Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Kinachotarajiwa kutoka kwa Wenyeji na Matukio yao

Matukio lazima yakidhi viwango vya ubora na usalama. Wenyeji wa Matukio lazima waonyeshe utaalamu, ufikiaji wa ndani na uhusiano, ambao husaidia kuhakikisha soko lina Matukio yenye ubora wa hali ya juu yanayoongozwa na Wenyeji wenye ujuzi na wakarimu.

Kile tunachoruhusu

 • Kuzingatia afya na usalama: Tukio linaruhusiwa maadamu Wenyeji wanazingatia sheria za afya na usalama na matakwa ya usalama.
 • Tahadhari za usalama wa chakula: Tukio lenye chakula linaruhusiwa tu ikiwa Mwenyeji atachukua tahadhari za kutosha ili kuepuka magonjwa yanayosababishwa na chakula na kukidhi viwango vya Airbnb kwa ajili ya utunzaji wa chakula wakati wa Matukio.
 • Wanyama teule: Kuingiliana moja kwa moja na wanyama kunaruhusiwa tu kwa wanyama wa kufugwa au wa shamba. Umbali salama unapaswa kudumishwa kwa ajili ya wanyama wengine wote. Wenyeji lazima wakidhi miongozo ya Airbnb kwa ajili ya ustawi wa wanyama.
 • Matukio teule yanayohusisha silaha: Tukio linalohusisha silaha za moto au silaha za visu au za kurushwa linaruhusiwa maadamu Wenyeji wanaweka Tukio hilo liwe na wageni wenye umri wa miaka 18 au zaidi, wanatii sheria za eneo husika kuhusu eneo na bima inayohitajika na wameonyesha uthibitisho wa vibali sahihi vilivyothibitishwa na mtoa huduma mteule wa Airbnb.
 • Mada teule za ngono: Wenyeji wanaweza kutoa Matukio ya mada za ngono ambayo hayakusudiwi kuamsha nyege (mfano: darasa la mazoezi ya kucheza kwenye mlingoti, picha za sehemu za siri, historia ya ngono, n.k. zinaruhusiwa), maadamu zinafanyika katika majengo ya biashara tu. Lakini, Wenyeji lazima wakaribishe tu kwenye Matukio hayo wageni wenye umri wa miaka 18 au zaidi na wafichue mada zozote za ngono (kama vile uchi), nani mwingine anayeweza kuwapo, viwango vya faragha vya eneo na awape wageni chaguo la kuondoka iwapo watajisikia kuwa na wasiwasi.
 • Shughuli za kisiasa: Matukio yanayohusisha shughuli za kisiasa yanaruhusiwa tu ikiwa yamekusudiwa kutoa taarifa na elimu wala yasijumuishe vitendo vya kisiasa vya moja kwa moja, kama vile kufanya kampeni na kuchanga fedha.

Kile ambacho haturuhusu

 • Ukatili/unyanyasaji wa wanyama: Wenyeji hawapaswi kuruhusu mwingiliano wa moja kwa moja na wanyama pori (kwa mfano: kuendesha mnyama, kupapasa, kulisha), wanyama wanaofanyishwa kazi kupita kiasi na wanyama wa nyumbani waliobebeshwa mzigo kupita kiasi na/au wanaofanya kazi au wanaotangaza na kuonyesha hafla za michezo (kama vile mbio za ng'ombe na mbio za farasi) au ununuzi au ulaji wa bidhaa za wanyama pori.
 • Mada za ngono: Wenyeji hawapaswi kuandaa shughuli za ngono kama vile kwenda kwenye vilabu vya kuonyesha uchi au kutembelea ukumbi wa ponografia. Matukio yanayoonyesha uchi na mada fulani za ngono hayawezi kufanyika katika maeneo ya makazi.
 • Michezo hatari: Wenyeji hawapaswi kuonyesha Matukio yanayohusisha kimo kirefu mno au mapango (kwa mfano: bungee, kuruka angani, kuruka kwenye helikopta, kupiga mbizi pangoni), shughuli fulani za baharini (kwa mfano: kupiga mbizi bila vifaa vya kupumulia, kuendesha tiara majini, kupiga mbizi ya kutazama papa) au shughuli fulani za kwenye barafu au milimani (kwa mfano: kupanda kwenye makorongo, kupanda kwenye barafu, kupanda milima bila vifaa vya usaidizi).
 • Kupuuza usalama: Mwenyeji lazima achukue tahadhari za kutosha na zinazofaa wakati wa kupanga na kutekeleza shughuli.
 • Matukio yanayojikita kwenye jinsia moja: Wenyeji hawawezi kuandaa matukio ya watu wa jinsia moja, isipokuwa moja wapo ya sababu zifuatazo inahusika: mahitaji ya kisheria au kiutamaduni, mahitaji ya faragha au mahitaji ya sehemu salama.

Pata maelezo zaidi kuhusu viwango na mahitaji ya Matukio ya Airbnb.

Tuko hapa kukusaidia

Ikiwa unashuhudia au unapitia uzoefu wa tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.

Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kuhusu sera za jumuiya ya Airbnb.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili