Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Kuandika tathmini zinazofaa na zisizo na upendeleo

Tunataka uwe na uhakika kwamba tathmini unazosoma kwenye Airbnb ni halisi, zinaaminika na zinafaa. Tathmini husaidia tu wakati watathmini wanasimulia kwa usahihi mambo waliyopitia na kutoa maoni yao ya kweli, yawe mazuri au mabaya.

Kile ambacho haturuhusu

  • Kupotosha tathmini: Kujaribu kushawishi tathmini ambayo mgeni au Mwenyeji ataandika kupitia vitisho au vichocheo hakuruhusiwi katika jumuiya yetu.
  • Tathmini za washindani: Washindani waliothibitishwa wa Mwenyeji mahususi hawapaswi kuandika tathmini mbaya kwa nia ya kuwazuia wageni wasiweke nafasi kwenye sehemu ya kukaa au Tukio la Mwenyeji huyo.
  • Mgongano wa masilahi: Nafasi zilizowekwa kwa madhumuni tu ya kujaribu kupotosha mfumo wa tathmini kwa kuweka tathmini bandia na ukadiriaji bandia haziruhusiwi.
  • Tathmini zisizofaa au za upendeleo: Tathmini ambazo ni za upendeleo, za kulipiza kisasi au zisizojumuisha taarifa husika au muhimu zinaweza kuondolewa.
  • Maudhui yanayokiuka: Maudhui mengine yoyote ambayo hayazingatii Sera ya Maudhui ya Airbnb hayaruhusiwi katika jumuiya yetu.

Pata maelezo zaidi kuhusu Sera ya Tathmini ya Airbnb.

Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kuhusu sera za jumuiya ya Airbnb.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili