeni huyo ni wa tabaka linalolindwa.
  • Matamshi hatari: Hakuna mtu anayepaswa kuzungumziwa kwa lugha ambayo inaumiza, inadhalilisha utu au kudai kuwa mtu fulani ni tishio au anaweza kuwadhuru wengine kwa sababu mtu huyo ni wa tabaka linalolindwa.
  • Matusi, matamshi ya chuki au lugha ya dharau: Hakuna mtu anayepaswa kuzungumziwa kwa lugha ya kibaguzi inayohusiana na mtu mwingine kuwa katika tabaka linalolindwa, kama vile usemi wa dharau, karaha au upungufu wa kimwili, kiakili au kimaadili.
  • Kumwita mtu aliyebadilisha jinsia yake kwa jina lake la awali au kumtaja mtu kwa jinsia ambayo si yake: Watu ambao hujitambulisha kama waliobadilisha jinsia hawapaswi kuitwa kwa jina au viwakilishi vyao vya awali ikiwa wamewajulisha wengine kwamba wanatumia majina tofauti sasa.
  • Lugha iliyosimbwa au maneno ya kibaguzi yaliyofichika: Hakuna mtu anayepaswa kulengwa kwa kutumia misemo ambayo imejikita sana katika imani potofu ya kijamii kwa sababu yuko katika tabaka linalolindwa.
  • Picha, alama au vitu vyenye chuki, vya kibaguzi au vya kukera: Hakuna mtu anayepaswa kuonyeshwa picha ambazo zinadharau dini au utamaduni, picha ambazo zina lugha ya dharau/iliyosimbwa au alama, nembo au kaulimbiu zinazohusiana na makundi yenye msimamo mkali au ya chuki.

Tuko hapa kukusaidia

Ikiwa unashuhudia au unapitia uzoefu wa tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.

Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kwa sera za jumuiya ya Airbnb.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

  • Mgeni

    Kuripoti na kuzuia

    Chagua mazungumzo na mtu ambaye ungependa kumripoti au kumzuia kisha ufuate maelekezo.
  • Mgeni

    Kuwa mgeni anayejali

    Kuanzia kushiriki hadithi yako katika sehemu yako ya wasifu hadi kuweka tathmini za kweli, kuungana na wanajumuiya wengine wa jumuiya yetu n…
  • Ghairi nafasi uliyoweka ya Tukio lako

    Mara baada ya kupitia mchakato wa kughairi, utaweza kutathamini kiasi cha fedha zinazorejeshwa kabla ya kukamilisha mabadiliko.
Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili